Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Sehemu ya II

NCHI ZA WENZETU

Katika nchi za wenzetu , raia hawekwi chini ya ulinzi bila sababu za kufanya hivyo
Na anapowekwa katika ulinzi, kwa muda uliopangwa lazima asomewe mashtaka.

Hairuhusiwi kumkamata mtu bila kumweleza kwanini.
Ikitokea ni weekend au sikukuu, mtuhumiwa atasomewa mashtaka kwa muda uliowekwa.

Isipofanyika hivyo, mtuhumiwa anaachiwa huru. Haki ya dhamana ni ya hakimu

Mwendesha mashtaka ana nafasi kuzuia/kutozuia dhamana kama ilivyo kwa mshtakiwa.Mwamuzi ni hakimu au jaji anayesimamia shauri

KWA TANZANIA
Sheria tulizorithi kwa kiwango zinashabihiana na za mataifa

Inashangaza, mambo yanatendeka kana kwamba sheria ni mali za watu
Kukamata watu limekuwa jambo la maguvu sila kisheria

Imetokea karibuni kiongozi/mwanasheria alipotakiwa kuandamana na polisi.
Alipohoji ipo wapi hati ya kukamatwa, askari hawakuwa na jibu la kisheria

'Sisi tumetumwa' si jibu, kumnyang'anya mtu uhuru ni ukiukaji wa haki za mtuhumiwa

Lakini pia inawezekana kumfikishia mtu ujumbe afike kituo cha Polisi kama anahitajika
Kinachotokea, ni mtu kuitwa kwa mahojiano, kisha mahubusu.

Wapo wanaokamatwa ijumaa ilimradi tu wakalale mahabusu hadi jumatatu mahakama, kwingineko duniani shtaka litasomwa siku yoyote 'ndani ya muda uliowekwa kisheria'

Hapa ieleweke, kuambiwa tuhuma na polisi si sawa na kusomewa mashtaka kwa hakimu

Tunaona mbinu zinatumika kuhakikisha mtu analala mahabusu kama adhabu kabla ya sheria haijachukua mkondo wake

Watu kama waziri, mbunge au wana taaluma wanadhamana katika jamii 'public trust' lakini pia ni public figure

Ndiyo maana wana uwezo wa kutoa dhamana au kujidhamini kulingana na tuhuma

Wito ukitolewa,mhusika kufika anapotakiwa, kuna sababu gani za kumweka mahabusu?

Wapo wanaoambatana na wanasheria, nini kinachosukuma kuwaweka mahabusu?

Na hapa tunaongelea tuhuma au makosa yasiyo na athari za mara moja kwa jamii, usalama au amani.
 
Sehemu ya III

Kutokana na ukiukaji wa haki za raia, matumizi yasiyo sahihi ya madaraka na mamlaka,wenye madaraka/ushawishi hutumia nafasi zao kama 'silaha' kupambana na ''wabaya'' wao iwe katika biashara au siasa .Wanasiasa wamebobea katika tatizo hili.

Ushawishi wao umeingia katika vyombo vya kusimamia haki na sheria za nchi

Wanatumia mamlaka zao kushawishi hatua zichukuliwe kwa minajili tu ya 'kukomoa' na kuadhibu bila kutumia sheria! Yaani wao ndio ''sheria''

Rais alipoongea na wanasheria siku ya mahakama, aliwataka waharakishe kesi za kodi
Alisema, iwapo ushahidi upo uchunguzi gani unaotakiwa tena?

Pengine Rais hakuona ukubwa wa tatizo katika suala la siasa na si biashara na kodi tu

Kesi za kisiasa ni za mazingira tatanishi hadi wanasiasa wanapokamilisha malengo yao.
Watu wanakamatwa katika hali inayoonekana ni ya ubaguzi na 'adhabu'

Wanaadhibiwa bila kusomewa mashtaka, kujitetea au kuhukumiwa

Hivi kwanini aliyesababisha fujo awe huru aliyelalamika aswekwe mahabusu?

Viongozi wanapodai hawabagui wakati ubaguzi unafanywa wakiwa kimya, inafikirisha. Ndio maana tunasema vema viongozi waishi kwa kauli 'walk the talk'

kutotumia madaraka na kukiuka haki za Raia kwa misingi ya kisiasa.

Kupora haki kutumia vyombo vya dola kwasababu za kisiasa ni ubaguzi sawa wa dini, kanda, kabila, jinsia n.k.

Kutozingatia sheria , kukamata watu hovyo, kutowafikisha mahakamani kwa wakati, kuwaachia kwa kukosa ushahidi n.k. ni ukiukaji wa haki na ubaguzi kama mwingine tu

Sheria tumeziandika wenyewe, hatuziheshimu. Viapo vya uongozi
wanakula,hawaviheshimu. Tunaishi kwa sheria tusizoziheshimu wala kuzitumikia

Haki za raia zinakiukwa. Hatuheshimu sheria zetu wenyewe!
Lini tutajifunza kuheshimu sheria zetu tulizojiandikia wenyewe?

Viongozi wakisema hawabagui, hawanana budi kuishi kwa kauli zao!

Na wananchi, ifike mahali tuone ubovu wa mfumo tulio nao!

Tusemezane
 
UTIIFU NA UHESHIMU WA SHERIA 'LAW AND ORDER'

TUNAYOYAONA YAPO KATIKA MSINGI GANI?

