Dunia Nzima imeshindwa Kuwasaidia Wapalestina wa Kawaida Wasiendelee Kufa Pamoja na Magaidi ya Hamas?

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Sasa ni zaidi ya mwaka, operation ya kijeshi ya Israel kuwaangamiza magaidi ya Hamas inaendelea, huku tayari wapalestina zaidi ya 57,000 wakiwa wameuawa, na wengi wakitajwa kuwa ni wananchi wa kawaida.

Magaidi ya Hamas, ili kuhakikisha hawauawi kiurahisi, muda wote wamekuwa wakijificha katikati ya makundi ya raia, na hivyo kusababisha vifo vya raia wengi, na huenda baadhi yao ni watu ambao wangependa kuishi kwa amani na wayahudi.

Mazungumzo ya kukomesha vita mpaka sasa yameshindikana. Israel inasema ipo tayari kusimamisha vita kwa muda tu lakini siyo kukomesha vita. Kukomesha vita ni mpaka itakapowaangamiza Hamas wote. Hamas nao wanasema kuwa wapo tayari kuachilia mateka wote kwa mpigo kukiwa na hakikisho kuwa vita inakoma, na askari wote wa Israel wanaondoka Gaza. Hamas wanawashikilia mateka 50, na kati yao, walio hai ni 20 tu.

Baada ya mazungumzo kukwama, Israel imezidisha mashambulizi, ambapo leo pekee, wapalestina 116 wameuawa.

Jambo la kujiuliza, hivi kweli Dunia nzima imeshindwa kuwalinda raia wa kawaida wasiokubaliana na sera za Hamas? Kwa nini usingefanyika mpango wa kuwaondoa wapalestina wa kawaida kutoka Gaza, wakabakizwa tu Hamas ndio wapambane na Israel? Na ikiwa hivyo, raia wa kawaida, wangeweza kupelekwa mataifa mbalimbali, wakatafutiwa makazi salama, mpaka hapo Hamas watakapokuwa wameangamiza, ndipo wakarudishwa?

Mbona wakati wa vita, katika mataifa yote, hupatikana wakimbizi, na huhudumiwa na taasisi za umoja wa mataifa? Tanzania ilipokea maelfu ya wakimbizi toka Burundi, wengine mapaka leo hawajarudi kwao. Ukraine, wananchi wake wamekuwa wakimbizi kwenye mataifa mbalimbali ya Ulaya. Kwa nini wananchi wa Gaza, hawapewi nafasi ya ukimbizi kwa mataifa yanayowazunguka? Au wanakataa wenyewe kukimbia kwenda mataifa mengine ili kuokoa maisha yao? Au jamii ya kimataifa imegoma kuwapa hifadhi ili kuokoa maisha ya watu wa Gaza?

Kwa upande wa Hamas, hawajui ule msemo wa mwenye nguvu umpishe? Hawajasoma historia jinsi kingdoms mbalimbali zilivyokubali kupoteza hinaya zao zilipozidiwa kwenye vita na kingdoms nyingine?
Yakufaa nini kung'ang'ania kwa kitu ambacho unajua kabisa kamwe hutashinda, huku ukiwa na uhakika wa watu wako kuendelea kufa? Kwa nini Hamas wasiridhie matakwa ya Israel, kubwa ni Hamas kutokuitawala Gaza, badala yake ikapatikana mamlaka yenye misimamo laini, ndiyo ikaongoza Gaza?

ALJAZEERA
  • The Israeli military continues to pound the Strip, killing at least 116 Palestinians across the enclave since dawn, including dozens of aid seekers.
The spokesperson of the military wing of Hamas has said Israel rejected a ceasefire agreement that would release all captives held in Gaza, and pledged that the group is prepared for a lengthy war if there is no deal.
 
Hamas hujificha nyuma ya watoto na kina mamaa huku wakivaa buibui na kujichanganya na raia ... Ivo basi myahudi inabidi azidi kufanya usafi wa kinaa apo gaza.
 
Kwasababu wanaowatetea Palestine wengi hawana akili.

Wametanguliza DINI mbele badala ya UTU na UBINADAMU.
 
huo mgogoro ukiwaambia watu waweke vitabu vyao vya dini kando watafute suluhu hawataki --- kila mtu anakwambia ipo kwenye kitabu ---- sasa utafanya nini hapo, we pande mbili kila mtu anakwambia hili lipo kwenye kitabu lilishatabiriwa
 
Halafu wakiuliwa Hamas hawasemi wanaonyesha raia tu, sasa hao Hamas hawana wazazi wakawaonea huruma?
 
Dunia imejaa unafiki na wanafiki wengi wakiongozwa na Marekani.
 
Sasa hiv hamas kama hamas hawana commanding chain mkuu. Ni magenge tu yanajiendesha bila usimamiz wa uongoz. Humo humo kuna Islamic jihad nk nk. Na limeibuka hilo moja linalioungwa mkono na Israel nalo lina silaha. Kwa kifupi wapalestina wakiondoka imekulq kwao na wakibaki wanakalia moto.
 
Tungejiuliza upande wa pili nao!
Israel wameshindwa nini kuwaangamiza Magaidi wa Hamas?
Ni takribani miaka 2 sasa!
 
Kupigania dhidi ya ukoloni si kazi rahisi sana. Niwape heko wapalestina hapo Gaza kwa kutetea utambulisho wao dhidi ya mkoloni. Ikiwa tayari inakaribia miaka miwili lazima tukubali kwamba Hamas ni freedom Seekers wenye mioyo ya kiume kweli. Kupigania na Israel ni kupigania na familia ya dunia ya kimagharibi itawalayo dunia. Hapo Israel silaha nyingi hupewa tu na Wamagharibi yaani wamarekani, wafaransa , wajerumani na Waingereza.Wapalestina baada ya kugundua waarabu wote wamewatenga baada ya kukatwa ndimi na mikono sasa wameamua liwalo na liwe watapambana na Israel hata kama kutakuwa na kitisho cha watu wao kwisha kabisa. Cha kukumbuka tu ni kwamba waisrael hapo hawatafanikiwa kuishi kwa amani miaka nenda Rudi.
 
Hao unaowahirumia wenyewe hawajihurumii..

Wapalestina wanafurahia hicho kitendo Cha hamasinkujipeneyeza katikati Yao..

Wanaamini kwa njia hiyo, wanalipiza kisasi na IPO siku wanawafuta wayahudi. Watajukuta wameisha na Gaza imebaki nyeupe..

Waarabu Wana akili za kijinga sana.
 
Waafrika tu wanafiki sana,siipendi sana tabia hii,yaani tunajifanya tuna uchungu na walio mbali na sisi kuliko walio karibu na sisi
Kungekuws na dini moja tu mkuu, hii ngoma ni ngumu sana huko middle east.

Wengi wanakabia kwenye wanaoendana nao kiimani
 
Back
Top Bottom