Dully Sykes

Eyce,
Unaniuliza lipi jambo la kawaida na lipi si la kawaida.

Babu yake Ebby, Kleist Sykes, (1894 - 1949) aliacha mswada wa kitabu alichoeleza maisha yake na ya wazee wake kuanzia kijijini Kwa Likunyi, Imhambane, Mozambique alikotoka baba yake hadi yeye alipokuwa mtu mzima akiishi Dar es Salaam.

Mswada huu leo ni sura ndani ya kitabu, "Modern Tanzanians," (1973), kitabu kilichohaririwa na John Iliffe.

Hili si la kawaida.

Kuhusu mtazamo hilo nakuachia wewe.

Kuhusu "lifestyle," ya Ebby naweza kusema kaishi kama tulivyoishi watoto wote wa Kariakoo.

Hakuna la kunishangaza mimi.
Umetaja muziki.

Ebby akijua sana kupiga guitar na walikuwapo vijana wengi katika 1960s Dar es Salaam tuliovutiwa na pop music ya Uingereza na Soul Music ya Motown.

Sijapata kuyafikiri kuwa ni mambo makubwa.

Kwangu haya ni ya kawaida.
 
Log...
Nilikuwa sijui "click bait."
Ahsante umenifunza kitu kipya.

Sijui ni kipi kimekuudhi.

Wengi waliosoma makala hayo wameipenda.

Lakini bahati mbaya wewe umeiona ina kasoro katika kichwa chake.

Makala yote ulochoona ni hilo.
 
Likud,
Nimezaliwa 1952.
Marahaba.
Naam wewe ni mwanangu na nyote hapa wengi ni wanangu.

Watoto wenu ndiyo mimi wa kuniita babu.

Ukiwa una mtoto wa kike jua huyo ni mchumba wangu.
🤣🤣🤣🤣
 
Abby Sykes dakika za mwisho nilikua naonana nae sana kino block 41 ,akiwa na gitaa au siku anaimba tu karaoke.
Kusema ukweli ukimuona unaweza sema ni mvuta ganja,unga aliyebobea.
Ukikaa nae mkaongea mkasikilizana.
Ni mtu mcheshi saana na hata ugomvi hana.
Na ukiwa jirani nae mbavu zako za kwake.
 
Log...
Nilikuwa sijui "click bait."
Ahsante umenifunza kitu kipya.

Sijui ni kipi kimekuudhi.

Wengi waliosoma makala hayo wameipenda.

Lakini bahati mbaya wewe umeiona ina kasoro katika kichwa chake.

Makala yote ulochoona ni hilo.
Wala sijakasirika Mzee wangu Story yako ni nzuri tu ila naonglea Jibu ulilompa Mdau alivyokuuliza kuhusu Dully (Main Heading ya Habari yako) na wewe ukasema haumfahamu hii ikanikumbusha hii kansa iliyotapakaa kwenye maandiko ya siku hizi.., nikakumbuka enzi za Heading tu kuweka kukupa abstract ya habari nzima... (The good old days)
 
Log...
Ahsante.
 
Dah, na kiwanja kilikuwa kishatolewa kwa ajili ya ujenzi, nasikia mtukufu Aga Khan alitoa msaada wake
Lakini Kuna hotuba ya Nyerere akihutubia kama mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa chuo hili.Niliwahi isikilize TBC taifa Katika Wosia wa baba.
 
Lakini Kuna hotuba ya Nyerere akihutubia kama mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa chuo hili.Niliwahi isikilize TBC taifa Katika Wosia wa baba.
Bali...
Sidhani kama hotuba hiyo ipo kwani iliharibiwa pale pale uwanjani siku ya kuweka jiwe la msingi.

Kisa kirefu kinahitaji muda kukieleza.

Wewe unazumgumza uzinduzi wa chuo.
Hapakuwa na chuo cha kuzinduliwa.
 
Bali...
Sidhani kama hotuba hiyo ipo kwani iliharibiwa pale pale uwanjani siku ya kuweka jiwe la msingi.

Kisa kirefu kinahitaji muda kukieleza.

Wewe unazumgumza uzinduzi wa chuo.
Hapakuwa na chuo cha kuzinduliwa.
Mimi pia nilishangaa uzinduzi wakati sikuwa kukiona na wala kusikia kilipo.Hii hotuba Kuna siku waliirusha.Kuna hotuba nyingine pia Nyerere anasema visiwa hivi viwili vitatusumbua sana kama ningeweza ningevisukumia mbali baharini.Nayo niliisikia mara Moja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…