Dully Sykes: Hawa wamesahaullika?

Dully Sykes: Hawa wamesahaullika?

Hao WALIKUWA wacheza shoo wa TANU, hamna haja
tunapaswa kuheshimu watu waliojotolea maisha yao ili wengine waishi kwa uhuru na amani, kwa akili yako fupi unaonekana hata darsani mwalimu wako darasani alikuwa n shida
 
suala tunalizungumzia ni utaifa sio wadhifa wa kupora
Jukite kukaanga mihogo barabarani
Kweli isee maana kuna dk mihogo anasifika kweli japo yupo ughaibuni,

Mihogo deal sana kwa msaka tonge
 
Yaani ukiwataja hawa ndugu kwenye history ya Tanganyika na Uhuru basi hutokwepa kusema namna Uislam ulivyoleta Uhuru maana hao wenzao enzi hzo walikuwa kama wale wazee wa ndiooo wa miaka hii
 
Yaani ukiwataja hawa ndugu kwenye history ya Tanganyika na Uhuru basi hutokwepa kusema namna Uislam ulivyoleta Uhuru maana hao wenzao enzi hzo walikuwa kama wale wazee wa ndiooo wa miaka hii
Tutuo,
Huwezi kuukwepa Uislam katika mapambano dhidi ya ukoloni.

Ukisoma historia ya Vita Vya Maji Maji utakutana na ''symbols,''
nyingi za Uislam.
 
Huko Makerere kwenyewe Watanganyika walikuwa wakuhesabika hicho chama kingekuwa cha Waganda?
Sasa toa maelezo basi ilikuwaje kama unafahamu vizuri...na ueleze ni vipi walimtumia Nyerere barua Makerere ya kutambulisha chama (TAA)
 
Sasa toa maelezo basi ilikuwaje kama unafahamu vizuri...na ueleze ni vipi walimtumia Nyerere barua Makerere ya kutambulisha chama (TAA)
Fyatu,
Nyerere
hakuandikiwa barua na yeyote katika TAA wala hakuwa akijulikana
kama mwanasiasa hadi alipofika Dar es Salaam na kujiunga na wanaharakati
waliokuwa viongozi katika TAA.

Soma kisa hiki hapo chini kitakupa picha ya siasa zilivyokuwa Dar es Salaam
ya mwaka wa 1950:

Huyo Bi. Mkubwa ni Mama Daisy.
Huyu mimi ni mama yangu.

toW0HLKw0_eZRKHUURD38LIxZWcW5RXD7goNoYJWFVWEj8kMEyL1bPXqHWB5CmfrXmD1mA=w329-h566-no

Kushoto: Mama Daisy, mbele ni Bi. Titi Mohamed
na kushoto yake ni Bi. Zainab mkewe Tewa Said Tewa
katika maandamano siku za mwanzo za uhuru

Jina lake ni Mwamvua biti Masha.

Lakini kwa watu wa Dar es Salaam akivuma kwa jina la binti yake
Daisy kwa hiyo akijulikana kama Mama Daisy.

Ingekuwa si huu uhusiano wa kindugu Mama Daisy asingenieleza
chochote katika historia ya mumewe marehemu Abdulwahid Sykes.

Wakati ule watu walikuwa wakiogopa sana kusema lolote lililo kinyume
na historia ambayo watu walikuwa wameaminishwa.

Jina la Abdul Sykes na mdogo wake Ally na wazalendo wengine kama
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi, Tatu bint
Mzee, Iddi Faizi Mafongo
, Oscar Kambona kuwataja wachache yote
yalikuwa yamefutwa kabisa.

Siku ile Mwalimu Nyerere ambayo aliwahutubia Wazee wa Mzizima
yaani Dar es Salaam kuwaaga ambayo kwa bahati mbaya sana ndiyo
siku aliyosema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika
TAA yeye alipoingia TAA.

Mama Maria Nyerere alikuwa na kikao kifupi
na akina Mama wa Dar es Salaam hapo hapo Diamond Jubilee Hall.

Mmojawapo katika hao akina mama alikuwa Mama Daisy.

Mama Maria aliwaeleza akina mama wale kuwa yeye na mumewe
walipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes.

Wanamajlis,
Mtakumbuka siku niliposema kuwa Mwalimu Nyerere alisema kuwa
hakumbuki cheo cha Abdul Sykes katika TAA palizuka ubishi mkubwa
sana hadi Yericko Nyerere kusema yeye ataiweka hapa hotuba hiyo
tusikize kama kweli Mwalimu Nyerere alitamka kweli maneno yale.

Mama Daisy hakuwa na wasiwasi na mimi akinieleza kila kitu na kubwa
ambalo lilinishtua sana ni siku aliponiambia kuwa Allah ndiye atoae
ufalme, ''Baba yako yeye akimtaka sana Chief David Kidaha Makwaia
ndiyo aingie TAA wamchague president kisha waunde TANU.

IMG-20160406-WA0111%2B%25281%2529.jpg

Chief Daivid Kidaha Makwaia

Lakini Chief hakutaka.

Kila Chief akija Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya Legico tukimualika
nyumbani kwa chakula cha jioni na mimi nilikwa pale nikiwaandalia na
nikisikia mazungumzo yao yote.

Bwana Abdul akimwambia Chief Kidaha, ''David hebu achana na hao
Waingereza bwana njoo huku tudai nchi yetu.''

Mama Daisy alikuwa na mengi na akizungumza alikuwa hana uchungu
kwa yale yaliyopita akizungumza huku ametulia kabisa.

Hali ya siasa katika TAA ilikuwa hivi katika miaka ya mwanzoni ya 1950.
Yako mengi lakini kwa leo haya yanatosha.

