Dully Sykes-DHAHABU /Joselini v/s mr blue

Dully Sykes-DHAHABU /Joselini v/s mr blue

Pale unavyoanza napenda sana. Zamani nyimbo zilikua nzuri na mabiti yasiyokinaisha
Wote walikaza sana, ila dully kiboko japo alipambana na vijana wenye mitindo mipya ya kurap ila aliwakilisha vema. Hii collaboration inanikumbusha wimbo unaitwa NILIKATAA kutoka top band, TID, QChief ft Byser
 
Producers wa zamani walijua kupika mziki
Daah Joslin huyu jamaa ana mtindo fulan hivi matata sana anapo flow.
Mr blue aliweka mbwembe nyingi mnoo.
Ila ilikuwa ngoma kali Sana.
Dully humu mimi naona alifunikwa japo alijitahidi sana.

Ila yote tuseme lakini baba lao ilikuwa ni ile beat yake daah.
 
Producers wa zamani walijua kupika mziki
Saana yani, hii ngoma ilikuwa kali Sana kwenye biti hapo Master J ameitendea haki kabisaa.
Kulikuwa na biti kali nazikumbuka kama ile ya
Nikusaidieje ya Prof Jay
Starehe
Kuna ile bembeleza ya Marlow
Ingewezekana ya Squeeze na Ray c
Balozi kwenye chati
Understanding ya banana na Jaydee
N.k
 
Sasa mkuu hyo si nyimbo tu. Naamini pia Kuna nyimbo zimetoka mwaka huo 2006 pia km binadamu huzifahamu 😅😅
Kweli Ila sio kwa hii mkuu, mana ilikuwa kama nyimbo ya taifa vile yani.
Hapa nikikutajia nyimbo kama.
Wajua Kiba na Queen darlin
Distance ya Jadee
Latifa, Inamaana, waja za Mb doggy
Una Prof Jay
Ndugu zangu Afande sele
Zawadi Keisha
Agoust 13, mwanza mwanza za Fid
Zali la mental
N.k
Ukisema huzijui hizi nitakushangaa kidogo mkuu hapo itabidi tu nikuulize umri wako mkuu.
 
Dah.. ngoma ya kidunia hiyo.. Ilitendewa haki na kila mshiriki
 
Hii ngoma inatoka enzi hizo Niko secondary form 4 Pale mbeya zile top 20 za clouds ijumaa tumetoka darasani saa 6 tunangoja ubwabwa aka nyali na viredio vyetu vya betri [emoji1787][emoji1787][emoji1787]Basi ikifika namba moja dhahabu imeshika Wana walikuwa wanafurahi balaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
U-lonely tena bye, mi nafurahi
Niko stimu za mjani, kichwani niko high
Namuona manzi maskani, yuko so fly
Mi nawahi, najigeuza Dully namfuata nampa hi
Nimeshaini kama Mully, kadata mtoto hakatai
(Heheh heheh)
Anang'aa kama gold (yeah, yeah)
Yeah, yeah, yeo-yeoh yeoh, yeo-yeoh
Anaita kama bling thing
Kama dhahabu, amefika kwa king
Queen wa Kheri Rajabu
Anakila sababu, asipate tabu
Nimezimika ajabu (sana tu)
Heheh
Yeoh, hapendi pesa, hapendi show
Ye anampenda Blue
Washamteta hasemi no
Ye anaona fool
Ndo mama Kabyser ajulikana mpaka kwetu
Steve unataka kumjua?
Master J twenzetu
Hii verse Bluu alitisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote walikaza sana, ila dully kiboko japo alipambana na vijana wenye mitindo mipya ya kurap ila aliwakilisha vema. Hii collaboration inanikumbusha wimbo unaitwa NILIKATAA kutoka top band, TID, QChief ft Byser
Mr atabaki kua underrated heavyweight mc ever
 
Wote walikaza sana, ila dully kiboko japo alipambana na vijana wenye mitindo mipya ya kurap ila aliwakilisha vema. Hii collaboration inanikumbusha wimbo unaitwa NILIKATAA kutoka top band, TID, QChief ft Byser

Huu wimbo Blue aliwafunika wote japo napenda TID anavyoteleza na sauti!

Enzi zake Blue ukimpa kolabo ukienda vibaya wimbo unakuwa wake! Sijui kwa sasa
 
Hii ngoma nilikuwa naisikiliza kwenye dvd player fulani hivi kuna mtoto wa kigogo alikujaga nayo skuli enzi hizo form four.

Mr Blue is my all time Bongoflavour artist. Kuna vyuma ananyuka hata zama hizi, kama ile Mbwa Koko aliyofanya na T- Touch.
Producer anayepatia midundo ya bongo hiphop kwa miaka ya karibuni.

Alexander The Great
 
Blue anamaliza hivi...

Steve unataka kumjua?, Masta J twen-zetu..,
 
Huu wimbo Blue aliwafunika wote japo napenda TID anavyoteleza na sauti!

Enzi zake Blue ukimpa kolabo ukienda vibaya wimbo unakuwa wake! Sijui kwa sasa

Alikua hafai Blue. Unakumbuka alivompoteza PNC kwenye Mbona, au Gorilla Killers kwenye Jonita? Au Mimi Wewe Mimi Nitakufa na Wewe alivompoteza Abby Skills?

Huyu dogo alikua fire tokea kitambo sana. Hajawahi kuchuja pamoja na kubadirisha sana flow.

Wakina Joseline yaliwapoteza makundi makundi, MB Doggy, Makamua, etc. Blue one man army kitambo na yupo Hadi kesho.
 
Back
Top Bottom