Dully alaumu wasanii ambao hawakuja kumzika baba yake

Kwa upande wangu kweli ukiona watu wamekuja katka msiba unaokuhusu unapata faraja sana.
Ila in another way around Dully asiwalaumu sababu msiba sio kitu cha kuplan kbs na hapa mjini kila mtu anaratiba zake.Msiba ulitokea j2 nadhani j3 akazikwa hapo kwa upande wangu ni so fast.Ila pia kutokana na imani yke ilimlazimu kufanya hivyo.
Hata yeye msaani mwenzake akifiwa na ndg yake Nangwalengwale huko mtwara vijijini ataweza kwenda ghafla?Waliofika angewashukuru waliokosa inawezekana sio walidhamiria au kwa vile staa alitaka pale Kisutu pasitoshee watu:heh:
 
Diamond pia anaplan zake kama alituma mwakilishi jee?Watu kama nani tena yeye kila msiba yupo huu sijui alikuwa wapi hadi akaukosa ?Yap nimekumbuka alikuwa kuleee kwa yule dogo alipewa shavu kama la Mswati......:lol:
 
Wabongo kwa maneno kwan ni lazima aende kwenye mazishi si ataenda hata kuhan loo na hamumshushi ng'oooooooo

halafu nimeshangaa hata duli mwenyewe eti kalalamika kuhusu hili... hadi nkajiuliza inamaana yy alikuwa anahesabu watu waliohudhuria. hivi mtu unavyochanganyikiwa na msiba unaweza kubother eti fulani kaja fulani hajaja? mie sio fan wa dangote bali kwa hili hapana...wamwache apumuwe
 
ifike mahali wabongo tujifunze, yani watu wasipokuja kwenye mazishi ya baba yako basi unaita media unalalamika, sasa unalazimisha klila mtu ahudhurie mazishi ya baba yako? wengi wana shughuli zimewabana kama wameshindwa kufika siku ya maziko basi watakuja kukupa pole siku wakipata nafasi
 
inategemea kama na wewe unaendaga kwa watuuu au unalalamika tu funga domo lako
 
Sio lazima waje siku ya mazishi. Mtu anaweza kuja hata siku nyingine kukupa pole. Maisha magumu ni tight leo upo jijini kesho msiba unatokea afu wewe upo mkoani
 
Kwani asipokuja yeye ndio nini? au kwanini mnapenda kumsema mtu bila sababu za msingi? ivi ni chuki binafsi au kitu gani? walokua dar wamekwenda wangapi kuzika mpaka mumtie mdomoni yeye alokua Zanzibar? ebu semeni ukweli msizue,
sasa hiyo covereji mnaoingelea si ndio hiyo mnayo mpa? punguzeni roho mbaya na choyo ombeni na nyie mtapewa..
 
Mbona wameshindwa kuwasema hao mastaa walio mchana Diamond? Mimi ninacho jiuliza mastaa wote akiwemo Dully wamewai kuhudhuria misiba yote?

Haya ni mambo ya kitoto kabisa kuamza kuwalaumu watu kwasababu ya kutofika msibani wakati hatujui ni sababu gani na haya ameyaanzisha mfiwa Dully ... Kwani huu msiba ulipangwa mpaka watu wote wahudhurie?
 
Bora umewaambia ukweli
 
Huyu Dully ana mambo ya kitoto sana ndio maana hadi sasa ana nyoa kiduku!
Ninacho jiuliza.
Alikuwa anafanya sensa?
Msiba ulipangwa?
Msiba umekuwa show?
Yeye amehudhuria misiba yote iliyotoke?
Yani mtu ana walaumu watu utafikiri alipanga baba yake atakufa lini na alishagawa kadi! Hivi ni kweli kila mtu anaweza kuhudhuria msiba kila unapotokea? inamaana watu wote wana kuwa na nafasi kila muda? Hapa yeye ndio kaonesha roho ya chuki na umaskini maana ameshindwa kujiuliza nje ya anayo yafikiri!
 
Kuzika kiislam ni sunnat kifaya,usipoudhuria no prblm kama unasababu za kimsingi,ila kibinadam kama huna sbb za msingi yakupasa uende kumtia moyo mwenzio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…