Dunia haisimami na haitasimama kamwe, adui asiyethibitishwa kwa Lissu hayupo, tusongeni mbele

Dunia haisimami na haitasimama kamwe, adui asiyethibitishwa kwa Lissu hayupo, tusongeni mbele

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Kuendelea kuwa na hasira juu ya wasiokuwepo ni ujinga na kupoteza muda!

Muda hausubiri bali tukitaka muda utusubiri ni kufanya tulimbikize mambo mengi yatupasayo kufanya sasa!

Dunia iko mbaali sana kuliko mahali sisi tulipo! Tuna matatizo ya kiuchumi na umasikini wa watu uliokithiri

Tunakaa kulumbana na wafu ili hali tunayokazi ya kuwatoa watu kwenye umasikini wao kwa mipango inayotutaka tufanye sasa?

JPM hayupo, hawezi pata adhabu tena ya duniani, lakini pia hakuna uthibitisho wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba alimtafuna mtu na kumtwanga risasi

Mahaba ni mabaya. Kipindi cha JPM kuna watu ilifika pahala wakiwa na mahaba kwa JPM kuliko hata maisha yao wenyewe' watu walifikia kusema, kama kifo kingelikuwa kinabadirisha mtu wa kufa, wako tayari wafe wao kuliko JPM sembuse kumtwanga mtu risasi kwa aina ya mahaba yale

Kuna uzi humu ya clip moja ilimhusisha mwananchi mmoja akilaani kwa yoyote anayempinga na kumkashifu Magufuli kwamba atamshughurikia yeye kama yeye!

Sasa haya mambo yasituchukulie muda, tuendeleeni kulijenga Taifa letu

Haitasaidia kuendelea kumsagia meno marehemu na kwanza ni ujinga tu
 
Lisu ameendelea kudai kwamba hayati Magufuli aliagiza msaliti hasitahili kuishi na baada ya muda mfupi Lisu akashambuliwa kwa risasi Dodoma, je kumbe Lisu alikuwa anajijua ni msaliti wa nchi?, maana Magufuli hakutaja jina la mtu alitaja msaliti.

Kwanini Clouds FM hawakumuuliza dereva wake amemficha wapi?

Kwanini Clouds hawakumuuliza sababu za Acacia kufutwa Tanzania na hawakushitaki MIGA?

Kwanini Clouds hawakumuuliza kama alipigwa na Magufuli na sasa hivi ni miaka miwili Magufuli hayupo kwa nini uchunguzi haufanyiki sasa hivi?

Nb: watoto wa Mbowe na Lisu wote ni raia wa Marekani.
 
Wanakwambia Mungu alishaamua ugomvi ila ukiangalia kinachoendelea ni wazi bado wanamanung'uniko hawajaridhishwa na uwamuzi wa Mungu kwenye huu ugomvi, bado watu wana chuki na hasira ile ile kana kwamba hakuna kilichotokea kwa huyo Magufuli.
 
Wanachi wengi wana uelewa duni na wale wenye uelewa mkubwa ndio wako bize kubishana kuhusu Magufuli, yani yakianza hayo mabishano kuna watu pamoja na upeo mkubwa waliyonao unakuta nae anaongea utumbo.
 
Lissu amesema ktk mahojiano na Clouds kuwa aliwaona vijana wawili walioshuka na kumshambukia bt AMEWASAHAU na hata akiwaona Leo hatowakumbuka.

Imekaaje hiyo kisheria.
 
Back
Top Bottom