Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Katika msitu , watu dhaifu huawa huko ili wasipitishe udhaifu. Kwa njia nyingi, jamii ya wanadamu ni msitu.
Kuna nguvu mbaya dhidi yako. Lakini kile ambacho hakikuui kinakufanya uwe na nguvu zaidi.
Ulipewa maisha haya kwa sababu una nguvu za kuishi. Kwa nini sasa uwe mnyonge?
Zingatia kuwa hakuna kitakachotolewa kwako kwenye sinia la fedha. Takribani kila kitu utakachopata kutoka katika maisha haya ya duniani; ni lazima ukipate kwa kukipigania.
Yesu alisema wenye jeuri waichukue kwa nguvu. Aliwapiga Wafanyabiashara ndani ya hekalu. Aliwakabili Mafarisayo na kuwaita ni wazao wa nyoka (shetani). Alimwambia na Herodo "Mbweha, nitawatoa pepo na kuwaponya wagonjwa".
Yesu alikuwa mnyenyekevu Ila hakuwa mnyonge mbele ya waharifu wa kiroho.
Unyenyekevu sio unyonge, usikubali mtu aharibu biashara yako kwa jina la unyenyekevu. Pigania haki zako, acha unyonge.
Udhaifu mkubwa ni kukata tamaa katika maisha. Mapambano yako yanakuza nguvu zako.
Wachina wana usemi wao usemao "Anguka mara saba, simama mara nane".
Hii dunia sio ya wanyonge, pambana utatoboa. Mpinge kila anayejaribu kukufanya mnyonge.
Ubarikiwe.