Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,468
- 32,167
Kama kuna jambo ambalo dunia inapaswa kujifunza ni kutoka kwenye utawala wa Trump. Jamaa anaanzisha timbwili kila kona.
Nataka nigusie timbwili lake na Canada. Jamaa ana mapendekezo ya mikataba kwa Canada ambayo serikali yoyote yenye kujielewa haiwezii kuyakubali. Yani ni sawa ukaue uchumi na uhuru wako kumlidhisha Bw. Trump. Baada ya waziri mkuu wa Canada kumgomea, Trump katia vikwazo na kutangaza kuwa Lake Ontario ni Lake America.
Sasa hapa ndipo nimeona shida. Baada ya kupitisha hilo, Apple, Google na Microsoft wamelibadilisha jina na kuwa Lake America kwenye ramani zao ambazo kwa kiasi kikubwa ndizo zinazotumiwa kwenye vifaa vingi vya navigation duniani.
Ingekuwa ni kampuni za kichina zimefuata serikali ilichosema, basi ungesikia vyombo vya habari vya West kuwa kampuni za Kichina ziko chini ya serikali, mara chini inatumia tech na kampuni zake kuwaonea wengine.
Hili limenifanya nione ni kwanini China hataki makampuni ya West yawe dominant kwake maana kumbe zinatumika kama silaha kwenye mapambano. Sitoshangaa siku wakiamua Hormuz iwe Trump.
Ulaya wamechelewa sana kuzinduka maana ni ukubwa wao lakini kwa kiasi kikubwa kampuni za US ndizo zimetawala.