DURBAN: Bakhresa(Azam) anashindana na wazungu sasa

Ekasi

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
482
Reaction score
302
Jana naingia super market(cape town) naona unga wa ngano azam.
Watu wa rangi zote wananunua.

Nakumbuka nikiwa mdogo azamu inapoanziswa chumba kimoja pale Kariakoo leo tuna mtu ambaye hana diploma/degree/master, Phd lakini analisha Africa nzima kaajiri wafanyakazi wachina, weupe na weusi.

Kuna watanzania wana Phd's wamebakia kuiba, wapo walio na mabillion hawajui wafanye nazo nini. Mbaya zaidi wakifukuzwa kazi wanakufa masikini watoto wao wanatia aibu.

Napenda kumpongeza sana huyu mzee ambaye anahitaji kila sifa, na kutuonesha elimu sio makaratasi ni pamoja na kuelimika. Mzee wetu ana elimu ya pesa, hekima, busara, anafanya kazi kwa bidiii, hapendi makele na siasa, anajua anatoka wapi na anaenda wapi. Katengeneza kazi zaidi ya 120 hapa Durban.

Successful people do not blame a society, politics and community stop making noise wake up take responsibilities and change the global like sheak Said Bakhessa

Mungu akupe maisha marefu najisifu mbele ya marafiki zangu hapa nilipo kama natoka Tanzania ..Sio wanasiasa na wezi na wasio penda kazi wamebakia makelele kila siku..Tutakufa masikini na Mungu atatui motoni.
 
yupo wapi mzee wetu mengi, au karidhika ana alichonacho
 
Asante mleta mada kwa kutuhabarisha. Nampongeza sana mzee wetu Bakhresa kwa mafanikio makubwa aliyofikia yeye binafsi na familia yake. Kubwa zaidi ni kuitangaza nchi yetu ndani na nje ya mipaka yetu. Kwa sasa Bakhresa ameshika soko la Africa ya Mashariki na Kati kwa bdhaa ya nafaka chakula.

Haya ndio maendeleo anayopigania rais wetu mpendwa magufuli tuyafikie ya viwanda. Tulime na ku process wenyewe na baadae tu export ili kupata faida na si vinginevyo kama mtu mmoja mmoja na kama taifa.

Cha ajabu wanajitokeza watu kazi yao kupinga kila kitu na kutuona watanzania wote wapumbavu kama wao. Tujiepushe na upumbavu.
 
Ahahhahahhahaha nilijua tu wajinga wengi.. Samahani elimu niliyonayo inanikataza kumtukana mtu nikifanya hili nitakuwa natukana elimu yangu na nikawa kama miongoni waliosoma kwa ajili ya cheti sio kuelimika.

Sipendi kelele nilikuwa hivyo zamani baada ya kudundua elimu ni nini sipendi kabisa malumbano . Wewe huoni aibu kusema Bakhesaa anachuza" ni miongoni wa matajiri watatu Tanzania. Amewaajili watu na phds zao wengine ni wachina. Weusi na wazungu.

Hutakuwa mchawi kwa kauli yako...Entrepreneur wa ajabu kutoka kushona viatu mpaka kuwa na viwanda Afrika karibu yote...Achaaaaaaaaaaaaaaaaa ujinga.....Utabaki hivyo hivyo na roho mbaya yako
 
Phd's zenu tafuteni kazi muibie watanzania au kauzenu miogo, maana akili za kujiajiri hamna.. Na ungeeni umbea ndio mlizosomea Phd's. Degree zenu. You are nothing but a bunch of losers and shits.. Waongo waongo tu, usanii mwingi....
 
Mbona povu sasa ...hujaona ujumbe umeona herufi kubwa na msemo wenu wa kipuuzi huu eti pambana na hali yako

You could have done it better by praising him without offending the unfortunate ones.
 
sure! but they deserved it
 
Mkuu elimu na mafanikio ni sawa na kulinganisha Mlima na Kichuguu.

Wasomi wengi huja kufa masikini sana angalia Ma profesa wetu wako kwa sasa wanafundisha kwa mikataba baada ya umri wa kufika na wao kustaafu.

Si kwamba ukiwa na elimu kubwa ndo utafanikiwa, unaweza kuwa na elimu ya Msingi tu na ukawa na mafanikio makubwa sana.
 
the world is filled with arrogance and hate...

mkuu tatizo elimu yetu mbovu.... nimeangalia sana elimu ya nchi zilizoendelea wanafundiswa (life orientation) tangu grade 0 mpka chuo kikuu na nilazima usome kwa kila mtu (mandatory) ndio maana wanajielewa MSOMI WA KWELI HAWEZI KUWA MWIZI au mwongo kwani elimu inakataza hili.nk
 
hakuana watu wanaopenda kujuita wasomi kama watanzania.......they have failed us bigtime, not even ashamed
 
Sema unajichanganya mkuu kwenye maelezo yako. Unasema bakhresa hajasoma which means mafanikio sio hizo PhD unazo tukania watu humu. Mafanikio ni juhudi ya mtu asome au asisome. Mfano kuna PhD ambaye ni surgeon, ili aendelee kuokoa roho za watu anatakiwa ku concetrate kwenye hiyo kazi 100% akijichanganya na biashara nyingine ufanisi utashuka. Kwa mazingira ya bongo huyu mtu utamfananishaje na bakhresa kama sio akili za kijinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…