Kazi za vyombo vya dola ni kusimamia(enforce) utii na uheshimu wa sheria zilizowekwa
kutoa haki katika utekelezaji, wahusika 'hawafumgamani' na siasa

Sheria na miiko katika majukumu yao ni kutoa haki bila upendeleo,ubaguzi au uonevu

Upendeleo:
Unatokea kundi au mtu anapopata fursa zaidi ya mwingine katika mazingira yale yale

Kwa mfano, kuna watu 'wamehojiwa na kupewa dhamana' Zanzibar kwa kutoa matamshi ya 'uchochezi'ambalo nikosa kwa mujibu wa sheria na pengine ndio sababu za kukamatwa

Wapo watu walioandika mabango ya ubaguzi ambalo ni kosa kwa sheria za nchi.
Mabango yaliyolenga kuchochea hisia za kibaguzi kati ya makundi ya jamii.

Huo ni uchochezi kwa misingi ya ubaguzi. Hao hawakuitwa 'kuhojiwa'

Huu ni ndio upendeleo ambao unazaa jambo jingine, ubaguzi

Ubaguzi: Jamii inapotengwa kwa lengo na nia ya kubagua ni kosa kisheria

Ubaguzi ukitendeka unazaa tatizo jingine, uonevu

Uonevu: Ni kutendewa kinyume cha haki au haki kutolewa kwa ubaguzi na upendeleo

Hali kama hiyo imeonekana Dar es Salaam
Wapo viongozi wa serikali waliofikisha taarifa za kuahirisha uchaguzi. Ikatokea vurugu

Vyombo vya dola vikawaweka mahusubu baadhi , waliosababisha wakiwa salama

Swali la kujiuliza, mambo kama haya yanatueleza nini katika jamii?

Yanatokea kwa bahati mbaya au yamepangwa?
Ni kwa lengo gani na akina nani wapo nyuma yake

Ile law and order inatendekaje katika mazingira ya namna hii?

Unapokuwa na haki na dhuluma katika chungu kimoja, nafasi ya amani na utulivu ipoje?

Tusemezane
 
''LAW AND ORDER''

ZNZ: RAIA HURU WAPEWA 'DHAMANA' BAADA YA MAHOJIANO

Raia anabaki kuwa huru hadi pale vyombo vya kutoa sheria vitakapoamua vinginevyo

Mahojiano ni maongezi kati ya kundi, watu, mtu na watu , kundi, taasisi n.k. katika kuafikiana, kudadisi au kutafuta ukweli. Mahojiano si tuhuma wala makosa

Kilcihotokea Zanzibar kinaacha vichwa vikizunguka kuhusu vyombo vya dola
Watu wawili maarufu wametumiwa taarifa za kufika polisi kwa maohojiano

Waliambatana na wanasheria wao. Mmoja wao akatakiwa alete wadhamini.
Mwanasheria alipoondoka, mhojiwa akawekwa mahabusu!!!

Wote wapo nje kwa ''dhamana''. Haijulikani kama wamesomewa mashtaka

Hawa ni raia huru walioitwa kwa maojiano nwakajikuta mahabusu
Walioitikia wito walikuwa na hatari ipi kwa jamii kuwekwa mahabusu?

Laiti wangalitaka kukimbia, wangalifanya hivyo waliopeletewa ujumbe wa mahojiano
Mahojiano yakawa tuhuma. Kwamba, watuhumiwa wamepewa 'dhamana'

Swali la kujiuliza, raia waliokwenda mahojiano na kuwekwa mahabusu walikuwa na tuhuma tu. Tuhuma hazimfanyi mtu awe na hatia

Chombo kinachoweza kumtia mtu hatiani ni mahakama.
Watuhumiwa hawakufikishwa kwa wakati huo, wakapewa ''masharti ya dhamana''

Lini Polisi wamepewa jukumu la kuamua dhamana kabla ya kufikishwa mahakamani?
Ni dhamana ya nini, mahojiano au tuhuma walizoambiwa wakiwa kituoni?

Na tuhuma hizo zimesomwa katika chombo gani cha sheria ili kukidhi haja ya dhamana?

Dhana tunayoongelea hapa ni ngumu na inachanganya kidogo.
Raia aliyekwenda kwa mahojiano analazimika vipi kuomba dhamana kurudi nyumbani?

Na kama imebainika lipo shauri lini wamefikishwa mbele ya sheria?
Na kama hakufikishwa mbele ya sheria, shauri wanaloombea dhamana ni lipi?

Ni shauri kwasababu dhamana inapotoka bado linabaki shauri katika hali ya tuhuma. Itakuwa kosa pale tu mtuhumiwa atakapotiwa hatiani na kuhukumiwa

Katika muda wa kisheria hawakufikishwa mahakani shauri lizungumzwe, wakaambiwa watafute dhamana kurudi makwao na waripoti kituoni!

Pengine lipo tusiloelewa, tukiri jambo hili linachanganya!



Tusemezane
 
WAZIRI ANAPOWAFANYA WATANZANIA MAJUHA

ASHINDWA KUKEMEA UHUNI , AJIKOSHA KIDANGANYIFU

waziri huyu ni timu ya #Hapakazi


Home English
Home Swahili

Tumezungumzia sana sualala Umeya linavyoleta aibu.

Aibu ipo maeneo mawili;
kwanza, kushindwa kupata Meya kwa miezi 3 kwasababu za kipuuzi tu

Pili, kushindwa huko kupo chini ya Tamisemi, wizara chini ya Rais

Hakuna namna yoyote mtu mwenye akili timamu na uwezo wa kufikiri anaweza kulieleza suala hili kwa lugha nyingine kama si uzembe, kufeli kwa waziri anayemsaidia Rais

Ukisoma link ya gazeti hapo juu, waziri anatoa amri uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 25

Waziri anasema ni amri, hakuna sababu za wakazi wa Dar kutokuwa na uongozi

Waziri anaeleza kulaumiwa na makada wa CCM kwa kushirikiana na wapinzani

Kwakweli waziri anaitia serikali aibu hasa ikzingatiwa wizara ipo chini ya ofisi ya Rais

Waziri hakuwahi kutoa amri kabla, alikaa kimya CCM ikichelewesha uchaguzi kipuuzi

Majuzi katibu tawala na mwanasheria walipofuta uchaguzi waziri''hana habari ni kwanini''

Waziri alikaa kimya CCM ikifanya utoto anaudanganya umma analaumiwa na CCM

Hizi ni siasa muflisi, siasa za kijima na siasa zisizoitakia nchi hii mema.

