Dully Sykes-DHAHABU /Joselini v/s mr blue

Hatari sana aisee.. ngoma kali halafu wasanii ni Blue+Joslin na Dully moto sana hawa watu kipindi hicho.
Sjui Joslin yuko wapi.. huyu jamaa alikuwa na maneno flani ya swaga vijana wengi tuliyatumia kutongozea madem kitaa.. ngoma yake ya Pafyum hatar sana.
Huyo Blue sasa mpaka kesho ntazid kumuelewa... kosa tu apewe hata sekunde 30 kwenye songi anaua balaa.
 
Wadau wa JF wanasema Joslin anakaanga kiepe [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka huo nilikuwa Form one Morogoro secondary
 
Blue aliitambalizia hii verse kizazi sana
 
Pale unavyoanza napenda sana. Zamani nyimbo zilikua nzuri na mabiti yasiyokinaisha
Nyimbo za zamanio zilikuwa na Swag kama mbele yaani.

Sijui tuliyumba wapi.

1.

2,
3.
 
Kabla ya huu wimbo kulikua na hali ya 'bifu' ( sikuthibitisha) kati ya Mr Blue na Joseline, ikumbukwe Jose kamkuta Byser kwenye 'industry' lakini wakati Jose anaingia kwenye 'game' ni kama Blue alikuwa anapotea kwenye ramani.

Joseline akaachia mikwaju hatari kama Perfume, Mshkaji mmoja, etc... Later on Mr Blue akaja na NIPO feat Q Chilla bonge moja la wimbo huu. Sasa humu kwenye Nipo Blue ni kama alikuwa anafloo vile Jose anafanya. Kurap kwa Swags! Nafikiri tatizo likaanzia hapo.

Na ikumbukwe pia Mr Blue na Dully walikua washkaji sana wakati ule, marafiki walioshibana sana tu. Inasadikika Dully alipanga kuprove wrong watu kuwa Jose na Blue ni watu wawili tofauti kabisaa kwenye uandishi hata floo.

Japo nasikia wazo la hiyo 'Collaboration' Blue aliambiwa mapema tu hivyo alijiandaa vizuri tofauti na Joseline. Btw! Jose aliitendea haki nafasi yake kwa floo ambayo ilimtambulisha yenyw unyamwezi mwingi.

Blue nafikiri kwasababu ya kutaka kujitofautisha zaidi na Jose ikabidi azidishe swags sana kwenyw dhahabu ili ionekane kila mtu anapita njia yake. Kadri miaka ilivyokwenda ndio Rap Style ya Blue ilikua inabadilika hadi huyu wa sasa katika Pombe na Muziki.

Nimejaribu kurudisha kumbukumbu nyuma, moyo u radhi kurekebishwa.
 
Wote walikaza sana, ila dully kiboko japo alipambana na vijana wenye mitindo mipya ya kurap ila aliwakilisha vema. Hii collaboration inanikumbusha wimbo unaitwa NILIKATAA kutoka top band, TID, QChief ft Byser
Kabla ya kwenda kuingiza vocal Blue anakuambia alifanya mazoezi week nzima kama unavyojua zamani walikua wanazinatia sana...... Siku ya kurecord sasa pale MJ Rec Blue anaingia booth anapia averse yake, ile anamaliza tu watu wote waliokuwepo pale studio walisimama kupiga makofi
 
Woyiiioooooo piga kelele kwa joslin ake weweeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biti la ngoma ya Ngwea A.K.A MIMI ni noma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…