Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Majuzijuzi niliwaambia kwamba kwa sasa hii dunia inatengeneza watu soft sana, na niliwazungumzia waandishi wa habari walivyokuwa soft, si kama wale wa zamani, yaani usoft wao umekuwa kwenye kila kitu, dunia inatengeneza waandishi machawa kuliko hata wale wenye taalumu halisi ya uandishi.
Sasa hilo limehamia hata kwa watumishi wa Mungu, so sad! Yaani naandika mpaka natetemeka. Ukichukua Biblia na kusoma ndani, unakutana na watumishi wa Mungu, akina Eliya, Elisha, Musa na wengine wengi ambao walikuwa wakizungumza mpaka taifa linatetemeka.
Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuongea kwa niaba ya Mungu, kwenye taifa kulipokuwa na tatizo, walikuwa wakisimama wima na kuongea bila kumuogopa yeyote yule.
Akina Daniel na wenzake mpaka wakaingizwa kwente tundu la simba na hata tanuri la moto kwa kuwa tu walizungumza kwa niaba ya Mungu kuhusu nchi na namna ya kuabudu.
Leo vizazi vyetu havizalishi watumishi wa Mungu walio na nguvu, wameshika vitabu vya dini lakini kiuhalisia hawana nguvu. Kuna mambo mengi ya hovyo yanaendelea, wanayaona lakini wamekaa kimya. Si Tanzania, ni dunia nzima.
Wale watumishi wa Mungu waliokuwa na nguvu, misimamo wapo wapi? Dunia inazalisha watumishi wa Mungu wa aina gani? Unasikia tu kwamba mfalme alichanwa na mtumishi wa Mungu mpaka akachukia na kumuadhibu kifo, wapo wapi? ama zile nguvu ziliishi kwenye vitabu vya dini na kutoweka?
Leo tuna watu soft sana. Yaani dunia inataka kuzalisha watu waoga, wenye mioyo isiyo na ushupavu, inazalisha watu ambao hawawezi kusimama na kusema jambo lolote lile kinyume na mfalme, rais ama mtawala fulani.
Unajua hii husababisha nini?
Tunapata mataifa mengi ya hovyo kwa sababu wale tunaowaamini ambao kila siku wanasimama kwenye nyumba za ibada wameshindwa kusimamia kile kitu walichoagizwa na Mungu.
Mataifa yanapotea, watumishi wamekaa kimyaaa, matendo ya kikatili, ukocho yanaendelea, watumishi wa Mungu wamekaa kimyaaaa, halafu unaweza kuona huyohuyo anapiga goti chini na kumwambia Mungu nipe moyo kama wa Musa, nipe nguvu kama ya Eliya, nipe hekima kama ya Suleimani ama niwe kama Ibrahim.
Mtumishi wa Mungu ni wa kawaida ila ana nguvu kubwa, sema walio wengi wakisimama kwenye nyumba za ibada, wanazungumzia nguvu kubwa za watumishi wa Mungu wengine lakini kiukweli, hata nao hawana nguvu.
Ili taifa lisonge ni lazima liwe na watumishi wa Mungu wenye nguvu, misimamo, sauti kubwa na ya kuogopesha. Sauti ambayo hata mfalme, rais ama kiongozi yeyote akisikia, anaiogopa.
Hata kwenye nyumba za ibada watumishi wa Mungu wameshindwa kuweka msimamo fulani kwa mshirika fulani kisa tu ana pesa. Tukimsema, akiondoka, nani atatoa sadaka nyingi kama yule?
Pesa, woga vimeharibu hata misimamo ya watumishi wetu, tusahau kutengeneza mataifa yenye nguvu kubwa ya Mungu.oa