Duh! Kumbe Zanzibar ilikuwa na Sultan mwenye asili ya Oman aliyekimbilia uhamishoni baada ya Mapinduzi mpaka mwaka 2021

..nadhani katiba yao ilikuwa inamtambua Sultani pamoja na kwamba Waziri Mkuu ndiye aliyekuwa akiongoza serikali.

..nakushauri utafute taarifa za Znz kujiunga na umoja wa mataifa utaweza kujua walikuwa na utawala wa aina gani.
Cheo cha Sultan kilikuwa cha sherehe tu.
Shamte alikaa madarakani chini ya miezi 2.
Kabla ya hapo utawala ulikuwa wa Muingereza.
 
Cheo cha Sultan kilikuwa cha sherehe tu.
Shamte alikaa madarakani chini ya miezi 2.
Kabla ya hapo utawala ulikuwa wa Muingereza.

..taarifa mbalimbali zinasema Znz ilipewa uhuru 1963 na kuwa CONSTITUTIONAL MONARCHY.

..sasa labda tuangalie ktk mfumo huo Sultani na Waziri Mkuu walikuwa na madaraka gani.
 
Nimecheka sana...🤣
 
Kabla ya Waarabu kuja Zanzibar Waomani Zanzibar iliuwa inakaliwa na watu weusi.

Kuna kitabu, ''Omani Sultans in Zanzibar,'' (1988) kimeandikwa na Ahmed Hamoud Al-Maamiry.

Katika kitabu hiki anaeleza kuwa Waarabu walifika Pwani ya Afrika Mashariki miaka mingi sana kabla ya Wazungu na Wareno walipowasili 1498 waliwakuta Waarabu ni wenyeji sehemu hizo pamoja na hii Zanzibar.

Wareno waliikalia Oman kutokea India mwaka wa 1508 na mwaka wa 1650 Waomani walifanikiwa kuwatoa nchini kwao.

Wazanzibari wakaomba msaada Oman iwasaidie kuwaondoa Wareno nchini kwao na hili lilifanyika bila ya sharti yoyote.

Waomani waliizingira ngome ya Wareno Fort Jesus kwa siku 33 na mwisho Wareno walisalimu amri na kuondoka Pwani ya Afrika ya Mashariki 1698.

Hivi ndivyo walivyopatikana masultani 12 waliotawala Zanzibar.

Lakini muhimu ni lazima utambue kuwa kufikia hapo Waarabu na Waafrika walioana na hivi leo ndiyo unawaona Wazanzibari hawa waliochanganya damu.

Kwa bahati mbaya wapo wasiopenda hili na kulifumbia macho wakitaka kizazi hiki kinachokwenda nyuma karne na karne kionekane kuwa Zanzibar si kwao kwao ni hawa Waafrika tena wametokea Tanganyika haizidi hata miaka 100 kiasi ukimuuliza wapi kaburi la babu yake hana pa kuonyesha.

Ndiyo hawa leo wanauliza kabla ya kuja Waarabu Zanzibar walikuwa wanaishi watu gani?

Jibu nimelitoa kuwa katika visiwa hivi wakiishi watu weusi na hawa watu weusi wakachanganya damu na Waarabu na ndiyo hawa Wazanzibari waliopo Zanzibar hivi sasa karibia karne saba.

Mzanzibari Riyami ana damu ya Kimanyema. Mzanzibari Barwani ana damu ya Kimakonde.

Wapo wasiopenda hili na ipo sababu lakini hawana ujasiri wa kusema
 
Hao wamanyema walivukaje bahari mpaka Zanzibar?
 
Vipimbi nyie hamsomi hata historia ya nchi yetu na tulikotoka.
 
..kuna aliyefuatilia picha za Masultani wa Znz?

..kuna wengine ni WAAFRIKA kabisa.

..hata kuwaita waarabu-koko ni kuwaonea.

..inawezekana mama zao ambao inasemekana walikuwa Waafrika walikuwa na damu kali sana.

..au baba zao Waarabu walikuwa wakisaidiwa na Waafrika ktk masuala ya " kufyatua"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…