Dunia inasubiri marathon - ubabe baina ya Ethiopia na Kenya

Dunia inasubiri marathon - ubabe baina ya Ethiopia na Kenya

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Hapa hamna ubishi wala nini, kivumbi kitakua baina ya Wakenya na Waethiopia kwenye mbio za Olympic marathon kule Rio mnamo Agosti 21. Mashabiki wote duniani wanasubiri kwa hamu kuona mchuano baina ya hizo team mbili, japo kutakua na wakimbiaji kutokea nchi zingine, ila hao watakua wapambe tu. Lakini lazima tuwe makini na Mganda fulani kutokea kwa jamii ya Wakenya.

Marathon ya wanaume huwa kama hitimisho au fainali ya Olympics.

Mashujaa wa Kenya tunategemea:
Eliud Kipchoge
Stanley Biwott

Kutokea Ethiopia tunaye:
Tesfaye Abera

Eritrea nao hawachelewi, wanaye:
Ghirmay Ghebreslassie

Uganda kuna huyu jamaa mwenye majina ya Kikenya jamani, anaogopesha kiaina:
Stephen Kiprotich

Yote tisa, timu zote hizi za Mashariki mwa Afrika, hivyo ni fahari kwa ukanda huu.
 
Tupia basi hapa Jamiiforums their '' personal best times'' tuweze kuona kasi na pia ubora wao.

Je mchuano huo marathon KM 42.2 unaweza kuweka rekodi ya Olympics kuwa 2:00:00 au 1:58:57 ? the world record for the marathon is 2:02:57, set by Dennis Kimetto in Berlin 2014 and second fastest 2:03:38 by Patrick Makau in Berlin 2012.
 
Mwaka huu wa 2016 Eliud Kipchoge ndiye anashikilia taji ya kasi zaidi kwa kuwa na rekodi ya 02:03:05. Labda tusubiri tuone kwenye hii ya Olympic ataikwenda vipi, naona kama atavunja rekodi zote maana dogo yuko fomu sana.
 
Mbona akina Wamae, Githimba, Gichinga na Munyui hawapo kwenye majina ya Kenya?
 
Mbona akina Wamae, Githimba, Gichinga na Munyui hawapo kwenye majina ya Kenya?
Kenya ina watu zaidi ya milioni 40 hivyo hatuwezi kwenda wote kule. Wengine inabidi tuwe mashabiki na kuwakilisha kwa mambo mengine.
Ni jinsi tu hautapata kila Massawe, Mrema n.k. kwenye timu ya mpira ya Tanzania.
 
amesema (eluid) Rio iko na polution na pia iko na humidity kwahivyo inaweza affect forign athlete,,,, alisema yeye mwenyewe ashawai kuishi brasil kwa miezi sita lakini alikua akiishi sao pailo, lakini Rio iko poluted sana mpaka unaskia hewa ikiingia... but anyway good thing ni owamba local athletes ndo wako na advantage pekee, the rest suffere the same fate, lets pray hio siku ya 21st mawingu yatachulua humidity yote na ile mvua ilikua inanyesha jana imeenda na hio polution yote, alafu tuombe mungu all goes well atleast pia sisi tuvunje rekodi kwa hii olympic, BTW nani anajua steeplechase ya 3000m men iko lini? hapo its nothing else other than 1-2-3 and posibly 4 finish at the podium ..
 
Kenya ina watu zaidi ya milioni 40 hivyo hatuwezi kwenda wote kule. Wengine inabidi tuwe mashabiki na kuwakilisha kwa mambo mengine.
Ni jinsi tu hautapata kila Massawe, Mrema n.k. kwenye timu ya mpira ya Tanzania.

Awesome response.
 
Mbona akina Wamae, Githimba, Gichinga na Munyui hawapo kwenye majina ya Kenya?
hili swali la kijinga ni kama kuuliza kwa nini wamarekani weusi wanashiriki kwenye sprints na sio wamarekani weupe
 
Tanzania ya akina Kiyomo,Filbert Bayi,Gidemas Shahanga,Zakaria Barrie,Juma Ikangaa... Ilitutoa kimasomaso.Inabidi tuwe wapole kizazi cha mashujaa wa mbio ndefu,kati na fupi kimetoweka.
 
Kilomita 42 ni nyingi sana, anything can happen

Aisei... yaani 42km, kama gari vile... halafu jamaa anakimbia kwa kasi muda wote bila kupunguza, hivi hawa watu huwa wameumbwa vipi. Masaa mawili mtu anakimbia umbali wote huo na hapunguzi kasi, nafikiri labda wake zao kitandani huwa wanawakoma, maana duh...
 
