Mwalimu pitia kwanza video hiii
TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (LIVE)
Tumeandika kuhusu uteuzi wa Nape. Uzoefu wa chama si uzoefu katika serikali.
Tukaendelea kusema, Awamu ya 5 ipo katika mashaka makubwa katika eneo la habari
Ukisikiliza video , Nape anasema TBC imeondoa baadhi ya vipindi 'live'
Anasema gharama za TBC zinafidiwa na matangazo madogo asilimia 75 ni elimu ya umma na 25 ni burudani
Matangazo yalisitishwa 'live' juzi na jana alishapata habari wananchi wamefurahia
Anadai, kuonyesha 'live' watu wapo katika ujenzi wa Taifa ni tatizo vipindi vitaonyeshwa saa 4-5 usiku , muda watu wengi wanapoangalia TV
Tuzipitie hoja za Waziri wa habari na michezo kama tulivyoziorodhesha hapo juu
1. Kuondoa matangazo 'live' hilo wameondoa kabisa. Hatuna tatizo na kuondoa bali kauli yenye ni hila
2. TBC inajiendesha kwa matangazo madogo Nape hakusema inapata ruzuku asilimia 100 na ''monopoly''
3. Kama asilimia 75 ni vipindi vya elimu kwa umma, maana yake TV ni muhimu na 4 Bilioni si tatizo
4. Eti matangazo yamesitishwa juzi, jana keshafanya tathmini na kubaini watu wengi wamefurahia.
Haya hayawezi kuwa maneno ya serikali. Waziri hana takwimu, hata akiwa nazo masaa 10 hayatoshi kutathmini. Ni propaganda na udanganyifu unaokera na kuudhi umma. Kulifanya Taifa la mabwege
Waziri anasimama bungeni kueleza jambo bila takwimu wala ushahidi
5. Hana takwimu za kuonyesha rating wakati wa 'live' na wakati wa kurekodi.
Akiwa waziri hana mamlaka ya kuelekeza umma ni muda gani watazame TV.
Wapo wanaoangalia TV saa 10 usiku, saa 6 mchana kutegemeana na staili ya maisha na si jukumu la waziri wa habari kujua hilo. TV zinafanyakazi saa 24, Mbona hajauliza usiku wa manane nani anasikiliza radio au TV wakati watu wamelala
Haya ni mambo yasiyo na takwimu/ushahidi wa kutosha bali propaganda za kuufanya umma wajinga
6. Anasema saa 4 had 5 ni muda mzuri wa kuonyesha vipindi vilivyoripotiwa
Waziri hatambui ndio muda watu wanajiandaa kupumzika ili kuamaka Saa 11 kuwahi foleni
Ni muda ambao mzazi anafanya maandalizi ya watoto baada ya wao kupumzika kwa siku inayofuata
Ni wakati wanafamilia wanajadili mambo mengi yanayohusu maisha yaliyotokea au yatakayotokea
Waziri wa habari haelewi utazamaji wa TV unaambatana na masuala mengine ya kijamii.
Ukitazama, alichokifanya ni kuleta propaganda za CCM katika masuala yanayogusa maisha yetu.
Hatudhani 'live au recorded ' ni tatizo. Kinachoudhi/kukera wananchi ni jinsi wanavyofanywa mazezeta
Hili limeamsha hisia na hasira kutoka kwa wananchi
CCM inachukiwa na umma na waziri anafahamu kwa ushaidi.
Serikali tayari ina migogoro na wananchi kwa baadhi ya hatua inazochukua.
Haya yote yanajenga hasira na chuki kwa Rais na CCM
Wananchi wanapomsikiliza katibu mwenezi wa CCM ambaye ni waziri akidanganya, akibadili kauli na kuficha ukweli, akiingilia taratibu za maisha yao, wanaiona serikali kwa jicho la CCM
Tulisema kauli za Nape zitazua matatizo kwa serikali na hilo linaanza kuonekana mapema
Ni vema angebaki katika siasa za chama ambako propaganda zinaishia kwa wanachama wake
Wananchi wanakumbuka '' goli la mkono'' na ile ya majuzi ' serikali ilifikia pabaya sana''
Katika hali ya kawaida, waziri anaamsha chuki na hisia
Kauli zake zinamweka Rais katika mazingira yasiyotarajiwa.
Kwamba, makovu ya uchaguzi hayaponi kama tunavyoona bungeni.
Rais anapata taabu ya kuunganisha taifa kwasababu ya kauli kama za Mh Nape
Mzozo bungeni umesababisha hotuba ya Rais kutopata usikivu na kujadiliwa kwa heshima na kina
Zile propaganda na kauli tulizosema zitaiumiza serikali tulimaanisha haya. Nape anaumiza serikali
Ameanza kuligawa bunge,hotuba ya Rais imekosa heshima stahiki na Taifa limegawanyika
Chuki dhidi ya CCM zinazidi kupanda, makovu ya uchaguzi ''yanavuja damu'' na serikali inadhalilika
Kama Rais angependa utulivu katika kazi zake, kuliunganisha Taifa kama kitu kimoja na kujenga ustawi wa jamii yetu, Waziri wa habari ni JIPU linalohitaji uharaka kulishughulikia.
Vinginevyo tusubiri makubwa zaidi
Tusemezane