Dullah Mbabe: Mabondia wa Tanzania msiende Urusi na Kazakhstan

Dullah Mbabe: Mabondia wa Tanzania msiende Urusi na Kazakhstan

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Bondia wa Tanzania Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe amesema hawezi kwenda tena kupigana nchini Urusi na Kazakhstan kwa sababu mabondia wa kule ni wakali sana.

Pia amewatahadharisha mabondia wa Tanzania wanaokwenda kule kuwa mabondia wa nchi hizo huwa hawapoi na huwa wanapiga ngumi kama mawe.

Abdallah Pazi alikuwa na Pambano nchini Urusi Mei 20, 2021(Haijathibitika kama ataenda).

Hivi manpakiao (kama nimekosea jina lake mniwie radhi) ni wa nchi gani, mana naye alikuwa na ngumi jiwe, kumuumua mtu uso ilikuwa ni jadi yake.
 
Ulaya ya mashariki yote ile ni balaa,Ukraine na Rusia ndo funga kazi,unapigwa ngumi na kijimtu chembamba kama rula lakini uzito wa ngumi kama gurudumu la treni.
Mazoezi na lishe..walimu wazuri, vifaa vizuri na vya kutosha, mazingira mazuri ya mazoezi... Team kamili iliyojaa wajuzi kama
Mwalimu wa viungo
Mwalimu wa ngumi
Mpishi
Daktari
Mtaalam wa saikolojia
Mtaalam wa mavazi nknk
 
Afrika ya kaskazini pia yana miili mikubwa, kwa boxing fighters je! refer wachezaji wa mpira, Algeria, Egypt, Morocco n.k ni hatari
 
Bondia wa Tanzania Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe amesema hawezi kwenda tena kupigana nchini Urusi na Kazakhstan kwa sababu mabondia wa kule ni wakali sana.

Pia amewatahadharisha mabondia wa Tanzania wanaokwenda kule kuwa mabondia wa nchi hizo huwa hawapoi na huwa wanapiga ngumi kama mawe.

Abdallah Pazi alikuwa na Pambano nchini Urusi Mei 20, 2021(Haijathibitika kama ataenda).

View attachment 1790388
Russia wana utamaduni wakucheza wrestling na boxing kama michezo ya kawaida, ndio maana wanaongoza kwa Street fighting. Huku kwetu mpaka mtu kakomaa ndio anakuja kujifunza boxing tena kwasababu ya hali ngumu ya maisha. Naona wa Nigeria nao wameanza kutumia nguvu yao ya kula Cassava kupigana UFC na wanafanya vizuri nao wanautamaduni wa traditional wrestling kwaiyo by nature ni fighters pia lakini uku kwetu niishie hapo tu [emoji23]

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom