Dunia ilivyojaa unafiki wanaojifanya wanamsapoti Tundu Lissu na kumdhihaki anapowaita kwenye maandamano!

Dunia ilivyojaa unafiki wanaojifanya wanamsapoti Tundu Lissu na kumdhihaki anapowaita kwenye maandamano!

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
18,833
Reaction score
23,276
Pindi anapojitokeza lissu kutoa tamko flani utawaona watu wengi wanajitokeza kujifanya wapo pamoja nae, lakini Lissu anapowaita wamuunge mkono kwenye jambo mfano ni 23/9/2024.

Kila mmoja bila haya wala soni wanamkatalia kweupe kwa kutokuitika wito kuonyesha jinsi walivyo wanafiki hakuna hata kima mmoja aliyesogea pale kituo cha polisi halafu wakishika vifaa vyao vya kuandika wanamng'ong'a kwa kujifanya wapo pamoja nae .

Enyi vijana ni lini mtaacha unafiki wa kujifanya mpo na Lissu ilihali ni wanafiki na waoga.

Ushauri wangu kwakuwa Lissu ni msema ukweli bila kumuogopa mtu wala kumuonea aibu wachane tu wanafiki, ni heri ubaki na sisi wachache tunaokwambia ukweli kuliko kundi la watu wengi wanafiki na waoga ,kura hawakupigii wala kuipigia CHADEMA na maandamano ukiwaita hawatoki barabarani.

Soma Pia: Tundu Lissu kuiburuza Tigo mahakamani

Utawaona hapa jukwaani kukaza shingo na madole marefu yenye makucha machafu kila dakika kupandisha nyuzi,unafiki ulioje wa kujifanya wanampenda Lissu na CHADEMA.

Lissu dawa ya watu wanafiki kama hawa vijana ni kuwapangusa wengi wao ni mamluki!

Hawana faida kwenye uchaguzi wala maandamano.
 
Pindi anapojitokeza lissu kutoa tamko flani utawaona watu wengi wanajitokeza kujifanya wapo pamoja nae, lakini lissu anapowaita wamuunge mkono kwenye jambo mfano ni 23/9/2024...
kila mtu anataka kwenda peponi, lakini ukitaka kwenda peponi lazima ufe, je nani yuko tayali kufa ili aende peponi?
 
Pindi anapojitokeza Lissu kutoa tamko flani utawaona watu wengi wanajitokeza kujifanya wapo pamoja nae, lakini Lissu anapowaita wamuunge mkono kwenye jambo mfano ni 23/9/2024.
Sumu haijaribiwi kwa kuionja mkuu ,polisi walitapakaa JIJI zima, SMGs, washawasha, mabomu, wewe kuweza? Wewe huogopi?

Kuna mistake CDM wamefanya, mgomo hautangazwi public, mgomo inatakiwa uwe wa kustukiza kama wamaasai walivyofanya, walijiorganize kimya kimya.
 
kila mtu anataka kwenda peponi, lakini ukitaka kwenda peponi lazima ufe, je nani yuko tayali kufa ili aende peponi?
Kufa kwa ajili ya lissu wewe si unampenda sana kwanini andamane peke yake!
 
Sumu haijaribiwi kwa kuionja mkuu ,polisi walitapakaa JIJI zima ,SMGs ,washawasha,mabomu ,wewe kuweza? Wewe huogopi? Kuna mistake CDM wamefanya ,mgomo hautangazwi public ,mgomo inatakiwa uwe wa kustukiza kama wamaasai walivyofanya....walijiorganize kimya kimya.
Sio tatizo kutangazwa public ila wengi ni bendera na unafiki kwenye ukweli wanajificha kila mmoja ana udhuru waache kumdhihaki lissu!
 
Pindi anapojitokeza lissu kutoa tamko flani utawaona watu wengi wanajitokeza kujifanya wapo pamoja nae, lakini Lissu anapowaita wamuunge mkono kwenye jambo mfano ni 23/9/2024...
Maandamano ya kushindana na silaha za moto? Siuti unafiki...ila kama wasingejitokeza kwenye yale maandamano ya nyuma yaliyofana sana ndiyo ningesema unafiki.

Akili za ma CCM mnazijua wenyewe, yaani mnaleta jeshi zima dar halafu watu wasipojitokeza mnasema Chadema haikubaliki.

Kwenye mikutano ya mama yenu mnasomba wananchi mpaka watoto kila kona halafu mnajifariji mnakubalika
 
Maandamano ya kushindana na silaha za moto? Siuti unafiki...ila kama wasingejitokeza kwenye yale maandamano ya nyuma yaliyofana sana ndiyo ningesema unafiki. Akili za ma CCM mnazijua wenyewe, yaani mnaleta jeshi zima dar halafu watu wasipojitokeza mnasema Chadema haikubaliki. Kwenye mikutano ya mama yenu mnasomba wananchi mpaka watoto kila kona halafu mnajifariji mnakubalika
Maandamano gani yalifana usiyejitambua!
 
Mtu amekamatiwa mlangoni, nyumbani kwake, mtaandamanaje na wajomba wametapakaa mtaani wanawinda roho yako...

Kikubwa ujumbe umefika.
 
Vijana wangeambiwa na Ali kamwe kuna supu ungewaona jinsi watakavyojazana hata kama kuna polisi na mbabomu!
 
Back
Top Bottom