Tanzania ya akina Kiyomo,Filbert Bayi,Gidemas Shahanga,Zakaria Barrie,Juma Ikangaa... Ilitutoa kimasomaso.Inabidi tuwe wapole kizazi cha mashujaa wa mbio ndefu,kati na fupi kimetoweka.

Ngongo Vipi na kwenye kurusha mishale au hata kuogelea, yaani chochote kile maana kutokea kule Rio bila medali hata moja inakua aibu jamani.
 
kilam

Sawa,Wakalenjin washangilie...... Je, wanapokuwa huko huwa wanabeba, kupeperusha bendera na kuimba wimbo wa Kikalenjin? Ama kipindi cha Rugby Sevens,unataka wajaluo,waluhya na wakisii waimbe wimbo gani? Yule Mkenya of Indian descent anayewakilisha Kenya kwenye kurusha mishale amebeba bendera ya Kihindi?Kumbuka ni wanasiasa ndio hujaribu kutugawa, wanamichezo ndio hutuunganisha.
 
Hahaha....funny but very correct.
 
Ngongo Vipi na kwenye kurusha mishale au hata kuogelea, yaani chochote kile maana kutokea kule Rio bila medali hata moja inakua aibu jamani.
Mkuu, kweli hapo inatakiwa tujipange wabongo. ,
Suala la michezo halipewi kipaumbele kuanzia kwenye Sera za utawala hadi kwenye jamii kwa ujumla
Taifa LA watu 50mn kupeleka wawakilishi 7 ni masihara..
Na pia hii michezo mingine inahitaji tujitahidi zaidi Africa mashariki kwa ujumla,
Maana Kenyans ambayo kwa sasa mnawakilisha vizuri, bado medali zinatokana na michezo mmoja tu, (riadha),
Japo mnajitahidi kupeleka wawakikishi wengi katika michezo tofauti..
Na nimeangalia michezo mingine mingi kama kikapu , football, voliboli, netiboli, handball, masumbwi n.k,
Bado timu za Africa kuna shida Fulani, sijui labda ni Kujiamini,
Unaona timu ya weusi inaonyesha skills kushinda timu za wazungu but ultimately huishia kushindwa.
waafrica tuna safari ndefu sana bado.
 
Kwa ujumla, sports development ipo kwenye hali mahututi barani afrika.Yaani miaka nenda miaka rudi kuna mataifa hayatoshinda medali ,hadi na ya mbao. Sisi nako tusiwe wenye kushabikia wanariadha wetu kwa sauti maanake naona wenzetu toka pande zote za dunia wanatukaribia hadi na kuwapa wakenya uraia kusudi waongeze medali. Suluhu ni kufanya juhudi kubwa za kuendeleza michezo miongoni mwetu(sio vijana tu!) .Natamani kuona wenzetu wakishindania medali za water polo au synchronized swimming.
 
mi sioni serikali ikiamua tu hivi kuonheza mabilioni kwa michezo ambayo haijawai onyesha ubabe kwa mashindano nje ya nchi, na hata ikionyesha itakua sirahisi serilali kuchukua hatua kuu, mi naona wwatu na kampuni binafsi waungane na serikali. unaona vile south korea iliamua kutoka dola 100 millioni ili kujengwa chuo kikuu cha technologia pale konza ili hapo ndo pawe kama mahala penye uwezo wa kufanya research ya nguvu...... tunafaa sasa kutumia mabilioni kujenga chuo kikubwa kimoja tu, hicho chuo kiwe na primary-seconday-university, kiwe na kila aina ya world class swimming pools, rugby fields,football, indor stadiums....... alafu waajiri makocha bora kutoka nchi tofauti, kazi ya hio shule itakua ni kutembea nchi nzima na kuchukua wale wanafunzi walio na talanta kwa mchezo wowote afau wote wanawekwa kwa shule moja, hio shule iruhisiwa kua na program tofauti, kwa mfano wanarauka kufanya mazoezi, au wanarauka kusoma alafu nusu ya siku wanafanya mazoezi na world clasd coaches, baada ya miaka kadhaa utaona tunaanza kubobea kwa swimming, achery, judo, gymnasticd, na wote watakua wanatoka kwa hiki chuo, hapo ndo tutagundua kumbe talanta tunayo ni vile tu ilikua hatujawekeza vizuri
 
Back
Top Bottom