Dunia inaenda kasi sana, sasa hivi kila mtu anakamata mnyonge wake

Dunia inaenda kasi sana, sasa hivi kila mtu anakamata mnyonge wake

kidole cha simba

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2022
Posts
1,994
Reaction score
2,510
Habari za mchana bin-adam wenzangu,

Nimekaa jana baada ya kutoka kuganga njaa mjini niakawa nimejipumzisha nyumbani na kasimu kangu ka TECHNO nikisikiliza habari za dunia kupitia radio sauti ya UJERUMANI

Pamoja na kwamba akili yangu imechoka mpaka imechakaa na kubaki na akili yakukatia maparachichi, akini kuna kitu kilinishtua sana, yaani kwa sasa kila mwamba anakamata mnyonge wake na kumkaba loba ya mbao na kumpra alichonacho,du!!

Huku RWANDA anatuuhumiwa kuingia CONGO kwa mwavuli wa M23, na kupora madini{sina uhakika kama ni kweli}, RUSSIA nae kazama kwenye maghala ya kuhifadhia nafaka ya UKRAINE akapiga jiwe la FA2MA, maghala yakafunguka, akaiba NGANO ya wanyonge wake akauza kusikojulikana {sina uhakika nimesikia tu radioni}, mara mchina kaipiga mkwara TAIWAN, mara ooh!! kiduku kafanya yake kwakutest mitambo, mara COW-BOY{USA} kafanya luteka ya kijeshi na KOREA kusini,ili kumchimba mkwala kiduku.

Kilichinichekesha sana, ni kugundua kwamba kumbe sungura anaweza kumkaba tembo, kivipi tembo!!!!...kivipi?...Boko haram wanalipeleka kipute Jeshi bora na taifa linaloongoza kijeshi AFRIKA. Maana yangu ni nini?....manangu ni kwamba, kabla mama SAMIA hajaamua kumteua huyo YAKHE kuwa CDF afikirie kwa makini sana, kwani DUNIA sasa ivi ni ya kiababe sana....atafute mtu mwenye uso wa mbuzi na sio handsome boy!!!!
 
Mabara ni wabaguzi Kama wewe jinga wazanzibar kwamba wako lelemama kama ulivyodanganywa huko kanisani kwenu toka hapa
 
Back
Top Bottom