Waziri angekaaa kimya ingemsaidia Rais kuliko kauli zisizoonyehsa weledi au uaminifu

Waziri hakuwahi kuingilia mgogoro huo kwavile CCM wanataka kupora haki ya wananchi

Pili, waziri hakuwahi kutoa amri, leo nguvu za kutoa amri anazipata wapi

Hapa tusisitize baada ya kuandikwa na vyombo vya habari akihusishwa na mgogoro na kuitia ofisi ya Rais aibu,anajitokeza kutoa kauli aliyotakiwa kuitoa mwezi wa 11.

Bado tunaaminishwa huyu naye ni sehemu ya #Hapakazi

Tatu, waziri aliyeshindwa kupata ushahidi kutoka kwa msajili wa mahakama hana mamlaka ya kiroho (moral authority) kuongelea uchaguzi, alishindwa na kufeli

Nne, waziri anatoa amri ya kurudia uchaguzi wakati hajaeleza kwanini uliahirishwa.

Anachokifanya ni kuaminisha umma eti CCM anaowalinda wanamlaumu.

Haya yanatia kinyaa na ushahidi kuwa serikali hii ni mwendelezo wa iliyopita

Waziri alitakiwa kuwachukulia hatua waliovuruga uchaguzi, hakufanya hivyo.

Anajua ni mpango ulioratibiwa ,kuwachukulia hatua ni kuwaonea.Anajua!!!

Katika hali kama hii, wananchi wasitegemee lolote jipya kutoka serikali hii.

Mfano wa waziri unaeleza utamaduni wa lugha za kilaghai na siasa za ajabu nchini

Wizara ya Tamisemi ipo chini ya ofisi ya Rais, madudu , wanasiasa waongo na watu wazembe kama hawa wanaushawishi umma majipu ni mambo ya mpito.

Haiwezekani Rais aishi na waziri aliyeshindwa kazi kama huyu

Hawa wanaitia nchi umasikini. Hasimamii sheria au ukweli, ilimradi tu lugha za hadaa

Tusimame na kulaani kauli za waziri huyu za kuulaghai umma na kumtia Rais aibu

Mh Waziri, CCM hawawezi kumlaumu mlinzi wao ambaye ni wewe uliyekaa kimya miezi mitatu madudu yakiendelea. Umeshindwa kazi na kutitia ofisi ya Rais aibu

Mh, nawe pia ni sehemu ya timu ya Hapakazi? Kama ndivyo, hakuna jipya wala jipu

Tusemezane
 
UMEYA WA DAR
AIBU ISIYO YA LAZIMA KWA TAIFA

HATUWEZI KUSHINDA KATIKA HALI HII

Tafadhali rejea mabandiko #117,118, 119, 120,131 kuhusu suala la Umeya

Tulisema ni aibu kubwa sana kwa Taifa kuchukua miezi 4 kupata Meya
Aibu hii imetendwa na CCM kwa makusudi kabisa

Rais alisema hili ni aibu lifikie mwisho, kauli iliyochelewa ikitueleza zaidi ya tunayojua

Uchaguzi wa marudio wa ZNZ umemalizika kukiwa na hali ya simanzi

Hali ya simanzi kuhusu hatma ya Taifa na uongozi
Hali ya taharuki mbele ya uso wa dunia na hali ya kusikitisha kwa Tanzania ya leo

Tunafahamu yalikuwepo matukio yasiyo ya kawaida visiwani. Kamata kamata , Zombi n.k.

Matokeo yalitangazwa hata washiriki wakiona ''aibu'' wenyewe. Ni hali ya kusikitisha

Kwa kujua hilo, ilitafutwa mbinu ya kufunika habari za ZNZ kwa hili la umeya kukamilika

Kwamba habari kubwa iwe uchaguzi wa Meya na si mazingaombwe ya ZNZ

Uchaguzi wa Meya hakupaswa kuchukua muda mrefu kiasi hiki.

Hili ni suala la wizara ya Tamisemi chini ya ofisi ya Rais.
Kwa kasi inayoelezwa, kama hii ndiyo kasi yenyewe tuna safari ndefu

Waliochelewesha uchaguzi, waliofanya madudu wakwemo katibu tawala, mwanasheria wa Jiji na waziri husika wapo katika nafasi zao wakiendelea na kazi

Tunahoji, kauli ya umeya kutia aibu ilikuwa ya dhati kweli?
Kama ni ya dhati wahusika waliochelewesha uchaguzi wamechukuliwa hatua gani?

Hatudhani hili ni suala la bahati mbaya tukijua lipo chini ya ofisi ya Rais

Ni suala linaloonekana kupangwa likutane na lingine ili kufunika moja

Kama tulivyowahi kusema, ni aibu kwa Taifa, na katika hali hii ya 'kudanganya' umma kwa kutumia ucheleweshaji hadhi ya serikali kuwa inasimamia hapakazi imeharibika

Tuliwahi kusema ni muhimu kutenda yanayohubiriwa 'walk the talk'

Awamu ya tano hainonekani kuwa tofauti na hapa ndipo tunajiuliza, haya ndiyo mabadiliko yanayohubiriwa?

