QASSEM SOLEIMANI AUAWA NCHINI IRAQ
HALI YA MASHARIKI YA KATI NI TETE
Katika mabandiko 35 kuendelea na yaliyopita tumeeleza hali ya kisiasa mashariki ya kati
Wakati Rais Trump anaingia madarakani tulijadili pia kuhusu changamoto ya M.Kati
Katika wiki kadhaa Marekani imeishutumu sana Iran kuchagiza vikundi vya ''kigaidi''
Shambulio lililomuua Al Baghadad kiongozi wa ISIS lilifanyika miezi michache iliypita
Shambulio hilo limefanywa ''siri'' katika baadhi ya maelezo kama vile ndege zilizomshambulia Al Baghdad zilitokea wapi kwani eneo alilokuwepo lilikuwa mbali na majeshi ya Marekani.
Inaibainika kuwa intelejensia ilisaidiwa sana na serikali ya Iraq, lakini shambulio lilitokea Israel
Inafichwa sana ili kuitenga Israel na mgogoro wa Iran na Waislam wa mashariki ya kati
Israel imechagiza sana Marekani ishambulie Iran baada ya Marekani kujitoa katika nuclear deal
Tulieleza huko nyuma kuwa Marekani ilikuwa inatafuta sababu za kumshambulia Iran
Msaada mkubwa unatoka kwa nchi za Kiarabu kama Saudi Arabia na Israel
Saudia inalazimika kufanya kazi na Israel kwa hofu kubwa ya Iran kuwa mbabe wa M.Kati
Kamanda wa juu wa intelejensia wa Iran Qassem ameuawa akiwa katika airport ya Iraq
Inaripotiwa kuwa Qassem aliuawa akiwa anatoka safarini.
Qassem alikuwa mtu muhimu sana aliyeunganisha vikundi vya SHIA mashariki ya kati kama Hezbollah na vingine vinavyopata misaada kutoka Iran vikiwemo vya Kuds
Kuuawa kwa Qassem kumefanywa na Marekani iliyokiri hivyo, lakini suala hilo limeacha hali ya taharuki Mshariki ya kati kwani Iran inasema itajibu shambulio hilo.
1. Iraq imejikuta kati kati ya mzozo huo. Iraq ina Shia ambao kwa sehemu kubwa walikuwa tatizo kwa Marekani wakiongozwa na Murtada Al Sadr.
Stability ya Iraq inategemea Marekani na Iran. Hata hivyo, Iran ina ushawishi kupitia Shia.
2. Makundi ya Shia Mashariki ya kati kama Hebollah ya Sheikh Hussein Nasrallah na kwingine yanayomuheshimu sana Qassem yamechukizwa na hali hiyo.
3. Israel haitakuwa salama kwani wengi wanaamini yote yanatokea kwa shinikizo la Israel
4. Nchi wanachama wa EU na Washirika wa Marekani hawakujulishwa kuhusu Shambulio
5. Nchi za Mashariki ya kati zenye Shia nazo zina tatizo kukabiliana na hasira za Shia
Kuna hali ya wasi wasi kwamba Iran ikijibu mapigo huenda ukawa mwanzo wa vita nyingine
Tofauti na ile ya Iraq, vita ya Iran itakuwa na athari kubwa katika eneo lote la mashariki ya kati.
Inaendelea....
kamili Charles kilian