Anaetaka zaidi kuhusu Chief Kidaha Makwaia aingie hapa:
Mohamed Said: Chief David Kidaha Makwaia 1922 - 2007
 
Mzee Mohamed Said naomba kujua huyu "Mr Misifa" Dully Syakes mtoto wa K'koo ni mtoto wa nani kati ya hao wazee wapigania uhuru?
 
Ngaliba...
Dully Sykes
ni mtoto wa Ebby Sykes.
Ebby ni mtoto wa Abdulwahid Sykes.

Dully ni mjukuu wa Abdulwahid Sykes.

Unaweza kusoma habari za Ebby, baba yake Dully hapo chini:
Mohamed Said: TAAZIA YA EBBY "EBRAHIM" SYKES 24 FEBRUARY 1952 - 15 FEBRUARY 2015
Sheikh, ni Taazia au Tanzia? Neno hili Taazia sijawahi kulisikia likitumika katika muktadha huu. Sijui Kiarabu na ningependa kujua zaidi matumizi yake pamoja na tofauti yake na neno Tanzia. Shukrani!
 
Sheikh, ni Taazia au Tanzia? Neno hili Taazia sijawahi kulisikia likitumika katika muktadha huu. Sijui Kiarabu na ningependa kujua zaidi matumizi yake pamoja na tofauti yake na neno Tanzia. Shukrani!
Dah, makasa tu ya kiuandishi huwa inatokea, mengine wasomaji tunatakiwa kusahihisha tu na kupita kimya, haiwezekani kuwa hajui linavyoandikwa neno TANZIA.
 
Okelo pia Uhuru wa Zanzibar kasahaulika pia...😀😀
 
Dah, makasa tu ya kiuandishi huwa inatokea, mengine wasomaji tunatakiwa kusahihisha tu na kupita kimya, haiwezekani kuwa hajui linavyoandikwa neno TANZIA.
Hapana! Naamini siyo makosa ya kiuandishi kwa sababu mbali na heading, hata katika habari yenyewe karudia neno hili hili Taazia. Ungekuwa umesoma makala yote ungeona. Na nijuavyo mwandishi ni mwanazuoni na siamini kama anaweza kurudia kosa lile lile zaidi ya mara mbili.
 
Sheikh, ni Taazia au Tanzia? Neno hili Taazia sijawahi kulisikia likitumika katika muktadha huu. Sijui Kiarabu na ningependa kujua zaidi matumizi yake pamoja na tofauti yake na neno Tanzia. Shukrani!
Shimba...
Wewe ni mtu wa pili kuniuliza kuhusu neno, ''taazia.''

Mtu wa kwanza ni rafiki yangu Suleiman Seif kutoka Tanga na msemaji wa
Kiswahili kwa asili yake.

Mimi nilikuwa nikiandika, ''tanzia,'' hadi siku aliponisahihisha Abdilatif Abdalla.
Huyu ni bingwa wa Kiswahili.

Toka siku hiyo nimekuwa nikiandika, ''taazia.''

a2ft12AIm6n1dtrcoCXeZy570Z0mR-6SMy1ipLB7NlWsFHhjfXJu5zOhgXUgDclEFb6P7KQBd5zJwlogC2eAbxZWQzvo6SiLCzXEHzZObrIpkXIEhgrgqQtRlyO0lBZmp6fNSSsuSKYqUKPoQOpG1NLbjS6kO7CrMVJ4l2vmsntuzSf3P5l_gTDOqOriqZAuZQUOBFRKyUQCVFLZIY0bW2PrIDKoWrWWI0CBYv9m_eU3zd8iiiFaosAKNSFfKQQKmWLQ_HMe02CXNHDqP5r0d3zH7HQUbRwV4TaBobC5DkgWFvJmxyQVxjTLd3GIl9KZ7zGXvA-4CA22rUDPnvqJkplUA-OjNoxQ8y9YiyzPxEwRyTT0RV-sEVUa10cNuenmXh1xtcWGdhQoET8033geEeQ47a_G2t7C9WS06N7Pon_voMC3DbZ7Lhxs-vDEmezoLq7WfNPewXzZsU4-k57nugjhTZ9KpTPfWIgw49dVwD_iRQ0HyuBuVZN72Yr4mTG16i94OFqSC8lRuaK5mDSGE_6cQEkaQ5TKwSw4Y65WkJ8RYyfN5P_RJI4IJBJWr2325kIH8kdIpSMjhj-dMgJcKjqqr4MvTTPAFPRK-0f-ESGApIMTBg=w480-h360-no

Mwandishi akiwa na Abdilatif Abdalla Humburg, Ujerumani

Unaweza kumsoma Abdilatif hapo chini:
Mohamed Said: KENYA: TWENDAPI?: RE-READING ABDILATIF ABDALLA'S PAMPHLET FIFTY YEARS AFTER INDEPENDENCE Kai Kresse
Mohamed Said: MSIKILIZE ABDILATIF ABDALLA
Mohamed Said: KITABU KIPYA KUHUSU ABDILATIF ABDALLA: POET IN POLITICS
 
Dah, makasa tu ya kiuandishi huwa inatokea, mengine wasomaji tunatakiwa kusahihisha tu na kupita kimya, haiwezekani kuwa hajui linavyoandikwa neno TANZIA.
Taazia ni neno sahihi kabisa.
 
Sheikh, ni Taazia au Tanzia? Neno hili Taazia sijawahi kulisikia likitumika katika muktadha huu. Sijui Kiarabu na ningependa kujua zaidi matumizi yake pamoja na tofauti yake na neno Tanzia. Shukrani!
Taazia ni neno sahihi kabisa, maeneo ya pwani kama Mombasa hili hutumika sana.
 
Back
Top Bottom