Nafikiri watoto wote wana akili sawa za kuweza kumudu masomo. huyo mto awe wa Kenya, TZ, au Burundi.Ila tuseme mazingira wanayosomea wanafunzi yana influence kubwa na matokeo yaani kuelewa au kutoelewa masomo. Maksi za kushinda nadhani zina utatta kidogo Kwa mfano mimi siafiki na ushindi uliyo chini 50% katika somo.
hapo juu nimesema mazingira ndiyo factor kubwa katika mafanikio. Mimi nina mfano halisi wa binti Mtanzania ambaye shuleni kwake huko vijijini alikuwa alikuwa darasa la nne, hajui kusoma wala kuandika jina lake. Kaka yake naye alikuwa siyo mzuri darasani.
Huyu binti alihamia USA baada ya mama yake kuolewa huko. Huyu binti aliingia darasa la nne huko USA hajui hata kuandika jina lake. Mhula wa kwanza alikuwa kama zezeta darasani. Huko shuleni alipewa mwalimu special wa kumsaidia hasa Kingereza. Baada ya mwaka huyo binti alianza kujuwa kusoma, kuandika, na hesabu. Alipingia middle school alianza kufanya vizuri, na alihitimu darasa la 8 na A tupu. Sasa hivi huyu binti yupo shule ya sekondari ya vipaji (darasa la 9). Huyu binti kwa maneno yake anasema kule kijijini shule alikuwa "yupo yupo tu". Alikuwa hajui sababu gani yupo shule. Anasema yeye ameweza kufanya vizuri huko USA kwa sababu "nikikosea naelekezwa na TZ nikosea nachapwa". Anadai walimu walikuwa hawafundishi ila kuwa wakali muda wote. Alipofika USA alikutan walimu wanafundisha na hawachapi, na ukikosea hasa nidhamu taarifa zinaenda nyumbani.
Kwangu mimi huu ni ushahidi kamili kuwa walimu wanatakiwa kutafakari namna ya kufundisha na kuwasaidia watoto kuelewa. Na huenda ni sababu hizihizi huwafanya watoto wa English Medium TZ kufaulu vizuri kwa sababu walimu wamejikita kwenye kuwasaidia watoto kuelewa masomo kuliko kukimbilia fimbo kuwaelimisha watoto, hasa wale wadogo.