Kipi kimebadilika kuliko mwaka jana? CCM inayobadilika ndiyo hii tunayoona?

Kwa hili serikali imefeli na wananchi watapoteza imani waliyoanza kuijenga

Hatuwezi kujenga Taifa la maendeleo katika mambo ya aibu kama haya!

Tena yakifanyika mbele ya wanaotuambia tukimbie wao wakitambaa

Tusemezane
 
Ninapenda kutazama dhana ya mfumo katika namna mbili tofauti lakini zinazofungamana kiundani;
A: Mfumo, ni muunganiko wa taratibu, kanuni, sera, itikadi, sheria, desturi, imani, n.k. zenye kufungwa/kubeba dhana kuu moja na kufanya zifungamane/ziumane/zihusiane/zitegemeane. Dhana tofautitofauti zinazofungwa na dhana kuu moja(DIRA YA TAIFA), huo ndio mfumo. Kama Taifa, hili kwetu ni uozo na kelele zake hazijaanza leo.

B: Mfumo ni kundi la watu wenye nguvu na mamlaka ndani na nje ya serikali, lenye kubeba malengo sawa ya aidha kuilinda au kuikiuka katiba kwa maslahi yao binafsi, au lenye malengo ya kuilinda au kuikiuka katiba kwa masilahi ya umma. Wapo waunganao kuilinda masilahi ya umma, lakini pia wapo wale walindao masilahi yao binafsi.

SWALI:
a. Kama wapo wakiukao sheria kulinda masilahi yao binafsi, je kuna ubaya gani wa kuikiuka sheria hiyo hiyo kulinda masilahi ya umma?
b. Kama mfumo/katiba katika sehemu A ni uozo, i wapi nafasi ya wale waitiiyo au waikiukayo?
 
Ninapenda kutazama dhana ya mfumo katika namna mbili tofauti lakini zinazofungamana kiundani;
A: Mfumo, ni muunganiko wa taratibu, kanuni, sera, itikadi, sheria, desturi, imani, n.k. zenye kufungwa/kubeba dhana kuu moja na kufanya zifungamane/ziumane/zihusiane/zitegemeane. Dhana tofautitofauti zinazofungwa na dhana kuu moja(DIRA YA TAIFA), huo ndio mfumo. Kama Taifa, hili kwetu ni uozo na kelele zake hazijaanza leo.

B: Mfumo ni kundi la watu wenye nguvu na mamlaka ndani na nje ya serikali, lenye kubeba malengo sawa ya aidha kuilinda au kuikiuka katiba kwa maslahi yao binafsi, au lenye malengo ya kuilinda au kuikiuka katiba kwa masilahi ya umma. Wapo waunganao kuilinda masilahi ya umma, lakini pia wapo wale walindao masilahi yao binafsi.

SWALI:
a. Kama wapo wakiukao sheria kulinda masilahi yao binafsi, je kuna ubaya gani wa kuikiuka sheria hiyo hiyo kulinda masilahi ya umma?
b. Kama mfumo/katiba katika sehemu A ni uozo, i wapi nafasi ya wale waitiiyo au waikiukayo?
Ahsante kwa mchango unaofikirisha sana

Kwa nchi yetu mfumo umebeba maana zote mbili ulizotaja hapo juu

Kwa dhana ya kwanza, mfumo unatakiwa uwe kama ulivyoanisha na tusemavyo kila siku

Kwa bahati mbaya mfumo wetu umeoza, hautii wala kufuata kanuni za mfumo na hivyo kuwa disqualified kwa maana ya mfumo.

Labda neno mtindo lingeweza kuwa na maana kwa mtazamo wa nchi yetu kuliko mfumo

Maana ya mfumo kwa hoja ya pili(B) ipo wazi kama yale tuliyoyaona uchaguzi mkuu 2015

Tukirudi katika maswali yako
a) Kwavile mfumo wetu mbovu ndio unaweka viongozi, watu hao wanautumikia mfumo kwanza kabla ya taifa. Kwa maana hiyo watakiuka katiba kulinda masilahi yao binafsi.

Hawawezi kukiuka katiba kulinda masilahi ya umma kwasababu umma hauna nguvu mbele ya walioweka mfumo na wanaotumikia

b) Kwa wale wanaoutii mfumo utiifu wao hautokani na utashi, ni utiifu wenye makando kando 'strings attached' .

Wale wanaoukiuka nafasi yao ni kubwa, hakuna kinachowazui kutenda watakalo.

Na kwa hoja zako, tunashawishika kutumia mifano halisi tunyaoishi nayo, kuonyesha kwa uhalisia maana za mfumo mbaya kama tulivyowahi kuzijadili na kama ulivyojadili

Kupitia mifano hiyo, tunaweza kupata chembe ya majibu kutokana na maswali yako

Lipo tatizo linalozungumza sasa kuhusiana na kampuni iliyopewa kazi na serikali
Tatizo lililopo si maudhui ya kazi, bali jinsi gani mfumo unavyoweza kujibu hoja za tatizo


Tuangalie ni wapi mfumo unaposhindwa

Tusemezane
 
Nguru ninakufuatilia vizuri sana katika huu uzi, ni mchanganuo makini sana, big up na endelea kuchambua so long as it take. usisahau kufikiria kuchapisha kitabu pia
 
Ahsante kwa mchango unaofikirisha sana

Kwa nchi yetu mfumo umebeba maana zote mbili ulizotaja hapo juu

Kwa dhana ya kwanza, mfumo unatakiwa uwe kama ulivyoanisha na tusemavyo kila siku

Kwa bahati mbaya mfumo wetu umeoza, hautii wala kufuata kanuni za mfumo na hivyo kuwa disqualified kwa maana ya mfumo.

