Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 471
- 1,217
Dunia haiheshimu walioanza mbio kisha kuishia njiani bali inawaheshimu waliomaliza wakiwa na matope magotini.
Kujikwaa sio laana bali nembo ya mashujaa kwamba ulikuwa uwanjani, hukubaki benchi Kwa hiyo ukianguka leo, tabasamu kisha jua Umepewa sababu nyingine ya kukimbia kwa hasira zaidi, kwa hekima zaidi na kwa dhamira zaidi.
Mdhamiria haogopi vumbi. Anajua taji linangoja baada ya jasho, machozi na makovu.
Kila siku watu tuko kwenye mbio na katika hizo mbio tunakutana mengi sana ikiwemo kuanguka, kuzomewa, kudharauliwa mpaka kutukanwa sasa ukisema uishie njiani basi utabaki kunenewa hayo na sahau kabisa kuhusu heshima kwani aliyemaliza tu mbio ndiye atakayeheshimika.
Timu hata icheze vizuri vipi bila kupata ushindi hakuna atakayeisifia mwisho wa mchezo bali ile iliyoshinda ndio itapata heshima zote mpaka kutunukiwa.
Mbio kweli huchosha na kujikwaa ni kwingi lakini katika yote tusimame tena kisha tuanze mdogo mdogo kukimbia mpaka kieleweke mwisho wa safari.
Malenga wa Kiha