Jitindejangongwa
Member
- Jan 17, 2013
- 28
- 3
jamani wataalam naomba nisaidieni haya maneno maana ninaamini nilichofundishwa darasani kuwa dunia ni duara. lakini sasa kuna hili neno utasikia kwa mfano "kila kona ya dunia" sasa nimekuwa nikijiuliza huu msemo wa kila kona ya dunia wakati duara halina kona umetoka wapi na hadi ukajijengea umaarufu.nisaidieni waungwana.
Asante kwa ufafanuzi huu.Kama ulisoma hapa TZ si kweli kusema ulijifunza DUNIA NI DUARA peke yake bila KONA YA DUNIA,Vinginevyo uwe umesahau.
Ni kweli tumejifunza kua dunia ni duara [ki-jiografia],.Ila ktk somo la kiswahili tunajifunza FASIHI,huko ndio kuna misemo mbali mbali yenye kusisitiza au kuweka mkazo au kuelezea/kufunza kitu fulani ili kuielimisha jamii,Ndio hapo utakapokutana na maneno kama "kila kona ya dunia","kila pembe ya dunia":Uwe mwangalifu wapi linatumika hilo neno na kwa lengo gani.