Labda neno mtindo lingeweza kuwa na maana kwa mtazamo wa nchi yetu kuliko mfumo

Maana ya mfumo kwa hoja ya pili(B) ipo wazi kama yale tuliyoyaona uchaguzi mkuu 2015

Tukirudi katika maswali yako
a) Kwavile mfumo wetu mbovu ndio unaweka viongozi, watu hao wanautumikia mfumo kwanza kabla ya taifa. Kwa maana hiyo watakiuka katiba kulinda masilahi yao binafsi.

Hawawezi kukiuka katiba kulinda masilahi ya umma kwasababu umma hauna nguvu mbele ya walioweka mfumo na wanaotumikia

b) Kwa wale wanaoutii mfumo utiifu wao hautokani na utashi, ni utiifu wenye makando kando 'strings attached' .

Wale wanaoukiuka nafasi yao ni kubwa, hakuna kinachowazui kutenda watakalo.

Na kwa hoja zako, tunashawishika kutumia mifano halisi tunyaoishi nayo, kuonyesha kwa uhalisia maana za mfumo mbaya kama tulivyowahi kuzijadili na kama ulivyojadili

Kupitia mifano hiyo, tunaweza kupata chembe ya majibu kutokana na maswali yako

Lipo tatizo linalozungumza sasa kuhusiana na kampuni iliyopewa kazi na serikali
Tatizo lililopo si maudhui ya kazi, bali jinsi gani mfumo unavyoweza kujibu hoja za tatizo


Tuangalie ni wapi mfumo unaposhindwa

Tusemezane

Nimekupata Mkuu.
Hoja yangu hapa imejikita katika kutafakari hali tatanishi inayoendelea kwa walio wengi, na katika hilo nimejikuta katika matokeo hayo hapo juu.. kuwa;-

Kwa Tanzania kama Taifa, mfumo kama sehemu A ni uoozo mkubwa hivyo kuutii ni upumbavu uliopitiliza, na huo mfumo A umewekwa na mfumo kama sehemu B, kuutii mfumo A ambao ni uozo ni kulinda tu masilahi ya waliouweka si umma, kwani haufai kitu. Kutoutii mfumo kama sehemu A ni kuuepusha uozo wake kwa umma, na pia tuzingatie kuwa Mfumo kama sehemu A husimikwa na mfumo kama sehemu B. Si jambo la kuamka na kuukuta inahitaji HESABU NDEFU zinazoongozwa na dhamira na dhati ya kweli kuusuka.

Mfumo mbovu hutiiwa na watu waovu, wema huukiuka na kuuepuka, kelele za Ukiukaji zatoka wapi?
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani, Anaita sasa!
 
Mfumo mbovu hutiiwa na watu waovu, wema huukiuka na kuuepuka, kelele za Ukiukaji zatoka wapi?
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani, Anaita sasa!
Natumaini katika hoja hii umehoji wale wema , sauti zao zi wapi?

Kuna sehemu mbili katika hili
Kwanza, wananchi wengi hawaelewi haki zao. Hili linachagizwa na umasikini

Kwamba, wapo tayari kuuza haki zao kwa mkate wa siku, si wa siku zijazo

Umasikini unachangia weledi, na ndilo linalotumiwa na watiifu wa mfumo mbovu kuendelea na mambo yao.

Sehemu ya pili ni wale waliobahatika kuwa na weledi.
Hawa hawana umasikini, wana ubinafsi.

Kwamba, matumbo yao ni muhimu sana kuliko masilahi mengine.

Wanasahau kuwa kupitia kodi za masikini wameweza kupata mwanga wa elimu

Wanatumia elimu waliyoipata kwa gharama kubwa kuwasaliti masikini

Kundi hili la wasaliti ni la wasomi wa kada zote.
Kuanzia chini hadi ngazi yoyote unayojua. Ni kundi baya kuliko lile la wananchi masikini.

Linatumia elimu kulaghai ilimradi tu liendelee kulimbikiza.

Linatumia elimu si kama nyenzo ya kuboresha maisha ya umma bali chombo cha kujilimbikizia mali za umma. Kundi linaishi kwa kujipendekeza

Hili kundi ndilo lilipaswa kuongoza katika kusimamia 'kelele' dhidi ya mfumo mbovu.

Utakubaliana nami kuwa wasomi wetu wamegundua njia ya mkato, kuendelea kuungana na 'waouvu' ili waendeleze masilahi yao binafsi

Taasisi zinafanyaka kazi si za kutumikia umma, bali wale wanaoziweka na kuteua wasomi.

Mfano rahisi, tullipokuwa na matatizo ya uchaguzi kote bara na visiwani, ni kana kwamba nchi haikuwa na watu wenye weledi. Walikaa kimyaa!

Hakuna aliyesimama na kusema hili hapana hili ndiyo

Tuliwaona wakipigana vikumbo katika TV kubabaisha umma. Hawasemi kilicho cha kweli.

Vyama vya kitaaluma, vyombo vya habari n.k.
vyote vilinywea kana kwamba mambo yalikuwa shwari hata pale yalipokuwa kombo

Katika mazingira hayo wanaotumikia mfumo mbovu wananeemeka.
 
REJEA BANDIKO #36 (WIZARA YA HABARI, MICHEZO NA UTAMADUNI)

Katika bandiko hilo tumezungumzia Waziri husika katika namna mbili.

