Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Hata hili swala la wamasai kuzuiliwa kutembea na dhana zao za kiasili Lina maswali ndani yake
 
Hata hili swala la wamasai kuzuiliwa kutembea na dhana zao za kiasili Lina maswali ndani yake
Suala la Wamasai limeonyesha ufa si kwasababu ya ukubwa bali linavyokuzwa kwa chuki.

Wamasai si jamii ngeni Afrika Mashariki. Tamaduni zao zinawafanya waonekane jamii tofauti kwasababu bado wamezingatia mila na desturi wakizilinda kwa wivu mkubwa.

Inatosha kusema tamaduni za kigeni hazijaiathiri jamii ya Wamasai na kuwafanya wawe 'unique'

Fedha ya Tanganyika huru ya Tsh 100 ilikuwa na picha ya Mmasai akiwa na mkuki na Lubega kuenzi Utamaduni.

Kuvaa Lubega si ukosefu wa mavazi, kutembea na rungu au Sime si kwa ajili ya kushambulia Watu. Ni utamaduni

Moja ya Tamaduni za Kimasai ni kuheshimu Umri, Rika pamoja na matumizi ya Silaha au Miito ya kuashiria hatari.

Karne zimepita , Wamasai wanaishi katika miji wakivaa Lubega , Rungu na Sime zao , ni nadra sana kuwaona wanazitumia bila sababu ya maana. Matumizi ya Silaha yana miongozo katika Jamii ya Wamasai.

Tukio la Zanzibar si la bahati mbaya. Kwa muda mrefu Wazanzibar wamelalamika uwepo wa Wamasai Visiwani wakiwaona ni jamii isiyostaarabika na pengine 'inachafua' Visiwa hivyo kwa kile wanachosema ' Si utamaduni wao'

Video inayosambaa inaonyesha Wamasai walilengwa ''targeted'' kule Beach na kuchokozwa ndipo walipoamua kutumia silaha kujilinda , yaani Fimbo.

Hata kabla ya wamasai kushambulia lilikuwepo tangazo la kuwataka wasitembee na 'Silaha' .
Wale askari waliokwenda Beach walikwenda kuwanyang'anya fimbo na Rungu zao.

Baada ya tukio tunapata picha kamili ya nini Wazanzibar walikusudia.

Ipo video ikimuonyesha DC wa Zanzibar akijigamba kuwatafuta Wamasai na wameanza kuvaa T-shirt na Jeans.

Maana yake Rungu, Sime , Fimbo halikuwa tatizo bali mavazi ya Lubega yaliyowakera Wazanzibar.
DC anafurahia Wamasai kuanza kuvaa T-shirt na Jeans!

Maswali yanayojitokeza ni pamoja na lile linalouliza, kama Wamasai wanapeleka utamaduni usio wa Kizanzibar, upi ni Utamaduni wa Wazanzibar ?

Tunaona Watalii si kwamba wamevaa Lubega bali wana 'Bikini' wakizunguka visiwani humo.
Je huo ndio utamaduni wa Zanzibar? Tunaona Vijana wakivaa 'kata K', je huo ndio utamaduni wa Zanzibar?
Tunawaona mashoga, je huo ni utamaduni wa Zanzibar? Lipi kati ya hayo ni zuri zaidi ya Lubega ya Wamasai?

DC wa Zanzibar anatuaminisha kwamba ili mtu astaarabike ni lazima avae T-Shirt na Jeans, au Kanzu na Kofia.
Kwamba Utamaduni wa Wamasai ni uchafu na kero Visiwani Zanzibar.

Jambo hili limechukua sura ya Muungano kwasababu Viongozi waliopaswa kulikemea wameamua kukaa kimya.

Ni kama lile tatizo la ndizi kutoka nchi ya Jirani ya Tanganyika kutoingizwa nchini Zanzibar.
Matatizo yote yanayotokea ni kwasababu Zanzibar ndani ya Muungano wamepewa kauli hata viongozi kuwaogopa.

Rais SSH na Rais Mwinyi ambao ni Wazanzibar wanadhima ya kujitokeza na kukemea Ubaguzi na dharau dhidi ya Tamaduni na Mila za Wamasai zinazobaragazwa na kudhalilishwa.

Marais wana kazi ya kuleta Taifa pamoja, kukaa kimya ni kuangalia ufa ukipanuka.

Kama ufa si kweli, pitia mitandao ya Jamii na huko mitaani utakautana na hasira kali.
Hasira ya jambo dogo kama hili si ya bure, kuna nguvu ya duku duku na manung'uniko nyuma yake

Mwenyekiti wa Chadema aliptahadharisha kuhusu taswira ya suala la DP na Muungano viongozi wote walijitokeza wakilaani na kusema huo ni ubaguzi dhidi ya Wazanzibar hata kama ulikuwa ukweli mtupu.

Jambo linaloshangaza Ubaguzi ukifanywa na Wazanzibar ni jambo la halali.
Si mara moja au mbili, Wazanzibar wameruhusiwa kutukana viongozi , Muungano na Watanganyika 'with impunity'

Hili la Wamasai linaweza kuzaa tatizo, ubaguzi ukianza watakaoumia ni Wazanzibar!

Tahadhari ichukuliwe mapema kwakukemea. Kama Wamasai hawatakiwi Zanzibar isemwe hivyo lakini si kuutusi, kuutukana na kuudhalilsha utamaduni wao ambao Watanganyika wana kila sababu ya kusema 'utamaduni wetu'
 
Back
Top Bottom