Dunia inapaswa kumuelewa Mchina anapokuwa anapambana na Marekani na hata kumuunga mkono

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,468
Reaction score
32,167
Kama kuna jambo ambalo dunia inapaswa kujifunza ni kutoka kwenye utawala wa Trump. Jamaa anaanzisha timbwili kila kona.
Nataka nigusie timbwili lake na Canada. Jamaa ana mapendekezo ya mikataba kwa Canada ambayo serikali yoyote yenye kujielewa haiwezii kuyakubali. Yani ni sawa ukaue uchumi na uhuru wako kumlidhisha Bw. Trump. Baada ya waziri mkuu wa Canada kumgomea, Trump katia vikwazo na kutangaza kuwa Lake Ontario ni Lake America.
Sasa hapa ndipo nimeona shida. Baada ya kupitisha hilo, Apple, Google na Microsoft wamelibadilisha jina na kuwa Lake America kwenye ramani zao ambazo kwa kiasi kikubwa ndizo zinazotumiwa kwenye vifaa vingi vya navigation duniani.
Ingekuwa ni kampuni za kichina zimefuata serikali ilichosema, basi ungesikia vyombo vya habari vya West kuwa kampuni za Kichina ziko chini ya serikali, mara chini inatumia tech na kampuni zake kuwaonea wengine.
Hili limenifanya nione ni kwanini China hataki makampuni ya West yawe dominant kwake maana kumbe zinatumika kama silaha kwenye mapambano. Sitoshangaa siku wakiamua Hormuz iwe Trump.
Ulaya wamechelewa sana kuzinduka maana ni ukubwa wao lakini kwa kiasi kikubwa kampuni za US ndizo zimetawala.
 
mchina hua namuunga mkono 100% karibu mambo mengi sana , vitu ambavyo najiuliza sana ni viwili
1. Mchina alipigaje haya mahesabu yake ya kwamba tunatakiwa tuwe na kila kitu chetu kwa gharama na njia yeyote ile.
2. Aliwezaje kufanikisha mambo hayo bila ya kua katika mvutano mkubwa na west, (au kigezo kikuu ndo kilekile kujihami kwa nyuklia?)
 
Walikuwa West hawajashtuka kama ambavyo walilala wakaja kushtuka tayari Hiitler ana jeshi kubwa. Siku hizi USA wanasema wazi wazi kuwa hawawezi iruhusu India ikue ije kuwa kama China.
 
Kama sio presha za Mabeberu Ccm wangetumaliza wote.
Hizo zama zimeisha mkuu. USA wakimpa mgodi basi watasifiwa. EU hawana meno wangekuwa na meno wangeshamalizana na Museveni. Ndiyo maana naona kuna uwezekano mkubwa Lissu akapigwa kifungo maana nadhani museveni ni mentor wetu and he does not give a fuc... about EU. Kiza Besigye yuko huko ndani siku nyingi tu.
 
Walikuwa West hawajashtuka kama ambavyo walilala wakaja kushtuka tayari Hiitler ana jeshi kubwa. Siku hizi USA wanasema wazi wazi kuwa hawawezi iruhusu India ikue ije kuwa kama China.
kongole nyingi kwa mchina, ni mtu ambaye anatakiwa kusomwa kwa makini sana
 
kongole nyingi kwa mchina, ni mtu ambaye anatakiwa kusomwa kwa makini sana
Kafanye kazi kwa wachina, waarabu na wahindi ndiyo utawajua vizuri
Usidanganyike na tv, simu, magari na laptop za kichina ambazo zipo nyingi low quality na ni bei nafuu. Ukinunua Scania moja hapo una Howo mbiliπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Hapo ulipo unatumia computer na simu ya kichina lakini Operating System (OS) ya MarekaniπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Ndiyo utajiuliza kwanini mchina hakuwa wa kwanza kutengeneza AIπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Matatizo ya Trump yanaisha mwaka 2028.

Matatizo ya China ni endelevu.
 
Wote wajinga wametanguliza maslahi binafsi kuangamiza dunia,huyo mchina nae mnyonyaji tu wa aAfrika kupitia mikataba ya hovyo yeye kwake maslahi kwanza,Marekani anavunja amani dunia ingawa kuna wakati anaisaidia Afrika ktk miradi ya kijamii,utawala bora na haki binadamu,mchina yeye kafanya dampo la bidhaa za hovyo.
 
