Dunia ina mambo

Dunia ina mambo

Maty

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2010
Posts
2,167
Reaction score
727
Leo asubuhi nimekutana na huyu mtoto akanikumbusha hichi kisa, kinaweza kutusaidia pia kujifunza kitu. Ni cha kweli wapendwa msianze kuchakachua

Kuna jirani yetu alizaa na mwanaume watoto wawili hawakufunga ndoa ila waliishi pamoja kwa muda na kuachana maisha yakaendelea. Kuna kipindi wakaanza kugombania watoto mama anawataka na baba anawataka.

Baada ya muda baba alikua akamchukua mtoto mkubwa alikua na 10yrs, alipofika huko kwao akaanza kuumwa, mama alipopata taarifa ikabidi aende kumuona mwanae, kwa hali aliyomkuta nayo akaomba kuondoka nae, ndugu wa mume na mume mwenyewe wakakataa ila mama akamchukua kwa nguvu.

Baadae ilikuja kugundulika mtoto ana sickle cell, hivi wandugu sicle cell mtu huwa anazaliwa nayo au inaweza kujitokeza hata mtoto akiwa na miaka kumi? hiki kinanichanganya kidogo.

Mtoto yule aliumwa kwa muda wa miezi nane akaisha kuliko maelezo, na kipindi chote mtoto anaumwa yule baba hakuwahi kanyaga wala kutuma pesa za matibabu ya mtoto, baada ya miezi tisa yule mtoto akafariki dunia. Cha kushangaza yule baba hakukanyaga msibani tukazika yule mtoto.

Yule mama kifo cha mwanae kilimuumiza sana, alikua na vidonda vya tumbo vikaanza kumsumbua sana, hali ikawa mbaya baada ya wiki mbili toka mtoto wake afe na yeye akafa tukamzika. Cha kushangaza tena huyo baba hakuja kwa mazishi ya yule mama, na mpaka nazungumza hivi yule baba hajawahi kanyaga hata yule mtoto mwingine hajawahi leta matunzo yake, leo asubuhi nilivyomuona amenikumbusha na kuamua kuleta hichi kisa.

Ninachojiuliza hivi mtu unaweza gombana na mzazi mwenzio mpaka ukafikia maamuzi haya. Hata kama ni maudhi mmeudhiana mtu unaweza kufikia hatua ya kususa watoto wako na kususia mpaka mazishi?

Dunia hii ina mambo jamani. Poleni kwa maelezo mengi.
 
Mungu awarehemu marehemu ila binadamu tumegawanyika katika sehemu kuu mbili,moja uzuri nyingine ubaya!!Hivyo hawa hawakupata ushahuri nawatu waliokuwa hawakuwa na busara za kutosha!
 
Leo asubuhi nimekutana na huyu mtoto akanikumbusha hichi kisa, kinaweza kutusaidia pia kujifunza kitu. Ni cha kweli wapendwa msianze kuchakachua

Kuna jirani yetu alizaa na mwanaume watoto wawili hawakufunga ndoa ila waliishi pamoja kwa muda na kuachana maisha yakaendelea. Kuna kipindi wakaanza kugombania watoto mama anawataka na baba anawataka.

Baada ya muda baba alikua akamchukua mtoto mkubwa alikua na 10yrs, alipofika huko kwao akaanza kuumwa, mama alipopata taarifa ikabidi aende kumuona mwanae, kwa hali aliyomkuta nayo akaomba kuondoka nae, ndugu wa mume na mume mwenyewe wakakataa ila mama akamchukua kwa nguvu.

Baadae ilikuja kugundulika mtoto ana sickle cell, hivi wandugu sicle cell mtu huwa anazaliwa nayo au inaweza kujitokeza hata mtoto akiwa na miaka kumi? hiki kinanichanganya kidogo.

Mtoto yule aliumwa kwa muda wa miezi nane akaisha kuliko maelezo, na kipindi chote mtoto anaumwa yule baba hakuwahi kanyaga wala kutuma pesa za matibabu ya mtoto, baada ya miezi tisa yule mtoto akafariki dunia. Cha kushangaza yule baba hakukanyaga msibani tukazika yule mtoto.

Yule mama kifo cha mwanae kilimuumiza sana, alikua na vidonda vya tumbo vikaanza kumsumbua sana, hali ikawa mbaya baada ya wiki mbili toka mtoto wake afe na yeye akafa tukamzika. Cha kushangaza tena huyo baba hakuja kwa mazishi ya yule mama, na mpaka nazungumza hivi yule baba hajawahi kanyaga hata yule mtoto mwingine hajawahi leta matunzo yake, leo asubuhi nilivyomuona amenikumbusha na kuamua kuleta hichi kisa.