Kwanza, kama katibu mwenezi wa CCM ambaye kazi zake ni za kichama
Na pili tumemueleza kama Mh Waziri wa habari , michezo na utamaduni na sanaa

Tulizungumzia umakini unaohitajika kutofautisha kofia mbili, yaani ya chama na ile ya serikaliTukasema kunahitaji umakini,yapo yanayoweza kuichanganya jamii na kuigawa badala ya kuiunganisha
Katika bandiko hilina 36, tulieleza kwa uchache matatizo yanayoweza kutokea waziri anaposhindwa kutofautisha shughuli za chama na za serikali.

Tulisema, Waziri Nape alikuwa kada na hivyo kauli zake na matendo ni ya kichama

Akiwa waziri, si kada wa chama. Ni kiongozi wa serikali na nchi.
Endapo hatatofautisha hayo mwili, ataleta mgogoro katika jamii usio wa lazima

Katika mabandiko mengine tumezungumzia suala la kurusha matangazo.
Tulieleza waziri alivyovuka mipaka na kusahau nafasi ya utumishi wa umma si chama

Kauli ya kwanza ya waziri ilikuwa kufuta matangazo kwasababu serikali haina pesa bilioni 4 kwa mtangazo kupitia kituo cha TBC kinachomilikiwa na umma

Tulizungumzia hoja ya waziri, kwamba bilioni 4 si kiasi cha nchi kushindwa kurusha.
Lau kingalikuwa, TBC isingetoa matangazo masaa 24 tena ya vipindi hovyo.

Tulihoji, iweje vyombo binafsi viweze na serikali ishindwe?

TBC imepewa monopoly hata kulazimisha vyombo binafsi kutoa matangazo yake

Inafanya biashara kama vyombo binafsi na inapata ruzuku kutoka serikali.
Hivyo gharama haikuwa sababu ya kuzuia matangazo

Ghafla tukasikia waziri akisema, ameambiwa na watu wengi kurekodi vikao vya bunge iliwapa faraja. Waziri alitoa kauli hizo siku si zaidi ya 7 kutoka tangazo lake.

Hakueleza kitakwimu 'watu wengi' ni kiasi gani , alifanya utafiti wapi na kwa njia zipi

Tulieleza, jukumu la wananchi kutoangalia au kuangalia TV si la serikali.
Jukumu la serikali ni kuheshimu uhuru wa habari kwa mujibu wa katiba

Hoja ya kwamba wananchi wapo makazini si kweli. Wanaweza kuwa nyumbani wakiangalia CNN, KTN au BBC. Mantiki ya hoja ya mh waziri ipo wapi?

Kauli hizi zilielekea katika propaganda ya jambo la kitaifa.

Mh waziri alidhani propaganda za kichama zinanya kazi mazingira ya umma wote.

Bila kupima uzito wa matamshi, aliwaingiza viongozi katika kwa kauli wanazojutia

Amechaonganisha umma na serikali na hata kufikia mahali umma una hoji, nini kinafichwa? Dhamira ya hili jambo ni njema? Kuna nini nyuma ya pazia?


Inaendelea...
 
UGOMVI WA UMMA NA CCM/SERIKALI

Wakati waziri wa habari anaendelea na ''propaganda'' ukatokea mfuko wa wakfu uliotaka kudhamini matangazo hayo kwa mwaka mzima. Waziri hakujibu hilo

Ghafla bunge likaingilia kati na kujenga kituo cha matangazo.

Lengo likiwa kuwa chanzo pekee cha habari za bunge kama 'mabunge ya Jumuiya za madola'' Hili nalo linasikitisha, je bunge letu linazingatia yale ya ''jumuiya ya madola?

Je, kamati za bunge na mgogoro wake ulizingatia taratibu za mabunge ya madola?

Utaratibu wa studio za bunge uliambatana na marufuku kwa waandishi wasibebe zana zao za kazi ndani ya ukumbi wa bunge kama kamera

Bunge na CCM kupitia waziri walilenga kuhakikisha habari zinachujwa na kurushwa kwa kurekodiwa kwa namna wanavyotaka. Hili linazidi kutia hofu ya nini kinafichwa?

Bunge ni mkutano wa wazi, iweje serikali ihangaike kuzuia habari zake?

Bungeni
Serikali kupitia waziri mkuu ikatetea hoja ya Nape ya waziri kwa nguvu kabisa

Rais: Akihutubia wanasheria aliungana na waziri kutetea hoja ya gharama kwa nguvu kabisa akitolea mfano wa mahakama ilivyokataa 'live' kwa gharama

Vongozi wetu waliongozwa na kauli za waziri ambaye siku za karibuni amekana suala hilo halikuanzishwa na serikali na ni la bunge. Anakimbia 'mgogoro' alioanzisha

Waziri anakana wakati serikali na viongozi wake wakitetea kauli zake.

Mh waziri ametaka wadau waunde kamati kuliangalia suala kwavile linazungumzika.

Tayari kaonyesha kubadili msimamo baada ya nguvu ya kauli ya umma.

Haishangazi waziri kubabaika,amekulia katika utamaduni wa chama bila kutambua majukumu yake ni ya umma. Utamaduni wa chama kudanganya hata mchana kweupe

Ni Mh waziri huyu aliyekitia chama chake katika matatizo kwa kauli ya 'CCM kushinda kwa bao la mkono' jambo linalozizima masikioni mwa wananchi hadi sasa

Inaendelea..
 
Mh WAZIRI WA HABARI ASIBADILI MSIMAMO

Katika mazingira yaliyotokea, wananchi wanatambua hakuna sababu za mashiko za kuzuia matangazo ya bunge. Zipo sababu wasizoambiwa zinazopelekea hali hiyo

Suala la gharama, studio, muda wa kazi n.k. hazina ukweli bali propaganda.

Ni kwa mantiki hiyo, waziri hana sababu za kukana kuanzisha 'mgogoro huu'

Na wala hana sababu za kubadili msimamo wa kuzuia matangazo
Matatizo ya kubadili msimamo ni makubwa zaidi ya kubaki na msimamo uliopo.

