Hbr wakuu hivi haya malalamiko ya mr misifa juu ya baadhi ya wasanii kutohudhuria mazishi ya baba yake na kudai kuwa hawamjali na kusisitiza kuwa wengine wanajifanya kumuita brother lakini hawakutokea na kudai kuwa sasa ashajua nani mkweli kwake na nani sio mkweli Je malalamiko yake yana msingi
Source; Amplifaya ya clouds
==========
==========
Source; Amplifaya ya clouds
==========
==========
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, ameshangazwa na kitendo cha wasanii wengi kutojitokeza katika mazishi ya baba yake mzazi, Ebby Sykes
"Nilitegemea kwakuwa tunampumzisha baba yangu hapa hapa Dar es Salaam, wangekuja wasanii wengi ambao ni marafiki zangu, lakini hali ilikuwa tofauti kabisa," .
"Sijui walijua nitakuja kuwaomba fedha zao, mimi nilishapata michango mingi kutoka kwa watu wengine mbalimbali, ukweli wasanii tuache roho za kimasikini," alisema.
Sykes aliendelea kusema amegundua asilimia kubwa ya wasanii wamekuwa wakipendana wakati wa raha tu, lakini inapofika muda wa matatizo kila mmoja hukimbia.
Chanzo: EATV