Ninachojiuliza hivi mtu unaweza gombana na mzazi mwenzio mpaka ukafikia maamuzi haya. Hata kama ni maudhi mmeudhiana mtu unaweza kufikia hatua ya kususa watoto wako na kususia mpaka mazishi?

Dunia hii ina mambo jamani. Poleni kwa maelezo mengi.

1.so dad was a kid?
2.nani ame kukumbusha?baba au mtoto?
3.Kweli dunia ina mambo mama mkwe,pole sana kwa mkasa huo
 
Duniani kuna watu na viatu
huyo mwanaume ni gubu tu
na atalipwa hapahapa duniani, haiwezekani akwepe responsibilities
kwasababu ya malumbano na mam watoto wake, haya basi hata msiba wa mwanao!
hatoishi kwa amani huyo itakuja kumuhaunt tu.
very sad story
 
Hawa hawakupata ushauri mzuri, ila malipo ni hapa hapa duniani huyu mwanaume jambo alilolifanya akali-extend hadi kwa mtoto inauma sana, inauma sana aisee.....
 
Hatuna uhakika kama alikua anaambiwa kuhusu misiba hii lakini au?
 
kuolewa/kuoa kwenye familia nyingine ni hasara tupu, bora kuwashwa upupu!!

haya ndiyo yanayonifanya niendelee bado kuwa single!!!!!!!!

nimekasirika utafikiri huyo baba ananihusu!!! kunauwezekano mkubwa ana pepo la hasira/kiburi huyo baba, si hali ya kawaida hii!!!
 
Labda na huyo baba amefariki unajuaje?
R.I.P mama wa mtoto pamoja na mwanae.

Hapa jamaa ata laumiwa hadi kesho,ila story haija kamilika!
Like,huyo baba alikua ana taarifiwa kuhusu misiba?
au
Wanaishi karibu kiasi kwamba msiba ukitokea tu atafahamu?
au
Labda na yeye kesha kufa!

kuna maswali mengi kabla ya kumlaumu mzee wa watu
 
siamini kama mwanao anaweza kufa usijue, hata kama huyo mama hakumwambia lkn wapo ndugu na majirani wangeweza kumwambia.

Speaker kumbukeni msiba si kama harusi hauhitaji kadi ya mwaliko!!!
 
kuolewa/kuoa kwenye familia nyingine ni hasara tupu, bora kuwashwa upupu!!

haya ndiyo yanayonifanya niendelee bado kuwa single!!!!!!!!

nimekasirika utafikiri huyo baba ananihusu!!! kunauwezekano mkubwa ana pepo la hasira/kiburi huyo baba, si hali ya kawaida hii!!!

Susy dear umesema kweli ndio maana wazee wa zamani huoi/kuolewa bil akufahamu familia some how ilikuwa inasaidia. Haiwezekani kutelekeza familia kiasi hicho hata kumsiba. So sad. Imeniuma sana.
 
watu wanasema jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.uwezijua yule mama alimwambia nini yule baba watoto.cku hizi wanawake wanakauli mbaya uwenda alimwambia wale watoto sio wako?je kama ni wewe utafanyaje?lazima utasusia tuu.jamani kina mama kuweni makini na kaulizenu mimi nimeshaona sana haya yanatokea kisa mama kasema mtoto sio wako>>>>
 
Hatuna uhakika kama alikua anaambiwa kuhusu misiba hii lakini au?
Mkuu kuna vitu vingine hauhitaji akili ya ziada kufikiri yaani utaarifiwe mtoto anaumwa halafu mtoto anapofariki usijulishwe hapa sioni unachojaribu kutetea ni nini, kama nina ugomvi na mke wangu sitawahusisha watoto hata siku moja, mtoto kamkosea nini huyu baba mbona alipoambiwa mtoto anaumwa kwanini hakwenda kumuona hata hela ya matumizi hakutoa hauwezi kuniambia eti tusikie na upande wa pili wakati mama na mtoto ni marehemu tayari inauma sana inauma sana aisee......
 
Inasikitisha sana hadi nakosa cha kusema but Mungu yupo atamsimamia huyo mtoto alie baki na kama baba yake yupo hai atapigwa fimbo na mungu tu hatoweza kuikwepa fimbo ya mungu.... fanya mabaya malipo ni hapa hapa duniani!!
 
Back
Top Bottom