Duh! Kumbe Zanzibar ilikuwa na Sultan mwenye asili ya Oman aliyekimbilia uhamishoni baada ya Mapinduzi mpaka mwaka 2021

Wakati wazanzibari wanataka kujitenga msisahau kuna wapemba na waunguja, hawa waunguja wakiwa Bara wanasema wanaenda Zanzibari na wapemba wakiwa Bara wanasema wanakwenda Pemba.

Hapo tayari kuna mgawanyiko unao ongeza nyufa za matabaka ya kinchi, na ipo siku endapo Zanzibari ikijinasua kutoka JMT basi wapemba nao watapambana kutoka kwenye kifungo cha kutengwa kisaikolojia kama si kiuchumi.

👉🏾 Bado naendelea kujifunza.
 
Kwani kati ya Jamsheed na Shamte ni nani alikuwa na madaraka makubwa ya kiutendaji huko Visiwani kabla ya mapinduzi ?
 
Rais Salimini Amur alishawakaribisha zamani sana. Hata kijukuu cha Princess Salme binti Said ambaye aliolewa na Mjerumani alikuja kutembelea Zanzibar na kupigiwa bonge ya shoo ya taarab.
 
Hapa naeleza kama historia tu nisijeambiwa nataka kutenganisha visiwa hivi viwili vikubwa.

Pemba ilikuwa chini ya utawala wa Mazrui wa Mombasa mpaka alipokuja huyo Seyyid Said kutoka Oman na kupigana na Mazrui na kuwashinda ndiyo akakiweka chini ya utawala wake pamoja na Zanzibar.

Hiyo ilikuwa (kama sijakosea) 1820 kabla hata ya kuhamisha makao yake makuu Unguja.

Mabaki ya utawala wa Mazrui bado yapo Pemba kaskazini.
 
Kwani kati ya Jamsheed na Shamte ni nani alikuwa na madaraka makubwa ya kiutendaji huko Visiwani kabla ya mapinduzi ?

..nadhani katiba yao ilikuwa inamtambua Sultani pamoja na kwamba Waziri Mkuu ndiye aliyekuwa akiongoza serikali.

..nakushauri utafute taarifa za Znz kujiunga na umoja wa mataifa utaweza kujua walikuwa na utawala wa aina gani.
 
Hapa ndipo ugomvi wa muungano ulipo.ila usisahau yule Bibi wa uingereza anasema tanganyika na Zanzibar ni zake.kwa hyo muungano hataki uvunjike mtavunjika nyie muungano utabaki
Tang na znz ni zake wakt zilishapata uhuru mwaka 61 😀😀😀
 

Mkuu unajidanganya sana, Wapemba hawawezi kujitenga na Zanzibar, Mana Bila ya Muungnao Zanzibar lazima itaongozwa na wapemba.
 
Nyie watoto manunda kweli kweli.
Historia hamsomi?
Kwani mapinduzi ya 1964 mnafikiri yalikuwa nani kumpindua nani?
Hivyo vitabu vy historia vya kwenye syllabus kuna sehemu vinasema Sultan aliyepinduliwa alikuwa bado sultan wa Zanzibar uhamishoni Uingereza?
 
Hivyo vitabu vy historia vya kwenye syllabus kuna sehemu vinasema Sultan aliyepinduliwa alikuwa bado sultan wa Zanzibar uhamishoni Uingereza?
Usultani ni himaya, kama Mkuu wa Mkoa.
Kama huna mkoa utaitwaje Mkuu wa Mkoa?
 
Msilete longolongo rudisheni kilomita kumi kuanzia kenya hadi Ntwala,Ukanda wa kilomita kumi ni milki ya Zanzibar,pato mnalopata kutokana na ukanda huo ni pato la haramu na ndio maana Tanzania haiendeleinyote mnajua hela inayopatikana kwa njia za haramu haidumu na haina faida,mnaona masonga mbele kumbe mna ludi nyuma.
 
Retire hii haina maana ya kustaafu.
 
Baada ya Seyid Said watoto wake waligombana,ikabidi wagawane,mmoja akabaki kutawala Oman mwingine Zanzibar.Wakawa mahasimu na ndo maana Jamshid alishindwa kuingia Oman hadi 2021.
 
Oman ni ndugu zetu. Ule uasi wa mwaka 1964 uliofanywa na mganda John Okello na wenzake waliopewa silaha na Nyerere ili waje kuuwa ndugu zetu tunaupinga na tunaulaani.
 

..hata Oman ni mali ya Zanzibar.

..Oman ilitenganishwa na Zanzibar kwa HILA baada ya Sultani kufariki.

..ukanda wa Pwani wa kilomita 10 uliuzwa kwa Wajerumani na mmoja wa Masultani wa Zanzibar. Kwa msingi, huo ni sahihi ukanda huo kuwa miliki ya Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…