Dunia inatembea juu chini inapokosekana imani/dini. Leo nathibitisha kuwa imani ni muhimu kwa usalama wa ulimwengu

Dunia inatembea juu chini inapokosekana imani/dini. Leo nathibitisha kuwa imani ni muhimu kwa usalama wa ulimwengu

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Nimeshawahi kuchapisha bandiko mbalimbali yenye mlengwa wa kuhoji/kupinga vikali uwepo wa Mungu mkuu hoja zangu zilikuwa based on theories nadharia, ufahamu na akili/rational thinking katika kutambua uwepo wa Mungu sikufanikiwa kutambua uwepo wake katika kuyaongoza maisha yetu, ila nimekuja kugundua kuwa kuna mambo hayahitaji uthibitishaji ili uutambue uwepo wake ila ni kukubali kupitia matukio na hali.

Hata sayansi ina mambo ambaya kawaida yanatumia imagination reasoning katika kuconclude/kusolve tatizo mfano mdogo compressional force na tensional force nani amewahi kuziona?

Dini ni mfumo mzuri wa kiusalama kwa wanadamu ili kupunguza zile uncertenity zitakazotokana na hisia na akili za kibinadamu,kawaida unapoitoa dini binadamu anabakia kama kopo tupu au sumaku kila wazo linakuja kichwani mwake ni ubinafsi na kutaka uhuru na madhara yake inakuwa ni kujitanua kwa namna au njia yeyote hapo damu na hata mbinu chafu zitatumika ili kuweza kuyafika malengo.

Dunia inayokuja inapanda mbegu chafu na si salama kwa kizazi kijacho,tunaweza kushuhudia mengi miaka 50 ijayo.

Wazazi kumbuka kuwalea watoto katika misingi ya imani.
 
Bila dini binadamu ni mnyama.. Bila dini binadamu hana tofauti na Ng'ombe au Mbwa.. Dini inampa binadamu ubinadamu wake.. Dini inampa mtu ustaarabu.. Bila dini tutauana, tutaibiana, tutajamiiana bila adabu, ushenzi wa kila aina ndio utakuwa maisha yetu.

Mungu yupo na shetani yupo.. Kazi ya shetani ni kuvuruga mpango wa Mungu.. Na ndio sababu mawakala wake wapo bze kukataa uwepo wa Mungu.. Kila Kona mitandaoni watu wapo bize kupinga mafundisho ya dini.. Dini ni nguzo katika maisha ya mwanadamu..
 
MUNGU MKUU,MTAKATIFU MUUMBA WA KILA KITU KINACHO ONEKANA NA KISICHO ONEKANA NATHIBITISHA KWAMBA YUPO%
PIA NATHIBITISHA BILA SHAKA KWAMBA YEYE HANA DINI YOYOTE NAWALA HAFUNGAMANI NA DINI YOYOTE DUNIA HII..HAITAKUA HIVYO NAWALA HAITAKUJA KUTOKEA MILELE NA MILELE.
MUNGU NI UPENDO DAIMA HUDUMU MILELE NA MILELE.
 
Back
Top Bottom