Duniani kuna mambo mengi hatuyaoni ila dalili hizi ni ushahidi kuwa yapo

Duniani kuna mambo mengi hatuyaoni ila dalili hizi ni ushahidi kuwa yapo

Ibun Sirin

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
50
Reaction score
106
Huwezi kuona kwa macho vidudu vingi tu kama vya malaria, typhoid, amoeba, nk mpaka vipimo! lakini dalili za malaria na typhoid zipo na unaweza kuzigundua tu na kisha ukajiridhisha kwa vipimo na kuanza tiba.

Mikosi na nuksi dalili zake ni:

-Kuchukiwa na watu wengi bila sababu
-Kupanga kazi na watu kisha watu wakakususia na kukutenga
-Kuanzisha shughuli zako kwa makini na ukaharibikiwa bila sababu inayoonekana wazi
-Ndoa kuharibika au uchumba bila sababu
-Kila jambo unalopanga na kufanya halikui wala kuwa na tija japo kuna bidii
-Kazini au kwenye biashara unaonekana hufai kabisa hata kama una juhudi

Chanzo cha mikosi na nuksi

-Kurogwa
-Kukumbwa na majini au viumbe wabaya
-Kuwa na jamaa wenye husuda mbaya kwako
-Kufanya madhambi kila mara kama zinaa, ushirikina, ulevi na mengine machafu
-Kutosaidia wenye shida kama masikini, mayatima na wajane kiasi kwamba wakikulilia shida unawakejeli,
-Kutenga ndugu zako wa damu kiasi kwamba unawaona si chochote na unawadhihaki
-Kutofurahia maendeleo na mafanikio ya watu wengine
-Kutokufanya ibada, kuwa mvivu kwenye maswala ya kheri
-Tabia ya kuokota vitu vilivyotupwa njiani kama pesa n.k

Ibun Sirin
Kazi yangu ni kukupa muongozo ili kujikwamua kutoka kwenye nyavu hizo, uwe huru kama watu wengine.
 
Huwezi kuona kwa macho vidudu vingi tu kama vya malaria, typhoid, amoeba, nk mpaka vipimo! lakini dalili za malaria na typhoid zipo na unaweza kuzigundua tu na kisha ukajiridhisha kwa vipimo na kuanza tiba.

Mikosi na nuksi dalili zake ni:

-Kuchukiwa na watu wengi bila sababu
-Kupanga kazi na watu kisha watu wakakususia na kukutenga
-Kuanzisha shughuli zako kwa makini na ukaharibikiwa bila sababu inayoonekana wazi
-Ndoa kuharibika au uchumba bila sababu
-Kila jambo unalopanga na kufanya halikui wala kuwa na tija japo kuna bidii
-Kazini au kwenye biashara unaonekana hufai kabisa hata kama una juhudi

Chanzo cha mikosi na nuksi

-Kurogwa
-Kukumbwa na majini au viumbe wabaya
-Kuwa na jamaa wenye husuda mbaya kwako
-Kufanya madhambi kila mara kama zinaa, ushirikina, ulevi na mengine machafu
-Kutosaidia wenye shida kama masikini, mayatima na wajane kiasi kwamba wakikulilia shida unawakejeli,
-Kutenga ndugu zako wa damu kiasi kwamba unawaona si chochote na unawadhihaki
-Kutofurahia maendeleo na mafanikio ya watu wengine
-Kutokufanya ibada, kuwa mvivu kwenye maswala ya kheri na ibada

Ibun Sirin
Kazi yangu ni kukupa muongozo ili kujikwamua kutoka kwenye nyavu hizo, uwe huru kama watu wengine.
Ahsante kwa bandiko lako japo sio sahihi au halina uhalisia kwa kwa 100%. Bango lako limejikita sana kwenye dini pamoja na kwamba hujataja ila tayari unaonesha akili yako imejaa sana mambo ya dini dini.

Mafanikio ya mtu huja kwa kufuata kanuni za mafanikio na Baraka za Mungu, kumtaja Mungu sina ungamano na imani yoyote hapa bali nakiri tu kuwa Mungu yupo na ndio anatuwezesha. Kanuni za mafanikio ni pamoja na
  • Nidhamu kwenye mambo unayofanya ikiwemo matumizi ya fedha na kukukazia kwenye malengo yako.
  • Kuwa na bidii katika kile ukifanyacho. Kwani ukiwa na bidii utakua mvumbuzi, mbunifu na mgunduzi hii inapelekea mtu kujikuta mambo yake yanaenda vizuri bila tabu.
  • Kusaidia wahitaji, waingereza husema.. "A hand that gives, always receive " hivyo kadri unavyosaidia wahitaji ndivyo unavyojifungulia milango ya kufanikiwa.

Dini uislam, ukristo, ubudha na nyingine nyingi ambazo watu wanaabudu ni njia tu zilizotumika kuwapa watu ustarabu na kuwaondolea zile akili kama za wanayama pori na kufanya matukio kama kuuana na kudhuriana kuwa kama jambo ambalo sio jema na halikubaliki ( na hii naikubali) nje ya kumfanya binadamu awe mstarabu na kujali wanadamu wengine dini hazina lolote la maana zaidi ya kupoteza muda.

Naomba niishie hapo, nahitimisha tu kuwa mafanikio ya mtu hayaletwi na dini. Dini zinasababisha watu wapoteze mali na kuwa hohe hahe na wale wajanja kujineemesha kama akina mwamposa na Gwajiboy.
 
Mawazo ya masikini ni giza tupu. Siku ukiweza kuwa na akiba ya 20m na kuendelea ndio utajua umasikini ni hatari, utakuwa tofauti sana na utaheshimu sana pesa zako kuliko binadamu yeyote. Kuwa uyaone, pesa ndio kila kitu
 
Well put
 
Waganga wa kienyeji wengi mpo hivyo

Just ku mention shida za watu then mnamhusisha Mungu!

This is rubish
 
Back
Top Bottom