Hatibu Shemnyama
Member
- Sep 3, 2026
- 11
- 10
Habari za wakati huu, wana-JamiiForums.
Ninatumia kalamu yangu kutoa faraja kwa kila anayejaribu kuboresha maisha yake na familia yake.
Kutokana na sababu kadha wa kadha, kama vile kubadilika kwa mifumo ya kidunia na mivutano ya kijiopolitiki inayoendelea duniani, ni dhahiri kwamba uchumi wa dunia kwa sasa upo katika hali ya utaabani. Athari zake zinajidhihirisha moja kwa moja katika maisha ya kila mmoja wetu, hasa katika nchi zinazoendelea.
Kila mmoja wetu anapambana usiku na mchana kujinasua kwenye wimbi hili la ukata na changamoto za kimaisha.
Katika mapambano haya, ni rahisi sana kujikuta ukiamini wewe pekee ndiye unayepitia hali ngumu. Lakini ukweli ni kwamba wenzako wengi wanapitia changamoto hizo hizo au hata kubwa zaidi.
Usikate tamaa. Endelea kupiga hatua zako ndogo ndogo kila siku. Unaweza kuona unachelewa kufikia malengo yako, lakini utafika tu.
Ni jambo la kawaida kabisa kibinadamu kuhisi umeachwa nyuma pale unapoona wengine wakipiga hatua. Hata hivyo, usihukumu maisha yako kwa tabasamu unazoziona kwenye nyuso za watu. Usifikiri wamefanikiwa kila kitu. Hata wenzako wana milima na mabonde wanayopitia kama wewe.
Tofauti ni kwamba, pengine wao wameamua KUISHI na kufurahia pale walipo sasa, huku wakiendelea kupambana kufikia maisha ya ndoto zao.
Kwa hiyo, weka nia na endelea kusonga mbele. Usijilinganishe na mtu kwa namna inayokufanya ujiumize na kujidharau. Kila mtu ana safari yake, muda wake na mapambano yake.
Ninakutakia mapambano mema.