Sasa toa maelezo basi ilikuwaje kama unafahamu vizuri...na ueleze ni vipi walimtumia Nyerere barua Makerere ya kutambulisha chama (TAA)
Fyatu,
Nyerere hakuandikiwa barua na yeyote katika TAA wala hakuwa akijulikana
kama mwanasiasa hadi alipofika Dar es Salaam na kujiunga na wanaharakati
waliokuwa viongozi katika TAA.
Soma kisa hiki hapo chini kitakupa picha ya siasa zilivyokuwa Dar es Salaam
ya mwaka wa 1950:
Huyo Bi. Mkubwa ni
Mama Daisy.
Huyu mimi ni mama yangu.
Kushoto:
Mama Daisy, mbele ni
Bi. Titi Mohamed
na kushoto yake ni
Bi. Zainab mkewe
Tewa Said Tewa
katika maandamano siku za mwanzo za uhuru
Jina lake ni
Mwamvua biti Masha.
Lakini kwa watu wa Dar es Salaam akivuma kwa jina la binti yake
Daisy kwa hiyo akijulikana kama
Mama Daisy.
Ingekuwa si huu uhusiano wa kindugu
Mama Daisy asingenieleza
chochote katika historia ya mumewe marehemu
Abdulwahid Sykes.
Wakati ule watu walikuwa wakiogopa sana kusema lolote lililo kinyume
na historia ambayo watu walikuwa wameaminishwa.
Jina la
Abdul Sykes na mdogo wake
Ally na wazalendo wengine kama
Sheikh Hassan bin Amir,
Sheikh Suleiman Takadir, Bi, Tatu bint
Mzee, Iddi Faizi Mafongo,
Oscar Kambona kuwataja wachache yote
yalikuwa yamefutwa kabisa.
Siku ile
Mwalimu Nyerere ambayo aliwahutubia Wazee wa Mzizima
yaani Dar es Salaam kuwaaga ambayo kwa bahati mbaya sana ndiyo
siku aliyosema hakumbuki
Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika
TAA yeye alipoingia TAA.
Mama Maria Nyerere alikuwa na kikao kifupi
na akina Mama wa Dar es Salaam hapo hapo Diamond Jubilee Hall.
Mmojawapo katika hao akina mama alikuwa
Mama Daisy.
Mama Maria aliwaeleza akina mama wale kuwa yeye na mumewe
walipokelewa Dar es Salaam na
Abdul Sykes.
Wanamajlis,
Mtakumbuka siku niliposema kuwa
Mwalimu Nyerere alisema kuwa
hakumbuki cheo cha
Abdul Sykes katika TAA palizuka ubishi mkubwa
sana hadi
Yericko Nyerere kusema yeye ataiweka hapa hotuba hiyo
tusikize kama kweli
Mwalimu Nyerere alitamka kweli maneno yale.
Mama Daisy hakuwa na wasiwasi na mimi akinieleza kila kitu na kubwa
ambalo lilinishtua sana ni siku aliponiambia kuwa Allah ndiye atoae
ufalme, ''Baba yako yeye akimtaka sana
Chief David Kidaha Makwaia
ndiyo aingie TAA wamchague president kisha waunde TANU.
Chief Daivid Kidaha Makwaia
Lakini
Chief hakutaka.
Kila
Chief akija Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya Legico tukimualika
nyumbani kwa chakula cha jioni na mimi nilikwa pale nikiwaandalia na
nikisikia mazungumzo yao yote.
Bwana Abdul akimwambia
Chief Kidaha, ''
David hebu achana na hao
Waingereza bwana njoo huku tudai nchi yetu.''
Mama Daisy alikuwa na mengi na akizungumza alikuwa hana uchungu
kwa yale yaliyopita akizungumza huku ametulia kabisa.
Hali ya siasa katika TAA ilikuwa hivi katika miaka ya mwanzoni ya 1950.
Yako mengi lakini kwa leo haya yanatosha.
Anaetaka zaidi kuhusu
Chief Kidaha Makwaia aingie hapa:
Mohamed Said: Chief David Kidaha Makwaia 1922 - 2007