Duka la mangi vs men salon

Duka la mangi vs men salon

Kufungua duka la mangi halafu kumuachia mtu alisimamie ni uono, usimamizi wake huwa unachangamoto, uaminifu ni hafifu siku hizi..

Bora salon, unampa malengo kwa siku akuletee kiasi gani utayoona ina unafuu kwako na hata mshahara unaweza kukubaliana kutomlipa tofauti na mangi shop ambayo mwisho wa siku dogo atataka umlipe ama lah akuibie kila siku na hutojua.
Hii ndio changamoto kubwa.
 
Sijajua uko wapi, ila salon ya kiume ukiwekeza kwenye vitu viwili vikubwa, lazima upate hela especially kama upo kwenye miji mikubwa.

UFUNDI: Lazima uwe na vinyozi wazuri na mafundi haswa kiasi kwamba kila mteja anaekuja anatoka amefurahi. Kumbuka wanaume wengi akipata kinyozi anampatia huwa hahami kwa urahisi.

HUDUMA: Hapa tafuta pisi kali kwa ajili ya kuosha wateja baada ya kunyoa, kufanya scrub, kusafisha miguu, kucha etc. Mnakubaliana kwa kila huduma mteja anayofanya, mnagawana kiasi kwa sababu materials unanunua wewe. Na hapa ndio pesa ipo kuliko hata kunyoa. Bei ya wastani ya kunyoa kwa sasa ni 5000 kwa kichwa ila mtu akifanya scrub na massage ya kichwa akaweka na black kichwani unazungumzia 25k hapo.


Biashara itakua nzuri zaidi ikiwa hao wadada watakua niaje. Ukiwatoa Singida au Manyara itapendeza zaidi na hela utaiona. Hakikisha umeweka parking ya kutosha na kachuma ka kufanyia massage weka bafu.​
NAKAZIA
 
Back
Top Bottom