Kwanza, tayari amechonganisha umma na 'serikali yao'

Pili,ameliweka bunge katika wakati mgumu, likionekana kupoteza nguvu

Tatu, viongozi wakuu waliosimama naye hawataeleweka mbele ya umma

Nne, wananchi watapoteza imani na matamako ya viongozi wa serikali

Tano, jambo hili linaonekana kama mbinu za CCM kuficha maovu

Ni vema waziri akaacha kubadili msimamo wake wa awali wa kuzuia matangazo.

Ikitokea hivyo, kazi ya kwanza itakuwa kuomba umma radhi kwa kauli za kupotosha, viongozi wake kwa kuwapotosha na mwisho kukiomba chama chake radhi

Mzigo huu wa kuicha maovu unanasibishwa na ufisadi wa CCM, hata kama si kweli.

Wananchi watakapobaini serikali imebadili msimamo huku viongozi wakuu wakisema dhamira ni kubana matumizi, ni rahisi kusema 'kuna kukurupuka'

Je, mh waziri angependa neno kukurupuka lihusishwe na viongozi wake wakuu?

Na kwa upande wa serikali, hata kama itaridhia kubadili msimamo, ni vema ikaonyesha kuchukizwa na upotoshaji unaoleta sintofahamu katika jamii

Viongozi wanachaguliwa kuongoza na si kuwa chimbuko la mitafaraku

Katika kuonyesha kuchukizwa, Mh Waziri wa habari apangiwe kazi nyingine

Tusemezane
 
HATUA HIZI NI SAWA LAKINI ZINA DOA
LUGUMI NI TATIZO KWA AWAMU YA TANO

Wiki hii yamatokea mambo kadhaa yenye kuleta fikra.

Huko Bungeni wizara kivuli ya mambo ya ndani ilisusia kutoa hotuba, kisa ni kugusia mambo ya uuzwaji wa nyumba, na mikataba tata ukiwemo wa Lugumi

Picha nzima ilionyesha kuwepo na 'kinga' dhidi ya tuhuma kutoka kwenye kiti

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, waziri wa mambo ya ndani alitoa majibu akiwa amelewa jambo lililopelekea utenguzi wake mara moja.

Wizara ya mambo ya ndani ni wizara nyeti za nchi. Ndiyo yenye mamlaka zinazosimamia sheria kama Polisi inayoshughulikia usalama wa Raia na mali zao

Kitendo cha waziri kuingia bungeni akiwa amelewa si tu kilikuwa utovu wa nidhamu bali ukiukwaji mkubwa wa kanuni za utumishi kwa kiongozi aliyepaswa kuonyesha mfano

Hatua ya 'kumtumbua' ni sahihi kwasababu hakukuwa na namna ya kuficha uozo ule.
Hata hivyo, hatua hiyo inafunikwa na makando kando mengine

Gazeti la Mwananchi siku chache zilizopita liliandika kuhusu ufungwaji wa vifaa vinavyolalamikiwa kuwa na ufisadi vikihusisha kampuni ya Lugumi.

Katika tuhuma, ipo kampuni inayosemekana kuwa na masilahi na ''waziri mtumbuliwa''

Gazeti limeeleza kwa undani maeneo vifaa hivyo vinapofungwa.

Likaeleza jinsi ambavyo kamati ya bunge PAC inayochunguza suala hilo ilivyocheleweshewa pesa kuanza kazi ya uchunguzi

Hapa kuna hoja,ucheleweshajwi umefanyika kutoa nafasi ya wahusika kufunga vifaa.

Hizi ni hisia zinazozunguka katika maongezi ya kawaida ya wananchi.

Ikizingatiwa kuwa bunge nalo lilikataa suala hilo kujadiliwa, huku kamati yake ikicheleweshwa kwa pesa za kutimiza wajibu, na ikizingatiwa pia ufungaji wa vifaa unaendelea kama ilivyoripotiwa na gazeti, wasi wasi wa nini kinaendelea unazidi ukubwa wa subira ya matokeo

Mchanganyiko huo pamoja na uwajibishwaji wa waziri, unaacha maswali kuliko majibu. Ni kweli tatizo la waziri lilikuwa ulevi tu au linahusishwa na Lugumi kwa njia nyingine?

Hakuna anayeweza kujibu kwa uhakika, kwani waziri anawajibika kwa Rais na ni haki msaidizi huyo kuondolewa wakati wowote na mteule wake

Jambo ambalo ni wazi ni kuwa, suala la Lugumi linafunika kila hatua inayochukuliwa

Utaratibu wa 'kufunika' tatizo kuanzia bungeni na hizi harakati za kufunga vifaa zikiambatana na 'kuikwaza' kamati husika inatoa picha mbaya kwa serikali

Suala la Lugumi litahusishwa na kila hatua, litakuwa kipimo cha kila hatua na litakuwa ndiyo 'bar' ya utendaji wa serikali kwa kuzingatia kauli zake na maadili kwa ujumla

Ni vema serikali ikaliona hili kama tatizo,jawabu si kulifunika bali kuacha mkondo wa shEria za asili 'natural justice' ufanye kazi zake. Kwamba, ukweli ujulikane bila kificho

Tumeshuhudia matatizo kama Richmond ,n.k. yakIfunikwa na kujirudia kila siku.

Hatuoni Lugumi kuwa tofauti, na linapofungamanishwa na utendaji wa serikali ni mbaya

Serikali ijiulize, kila inapofanya jambo likahusishwa na Lugumi , je hilo ni jambo jema?

