Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,890
- 26,440
Serikali ya raisi Samia ilikuja na R nne ambazo mojawapo ni maridhiano na hadi sasa hakuna maridhiano yalotokea na badala yake ni kuona kuwa wapinzani wa serikali watekwa, kuuawa na kuteswa kama si kupotea kabisa.
CCM chama tawala ambacho viongozi na wanachama wake wamekuwa wakijinasibu kuwa wasisitiza amani na utulivu wamesahau kuwa amani na utulivu huja baada ya wananchi na wapiga kura kuridhika na kuiona serikali yao ikiwajibika kwa kuhakikisha kuwa maendeleo ni kwa kila mtanzania na si matabaka fulanifulani ya watu.
Wananchi wa jimbo la Bumbuli walichinja ng'ombe baada ya jina la January Makamba kukatwa na kushindwa kupita katika hatua ya mchujo wa wagombea walotia nia kugombea ubunge wa jimbo hilo lililoko katika wilaya ya Lushoto. Vilevile kijana Byabato nae baada ya kukatwa ameandikwa sana na watu pia kushangilia kukatwa kwa jina lake huko kwao Bukoba.
Jimboni Kongwa wananchi khasa vijana wadogo ambao ni sehemu kubwa ya kizazi kiitwacho Generation Z wameshangilia kifo cha aliekuwa mbunge wa jimbo lao Job Ndugai ambae alifariki jana na taarifa za kifo chake kuwa kitendawili.
Mkuu wa wilaya ya Kongwa amesema leo kuwa ataongea na vijana na wananchi hao kuhusu kuheshimu marehemu na kuwa na muda wa kutafakari vifo vya watu kama Job Ndugai.
Marehemu Spika wa zamani Job Ndugai hana rekodi nzuri kwa wananchi wa jimbo lake kuwa kushindwa kuleta maendeleo yoyote yanoonekana na hata alipokuwa akiomba kura wiki zilopita alisimama mahali penye vumbi tupu huku mwenyewe akiwa ameloa vumbi.
Isitoshe marehemu Ndugai pia hana rekodi nzuri ya mahusiano mema na wanasiasa khasa wa vyama vya upinzani kuanzia Godbless Lema, Sugu, na mbunge wa zamani Tundu Lissu ambae Ndugai mwenyewe alihakikisha anazuia malipo yoyote ya matibabu na marupurupu mengine kwenda kwa Lissu khasa pale alipokuwa akipata matibabu nje ya nchi baada ya kudundiliziwa risasi na maharamia wanosemekana ni watu wasojulikana.
Marehemu Job Ndugai amekaa bungeni kama spika na mbunge kwa miaka 10 bila kufanya lolote jimboni kwake jambo ambalo si zuri kwa mbunge. Angalau angehakikisha amejenga barabara nzuri, vituo vya kutosha vya afya na kuweka huduma zingine muhimu na mahitaji kwa wananchi wa jimbo lake kwa kuzingatia kuwa alikuwa na vyeo viwili yaani uspika na ubunge.
Tayari imeripotiwa kuwa katika eneo ilipo nyumba ya marehemu Ndugai kulikuwa na pilikapilika za ujenzi wa barabara nzuri zinoelekea hapo nyumbai kwake ili kuficha aibu kwamba kiongozi huyo wa zamani wa mmoja wa mihimii ya utawala wa nchi hii alikuwa amejificha katika jumba ambalo lipo mafichoni kusikofika kwa barabara nzuri.
Wananchi wa Kongwa kushangilia kifo cha Job Ndugai si jambo zuri lakini inakuwa ni jambo la lazima kwa watu wa aina yake ambao wameonekana kushiriki kwa asilimia 100 wakikandamiza uhuru wa kujieleza kwa wabunge wa upinzani wanapokuwa bungeni na hata kutumia nguvu kuwatoa Bungeni kupitia askari maalum wa Bunge.
Pia Job Ndugai amewahi kuamuru wabunge kama John Mnyika na Sugu watolewe kwa nguvu bungeni (ndani ya sakafu ya Bunge la Tanzania) kwa kuburutwa na kutolewa nje kabisa ( thrown out) huku wabunge wa chama tawala wakishangilia jambo hilo la udhalilishaji wa wabunge wenzao ingawa wote wamechaguliwa na wananchi kwa kura.
Hapa Duniani ni mapito na sote binadamu huzaliwa na kuna siku tutapumzishwa kila mmoja kwa wakti wake. Wapo ambao vifo vyao vitaliliwa na kusababosha majonzi si tu kwa familia bali kwa wananchi wengi.
Cha kujiuliza ni kwanini sasa? na tumefikaje hapa?
Bila shaka majibu tunayo na pengine baada ya hapo ndipo tutapopata muda mzuri wa kufanya maridhiano yanoelweka kwa jamii nzima ya watanzania.
RIP Job Ndugai.