Mkuu tunazungumzia kujitegemea... OS si kwamba watu wameshindwa kutengeneza OS ni kwamba kila nchi ikiwa na OS yake developers watatengeneza app ya Os ipi waache ipi? Ukitengeneza OS bila kuwa ana programs za kurun kwenye hiyo OS inakuwa haina maana.
Huawei wameuengeneza OS yao na ecosystem yao kwa china inafanya vizuri. Ukitaka kujua kuwashawishi developers sio jambo rahisi, kwani Microsoft na kuwa giant kwenye ukanada huo bado windows phone ilifail vibaya
 
Matatizo ya Trump yanaisha mwaka 2028.

Matatizo ya China ni endelevu.
Si kuna fununu kuwa anataka kuendelea. What if akiiingia JD Vance wale wale Maga movement? Na huu utawala wake umeonyesha kuwa kumbe hata marekani kiti cha rais kinaweza kufanya mengi ya hovyo na hakuna kile mnaweza fanya.
 
Si kuna fununu kuwa anataka kuendelea. What if akiiingia JD Vance wale wale Maga movement? Na huu utawala wake umeonyesha kuwa kumbe hata marekani kiti cha rais kinaweza kufanya mengi ya hovyo na hakuna kile mnaweza fanya.
Hao MAGA wenyewe wameanza kumchoka Trump.

JD Vance hawezi kuwa kama Trump, yani hata akitaka kuaumbua atakuwa analeta siasa tu ambazi watu watamdhibiti.

Sio hizi habari za kubadiliaha Lake Ontario kuwa Lake America.

Trump ni kichaa cha level nyingine.
 
Je Pete Hegseth? Au huyo hawezi kuwa rais?
 
Kwa sasa nanunua brand za mchina tu.
 
Reactions: Lax
suala la kwenda kufanya kazi kwa wachina , wahindi, waarabu si suala nalolilenga maana hata hao weupe kuna muda walijigawia dunia yote hii kama wanagawana keki.

nachosema mimi ni kwamba mchina anajitahidi kujitosheleza --- mchina anaenda mbali zaidi anakamilisha jambo hiko iwe kwa kugundua, kwa ku-copy na hata kwa kuiba tech. Huawei wamempiga vikwazo kaja na OS yake , hapo tayari mzani unabadirika

Howo hizo kwa construction anayopiga china na ukubwa wa nchi yake angekua anategemea mashine na vifaa mbalimbali vya kigeni angepigwa hela ndefu, kuna siku uzi mmoja wa shabiki lialia wa china Xi Jinping kama sikosei kuhusu vijiko vya kichina kuongezeka kwa wingi hapa TZ na africa kwa ujumla, kuna mdau akatoa hoja kwamba ni kwa sababu kampuni zilizopata tenda ni za kichina --- mkuu nakuuliza wewe hii huwezi sema ni big win? kama wasingekua na mikangafu yao si wangelazimika kununua ya kizungu, japan etc?


Mchina huyu wa low quality kama unavyosema wewe, anapata wateja maana yake soko bado lipo, watu wanataka unafuu kwenye maisha, mchina kaja kutukomboa sana 3rd world country kuna watu bila yeye vifaa vingi vya teknolojia wasinge tumia


mimi namuunga mkono mchina katika angle hiyo, ukikataa kumuunga mkono mchina alafu ukaja sikitika nchi yetu vitu vingi hatuwezi kufanya , basi inahitajika kupata darasa kutoka kwa mchina
 
Mxhina alikuwa sana mbele ya mda, miaka kumi na tano nyuma nilikuwa sielewi logic yao ya kupiga stop makampuni kama google, facebook, nk sasa ndo najua...
huyu beberu USA nguvu zake nyingi zipo kwenye pesa yake,
 
Reactions: Lax
Je Pete Hegseth? Au huyo hawezi kuwa rais?
Nakwambia hivi, hao wote ni wanasiasa wanaoweza kuleta vurugu za kawaida tu ambazo zilishawahi kufanyika na zitaendelea kufanyika.

Hakuna kama Trump kati yao wote hao.

Trump ana kichaa chake peke yake.
 
Mchina apewe maua yake, leo duniani watu wanaweza kumiliki vifaa vya electronic kwa reasonable price na kwa ubora ni sawa na vile vya magharibi au Japan na South Korea
 
Reactions: Lax
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…