Dunia duara

Dunia duara

Beeb

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2018
Posts
29,394
Reaction score
59,069
Dada hakubaatika kumaliza kidato cha nne lakini alibahatika kupata nafasi ya kuhenya jeshini akitegemea atapata wakau nafasi ya kuingia jeshini lakini kwa upande wake mambo hayakua alivyotarajia

Dada aliamua kurudi uraiani na kuendelea kusongesha gurudumu la maisha..kama bahati shirika fulani wakawa wanatafuta wafanyakazi wakulinda getini Dada akatuma maombi lakini pia ikawa holaa tofauti na alivotegemea .Dada akaamua kukata tamaa kabisa ya kuajiriwa na hakutaka kujishughulisha na kitu chochote cha kumuingizia kipato cha kueleweka..katika kipindi chote kuna mwanaume alikua anamfuatilia..Dada akaona bora amkubalie tu

Siku ya kwanza kukutana kimwili na mimba ikaingia..mwanaume hakua na kazi ya maana lakini alijitahidi kulea mimba ingawa kuna wakati alikua anakwama na ndicho kipindi ambacho nilikua namuonea huruma shemela maana alikua anaoga matusi na kashfa kutoka kwa Dada

Mtoto akazaliwa bado Shem hakua sawa kiuchumi kwa hasira Dada akamwambia Shem haitaji pesa yake yoyote atafight mwenyewe na kuanzia hapo ajihesabie hana mtoto..kilikua kipindi kigumu cha shemela ila nilimsihi ajikaze ndio majaribu ya Dunia

Mungu akashusha baraka zake Dada kapigiwa simu anahitajika kwenye usahili wa kazi..Dada akaenda wiki iliyofuata Dada akaanza kazi na kiukweli alikua analipwa pesa nzuri..haikupita muda Dada akahama home akaenda kuanzisha maisha yake mbali na home..miezi michache mbele tukasikia Shem Baba mtoto anataka kuja kutoa mahali

Mahali ikatokewa harusi ikafungwa wakaanza maisha ya ndoa wanalea mtoto wao..ndipo vitimbwi vikaanza rasmi sasa..Dada hamueshimu mume wake Mwenye pesa ndio yeye mwanaume anamuona takataka..Dada anaaga anaenda job shift za usiku kumbe anaenda kwa wanaume zake.. Dada hashikiki Dada hakamatiki..kumbi zote za starehe anazijua yeye ..hawajibiki kama Mke..Leo kanunua ndinga hili baada ya miezi kanunua nyingine..nywele za bei hazimpiti..shopping ndio kabisaaa

Ndugu wakaanza msisitiza anunue kiwanja ajenge lakini alikua anawaona kama wanamuingilia katika matumizi yake..vituko vilizidi ndani ya nyumba ilibidi Shem aombe kiitishwe kikao Dada akanywe tabia yake..kikao kikaitishwa Dada akatubu na kutoa tamko harudii tena..ndoa ikawa imara baada ya miezi kadhaa Dada akapata ujauzito akajifungua mtoto wa pili.

Umri wa watoto kwenda shule ukafika Dada akawaandikisha kwenye shule za bei kama walikua na makubaliano au hawakua nayo hayahusu..Dada kaanza tena kasumba kama ya mwanzo tena safari hii ilikua hatari maana alikua anafanya uchafu hadi Shem anajua..Shem alishindwa kuvumilia akampiga Dada akafunga safari hadi home Shem akaonekana yeye ndio mkosaji na kuambiwa Dada abaki home kwa muda
Kina kaka wakaona Shem hakutendewa haki ilibidi wamfukuze Dada arudi kwa mumewe.

Awamu ya jiwe ikaingia na mashirika mengi wafanyakazi wake walipewa barua na Dada akiwa mmoja wapo..Dada hakuamini hadi pale alipothibitishiwa na boss wake kua hatakiwi kazini..Dada presha ikapanda akapelekwa hospitali akapewa huduma akarudi home.

Dada akaanza kupungua mwili na lawama kibao eti familia haimjali ..Amesahau kipindi anafanya kazi alivyokua anafanyia wenzie ukipiga simu hapokei anahisi wataka muomba pesa.Dada akaanza kua Mama wa nyumbani Mwenye mawazo yasiyoisha..Shem amekua mnywaji tena yule wa masimango na maneno ya Kumkera Dada..Dada anajuta yote aliyoyafanya enzi yupo kazini ..anajuta kwanini hakusikiza ushauri wa wakubwa..anajuta kwanini alikua hamushimu mumewe.

Week iliyopita tumepigiwa simu Dada alitaka kujiua na tumshukuru Mungu Dada wa kazi alimuona akawahi kumpokonya vitendea kazi.

Dada anajuta sasa...hana mbele wala nyuma..miaka 10 aliyotumika kazini imekua bure ..Dada pressure haziishi.
 
Stress disorder itamtoa roho masikini ". Jitahidini mumtafutie wataalamu wa psychology wa mpatie ushauri nasaha dada yetu atakufa kihoro

NAMALIZIA NA POLE SANA KWAKE
 
Mwache afe ...si alijifanya kasahau kale kamsemo ka "hakuna marefu yasiokua na ncha"
 
Maskini dada alijua ofisi ni yake atakua hapo milele. Mkumbusheni kabla hajafa ajue ana watoto wanamtegemea
Alihisi ivyo labda..maana alipigiwa kelele kajiendeleze kielimu linaingilia kulia linatokea kushoto...jiwekee kitega uchumi hapo ndio kabisa anaweza gombana
 
Kupata mtihani kukosa mtihani. Ila mtihani Wa kukosa ndy mkubwa zaidy shidaa inakuja pale ukipata pesa.
 
