Dunia inarudi ilipotoka, itarudi kwa maumivu makali sana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
DUNIA INARUDI ILIPOTOKA, ITARUDI KWA MAUMIVU MAKALI SANA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kila kitu kitarudi katika sehemu yake. Kila mtu atarudishwa katika nafasi yake. Hakuna atakayevuka mipaka yake tena. Bahari itajidhibiti mawimbi yake, wala maji hayataenda sehemu ya nchi kavu, Usiku utabaki kuwa Usiku, na Mchana utabaki kuwa Mchana. Pepo hazizidi nguvu ya mvutano, wala nguvu ya mvutano haitazidi Ulimwengu.

Nyakati za Uhuru WA kujitawala Kwa kila kiumbe vitakomeshwa. Hisia haziizidi Akili, wala mwili haitazidi Roho. Bali kila kimoja kitakaa sehemu yake.

Chuki na Ubaya na himaya yote ya uovu itapatiwa hifadhi yake, wabaya watabaki kuwa wabaya katika milki Yao wenyewe. Na wenye upendo na Wema watabaki katika Milki Yao.

Dunia Ipo mbioni ili kukamilisha Mzunguko wake wote. Inarudi kule ilipoanzia. Ilipokuwa.

Ili mwisho ukutane na mwanzo. Na pale mwisho unapokutana na mwanzo ndipo maumivu Makali hufikia kilele chake, maumivu Makali, mabadiliko yasiyozuilika, upya katika uzamani unazaliwa.

Mwanaume mwenye mamlaka yote, mwenye nguvu zote, na amri zote atatikiswa tikiswa, lakini kamwe haitowezekana Mwanamke akamshinda na kumtawala Mwanaume, ingawaje majaribio ya kuvuka mipaka yatafanyika kila mara.
Ni kama vilindi vya maji kufurika katika bahari na kutaka kuingia nchi kavu. Hilo halitawezekana lakini majaribio na ghasia za hapa na pale zitakuwepo.

Kile kilichozidi kitaumizwa, Yule aliyezidisha mpaka ataumia zaidi. Kwa sababu nguvu za Asili zitataka kuyarudisha mambo yawe kama yalivyokuwa. Vitataka Mwisho uwe mwanzo na mwanzo ubaki kuwa mwisho Milele.

Kazi za asili zilizodharauliwa zitakuwa kimbilio la Ulimwengu. Na katika kurudisha kimbilio hilo wengi wataumia Mno.

Kwa sababu kwenye kuvuka mipaka kuna mateka, kuna watumwa na Ukoloni.
Lakini pale mambo yanaporejea kama mwanzo maumivu hayanabudi kuambatana.

Mwanaume ni mlinzi wa Mwanamke hiyo ilikuwa mwanzo lakini ilipo na inapoelekea Mwanamke atakuwa mlinzi wa Mwanamke. Kwa maumivu Makali Sana hiyo itaonekana ni safari ya kuzimu yenye kutisha na Maumivu na Mateso Kwa wote Wawili yaani Mwanamke na Mwanaume.
Kwa sababu Jambo hilo halipo kiasili.

Mwanaume ndiye anayetakiwa kuwa kiongozi na kumtunza na kumhudumia Mwanamke, lakini tulipo na tunapoelekea Mwanamke ndiye atatakiwa kuwa kiongozi na kumtunza na kumhudumia mwanaume. Hiyo imeanza polepole kwenye Familia.

Ikiwa Wanawake WA Zama hizi wanauwezo WA kutunza Watoto wao Baada ya kutelekezewa au kuleta tafrani Kwa Mumewe. Hii inamaanisha wanauwezo pia wa kumhudumia Waume zao. Ingawa hiyo itafanyika Kwa maumivu Makali, Mateso na manyanyaso Kwa wote Wawili, yaani Mwanamke na Mwanaume.
Turudi, turudi tulipotoka. Dunia na walimwengu watasema. Huko Mbele solo. Huko ni kuzimu. Dunia ya Wafu.

Wasijue kumbe walishafika ukingoni, mwishoni mwa dahari, pale mwisho unapokutana na mwanzo.

Kimya na Giza litatawala. Huo utakuwa ni Usiku, Giza la kuzimu, ukiwa wa Wafu wanaoisubiri alfajiri, mwanzo Mpya, Dunia Mpya.

Acha nipumzike sasa.

Ijumaa Kareem.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Yeremia 31:22
Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.
 
Heshima yako mkuu.
 
Kuna kitabu cha alvin toffler cha future shock kinaelezea haya kwa kiasi chake.
 
Hilo halitatokea bali Mambo yatazidi kuharibika na kuparaganyika zaidi ya leo
 
Back
Top Bottom