MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
- Thread starter
- #21
Maji siku zote hayasahau njia yake hata iwe miaka elfu yatarudia tu njia yake! hofu yangu nikwamba wamsumbiji wamewafukuza wanamsumbiji wenzao! kuna uhusiano mkubwa sana wa kimaisha katika mipaka yetu ya nchi za kiafrika hususani katika lugha,vyakula na tamaduni zao! kuziingilia hizi tamaduni kwa njia neno FUKUZA ni ufinyo wa uelewa kihistoria na impact yake ni kutengeneza UADUI ambao gharama yake ni mbaya mno! mfano leo yakatokea mafuriko au vita vya wenyewe kwa wenyewe nani atampokea wa msumbiji! kungewekwa taratibu nzuri za kutokudhalilishana ili kuhifadhi hadhi ya ujirani mwema! ushauri wangu kwa wote ni huu, Tusiwe wepesi kupandikiza chuki kwani daima itakudhuru na wewe siku moja!
Dah ushauri mzuri, ila pia ungewashauri uhamiaji wa Tanzania pale ulikua una wapakia kwenye malori Wanyarwanda na Warundi waliokua wanaishi na Watanzania kwenye maeneo ya mpakani.
Nilisoma sehemu kwamba mliwafurusha hata hamkuruhusu wapakie mifugo yao, wengine wameishi hapo zaidi ya miaka 40. Kuna taarifa pia kwa jinsi mlikua na mihemko, mliishia kuwafurusha hata Watanzania wenzenu ambao walishindwa kudhihirisha Utanzania wao vizuri, hamkuwa mnawapa muda wa kuweka sawa.