Dunia kuwachekea Magaidi wa Taliban kuvamia Ikulu itakuwa na madhara makubwa

Ile nchi ni failed state mkuu wanajeshi wengi walikuwa mamluki wa taliban ndio maana mkuu wa jeshi alifutwa kazi
 
Mbona magaidi wa Iran kina Ayatollah walipoiondosha serikali halali ya Shah hukuilaumu UN
 
Ungeilaumu pia Serikali ya magaidi ya Zanzibar ya Afro Shiraz walipoipindua Serikali halali ya Jamshud
 
Yes, Qutar, India, Saudi Arabia, Yemen, Kuwait, Iraq, Bangladesh, Morroco, Misri ,Sudan, Waislam wa Tanga-Nyikwa, hawa huwa wanawapinga sana wamarekani WALIPASWA WAO NDIO WAKAPAMBANE NA TWALIBAN, ama unaposema Ulimwengu ulitaka BABA MTAKATIFU AAMURU MAJESHI YA VATICAN yakaingilie huko AFGHAN?
 
Hao UN Ni takataka TU.

Wamesaidia Nini msumbiji ilipovamiwa na magaidi, au mpaka marekani aseme
 
Kinachotokea sio Cha kushangaza,
Serikali iliyokuepo ilkua ikipokea misaada lukuki.

Ila rushwa,ufisadi na ubadhirifu vilitawala.
keki ya taifa ilikua inaliwa na wachache sana.

Viongoz waliishi maisha ghali sana ilhali wananchi,wafanyakazi,wanajeshi na polisi wakiishi maisha magumu.

SIO kwamba
Mgambo wa Taleban Afghanistan kuingia ikulu na nchi haikua na jeshi.

Bali jeshi la serikali lipo,
ila wanajeshi wamegoma kupigana na taleban.

Wameamua kuungana na wananchi kuwaunga mkono Taleban.

Icho ndicho kinachotokea
 
Kabla ya kuanza kutupia lawama jiulize kwa nini jeshi la Afghanistan limewakabidhi Taliban nchi bwereree tu bila purukushani yoyote.
 
Watu wanadai taifa lao wewe unaita Magaidi. Haki ya nani.
 
Taliban wanatofauti gani na utawala wa ccm mbona wao wanatambulika
 
Mamluki wengi walikuepo jeshini walisaliti jeshi na kuanza kutumikia talban kisirisiri ndio maana mkuu wa jeshi alitimuliwa kazi
Kabla ya kuanza kutupia lawama jiulize kwa nini jeshi la Afghanistan limewakabidhi Taliban nchi bwereree tu bila purukushani yoyote.
 
Wananchi wa walioungana na talban ni kina nani hao?
Hawa waliojazana airport ya kabul na mpaka wa pakstani wakiitaka kukimbia nchi yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…