Duh! kati ta wahamiaji haramu 1,634 waliokamatwa Msumbiji, 1,561 ni Watanzania


Dah ushauri mzuri, ila pia ungewashauri uhamiaji wa Tanzania pale ulikua una wapakia kwenye malori Wanyarwanda na Warundi waliokua wanaishi na Watanzania kwenye maeneo ya mpakani.
Nilisoma sehemu kwamba mliwafurusha hata hamkuruhusu wapakie mifugo yao, wengine wameishi hapo zaidi ya miaka 40. Kuna taarifa pia kwa jinsi mlikua na mihemko, mliishia kuwafurusha hata Watanzania wenzenu ambao walishindwa kudhihirisha Utanzania wao vizuri, hamkuwa mnawapa muda wa kuweka sawa.
 
Labda nikusahihishe kidogo ndugu! ukifuatilia vyema utaelewa anayefanya mazoezi au utekelezaji huu sio RAIA bali ni vyombo vya dola! hivyo nadhani haipendezi kutumia sentensi za majumuisho utakuwa hutendi haki! kwa 100% raia kwa raia wa pande mbili za nchi jirani ndio hutengeneza joto la upendo na kukaribishana ila anayehoji uhusiano huo ni serikali,kwanini huoji? bila shaka ni kwa misingi ya katiba zao! si ilaumu Tanzania kwa jinsi ilivyo nyumbani kwa kila aliyepakana nasi,ila kilichotokea kama ulivyo andika nadhani kulikuwepo na kukithiri kwa wakaazi au wahamiaji au ndugu zetu walio tumia fursa hiyo ya UPOLE wa tanzania kuanzisha vitendo vya ujambazi na uporaji nk! Msumbiji wamefanya ya kwao,ila sisi hatujambugudhi hata mmoja wao! hili ni somo pia! Sio kwamba hawapo!
 
Zipo sheria za uhamiaji.Kama waliingia huko bila kufuata sheria ni sawa kuwafukuza.Watu ni lazima wafuate sheria.
 
Siungi mkono uhamiaji haram, ila najiuliza tu kuhusu hizo takwimu kukosa mmalawi hata mmoja!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…