Majuto ni mjukuu.
Na asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
Laiti angesikiza ushauri wa wakubwa zake kipindi hiko na angejifungulia hata kibanda cha mkaa yasingemkuta hayo.

Hata hivyo dada anahitaji watu wa karibu wawe naye wampe ushauri kama kesha fikia hatua ya kutaka kujiua anaweza arudie tena,pole yake.

Halafu hii tabia ya kupata pesa na kuanza kidharau wanaume,wanawake sisi tunaitoa wapi??
 
Dada hakubaatika kumaliza kidato cha nne lakini alibahatika kupata nafasi ya kuhenya jeshini akitegemea atapata wakau nafasi ya kuingia jeshini lakini kwa upande wake mambo hayakua alivyotarajia

Dada aliamua kurudi uraiani na kuendelea kusongesha gurudumu la maisha..kama bahati shirika fulani wakawa wanatafuta wafanyakazi wakulinda getini Dada akatuma maombi lakini pia ikawa holaa tofauti na alivotegemea .Dada akaamua kukata tamaa kabisa ya kuajiriwa na hakutaka kujishughulisha na kitu chochote cha kumuingizia kipato cha kueleweka..katika kipindi chote kuna mwanaume alikua anamfuatilia..Dada akaona bora amkubalie tu

Siku ya kwanza kukutana kimwili na mimba ikaingia..mwanaume hakua na kazi ya maana lakini alijitahidi kulea mimba ingawa kuna wakati alikua anakwama na ndicho kipindi ambacho nilikua namuonea huruma shemela maana alikua anaoga matusi na kashfa kutoka kwa Dada

Mtoto akazaliwa bado Shem hakua sawa kiuchumi kwa hasira Dada akamwambia Shem haitaji pesa yake yoyote atafight mwenyewe na kuanzia hapo ajihesabie hana mtoto..kilikua kipindi kigumu cha shemela ila nilimsihi ajikaze ndio majaribu ya Dunia

Mungu akashusha baraka zake Dada kapigiwa simu anahitajika kwenye usahili wa kazi..Dada akaenda wiki iliyofuata Dada akaanza kazi na kiukweli alikua analipwa pesa nzuri..haikupita muda Dada akahama home akaenda kuanzisha maisha yake mbali na home..miezi michache mbele tukasikia Shem Baba mtoto anataka kuja kutoa mahali

Mahali ikatokewa harusi ikafungwa wakaanza maisha ya ndoa wanalea mtoto wao..ndipo vitimbwi vikaanza rasmi sasa..Dada hamueshimu mume wake Mwenye pesa ndio yeye mwanaume anamuona takataka..Dada anaaga anaenda job shift za usiku kumbe anaenda kwa wanaume zake.. Dada hashikiki Dada hakamatiki..kumbi zote za starehe anazijua yeye ..hawajibiki kama Mke..Leo kanunua ndinga hili baada ya miezi kanunua nyingine..nywele za bei hazimpiti..shopping ndio kabisaaa

Ndugu wakaanza msisitiza anunue kiwanja ajenge lakini alikua anawaona kama wanamuingilia katika matumizi yake..vituko vilizidi ndani ya nyumba ilibidi Shem aombe kiitishwe kikao Dada akanywe tabia yake..kikao kikaitishwa Dada akatubu na kutoa tamko harudii tena..ndoa ikawa imara baada ya miezi kadhaa Dada akapata ujauzito akajifungua mtoto wa pili.

Umri wa watoto kwenda shule ukafika Dada akawaandikisha kwenye shule za bei kama walikua na makubaliano au hawakua nayo hayahusu..Dada kaanza tena kasumba kama ya mwanzo tena safari hii ilikua hatari maana alikua anafanya uchafu hadi Shem anajua..Shem alishindwa kuvumilia akampiga Dada akafunga safari hadi home Shem akaonekana yeye ndio mkosaji na kuambiwa Dada abaki home kwa muda
Kina kaka wakaona Shem hakutendewa haki ilibidi wamfukuze Dada arudi kwa mumewe.

Awamu ya jiwe ikaingia na mashirika mengi wafanyakazi wake walipewa barua na Dada akiwa mmoja wapo..Dada hakuamini hadi pale alipothibitishiwa na boss wake kua hatakiwi kazini..Dada presha ikapanda akapelekwa hospitali akapewa huduma akarudi home.

Dada akaanza kupungua mwili na lawama kibao eti familia haimjali ..Amesahau kipindi anafanya kazi alivyokua anafanyia wenzie ukipiga simu hapokei anahisi wataka muomba pesa.Dada akaanza kua Mama wa nyumbani Mwenye mawazo yasiyoisha..Shem amekua mnywaji tena yule wa masimango na maneno ya Kumkera Dada..Dada anajuta yote aliyoyafanya enzi yupo kazini ..anajuta kwanini hakusikiza ushauri wa wakubwa..anajuta kwanini alikua hamushimu mumewe.

Week iliyopita tumepigiwa simu Dada alitaka kujiua na tumshukuru Mungu Dada wa kazi alimuona akawahi kumpokonya vitendea kazi.

Dada anajuta sasa...hana mbele wala nyuma..miaka 10 aliyotumika kazini imekua bure ..Dada pressure haziishi.
Sijalielewa dhumuni la kuandika uzi huu..!?
 
Back
Top Bottom