Lugumi itaendelea 'kuitesa' serikali hadi lini? Kwanini kuna kila 'namna ya ' kulifunika?

Tusemezane
 
MAWASILIANO NA HADHRA

NINI KINATOKEA AWAMU YA TANO?

Imekuwa kawaida watu kulinganisha viongozi na Mwalimu Nyerere ni 'Std'

Mwalimu alijaliwa katika mambo kadhaa na adhimu kwa wengi

Kwanza, alikuwa na kisimati (Charisma) ya kupendwa/mvuto
Pili, kujieleza na kuwasiliana na umma. Tatu,kiongozi na mtawala

Mwl alitumia mchanganyiko huo kuvuta/kuwasiliana/ kuongoza na kutawala.

Lakini pia mwl alikuwa ana kitu kingine , uwezo wa kutawala lugha kwa asili
Si kila mmoja ana sifa hizi, wapo wenye mapungufu yasiyoondoa uwezo wao

Mfano,
waziri mkuu(PM) John Malecela ana uwezo mzuri wa kujieleza na charisma
Ndiyo maana alikubalika kama Mwanadiplomasia

PM mstaafu CD Msuya hakuwa na uwezo wa kujieleza bali utendaji
Alikubalika kama administrator mzuri sana

PM Salim Ahmed, alikuwa na uwezo wa kujieleza/charisma na utendaji
Mwanadipolomasia na kiongozi

PM mkuu Warioba ana uwezo wa kujieleza ingawa siyo naturally
Uwezo wa kujieleza unatokana na taaluma yake si wa asili (mwanasheria)

PM Mzee Kawawa, hakuwa na uwezo wa kujieleza au charisma
Alikuwa na uwezo wa kuhamasisha sana

PM Sumaye, hana uwezo wa kujieleza wala charisma
Ni mtawala tu

PM Lowassa, ana uwezo wa kujieleza na charisma
Anakubalika na ana ushawishi wa hali ya juu

Rais mstaafu Mwinyi alikuwa na uwezo wa kutawala lugha na charisma
Rais mstaafu Mkapa hakuwa na uwezo wa kutawala lugha wala Charisma
Rais mstaafu Kikwete alikuwa na uwezo wa kutawala lugha, na charisma

Kuwa na sifa au kukosa sifa hizo hakumfanyi kiongozi kuwa mzuri au mbovu

Kitu cha muhimu ni kama mtu huyo anatambua mapungufu na anayatawala

Kwa mfano, PM Msuya anatambua hakuwa na uwezo wa kujieleza
Alizungumza kile alichokiona bila kujali kitamfurahisha au kumuudhi mtu.

Alijiepusha na maneno au malumbano yasiyo na ulazima
Msuya aliheshimika kutokana na uwezo wake wa utendaji unaolingana na kauli zake.

Tunayaeleza haya ili tupate japo picha ya haraka.
mada yetu halisi inamhusu Rais Mh Magufuli anavyojieleza au kuwasiliana na umma.

Ni muda mfupi akiwa kiongozi, zipo hoja kuhusiana na hotuba au kauli zake.

Tutaangalia nini hasa kinaendelea na kupelekea mijadala inayomhusu

Inaendelea
 
MAWASILIANO

Kama kuna kitu chenye utata kutoka kwa Rais ni mawasiliano

Tumetoa mfano wa Mzee Warioba.
Kiasili si mzungumzaji, lakini taaluma ya sheria inamsukuma kama takwa la mawasiliano

Rais Magufuli si mzungumzaji kiasili na kitaaluma ni mwanasayansi
Rais ni mtu wa kutenda kuliko kulumbana tangu akiwa waziri

Kazi aliyo nayo sasa inamlazimu awe katika nafasi anazoweza kubadilika.
Kwanza, ni kiongozi wa umma, kuongoza ni mawasiliano na wafuasi.

Pili, ni mlezi wa Taifa , lugha yake na mawasiliano vinapaswa kuliona hilo

Mawasiliano ni kiungo muhimu sana katika ulezi, uwe wa familia, koo au Taifa

Tangu aingie madarakani imetokea mara nyingi Mh anazungumza na kuacha tafsiri, maswali na utata miongoni mwa kauli zake, ikiwa ni pamoja na mshangao

Ni kwa mantiki hiyo, kauli zake zimetumiwa aidha vibaya, kupotoshwa au kumrudi

Mifano ipo mingi, yatosha kusema kwavile watu wana maumbile,vipaji na karama tofauti kuazima au kuiga haviwezi kuwa jibu.

Muhimu ni kuhakikisha kile alicho nacho mtu anakitumia vema

Tungemshauri Mh katika kuzungumza na hadhra asome hotuba aliyoandaa au andaliwa ili kuwasiliana na umma na kutoacha ukakasi

Tofauti ya viongozi wengi na mwl Nyerere ni kuwa,yeye alijaaliwa kipaji cha kuwasiliana na umma, na alitumia elimu yake kuhakikisha anawasiliana (effective communications)

Mkapa alitambua hawezi kuwa kama Mwl,alisoma hotuba zake zilizoandaliwa kitaalamu

Kuna tatizo gani Magufuli akifanya hivyo?

Je washauri na wasaidizi hawajaona tatizo?

Tusemezane
 
MBINU HIZI ZINAZUA MASWALI YASIYO YA LAZIMA
SERIKALI INAPOSAIDIA 'KUJENGA' UPINZANI DHIDI YAKE

Mwalimu Nyerere akihutubia mkutano wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Jangwani alisema ' Mwanasiasa anayependwa kubebwa amevunja sheria gani ya nchi''

Maneno yalikuwa rahisi lakini kadri muda unavyosonga, thamani yake inaongezeka

Kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kuliambatana na utungwaji wa sheria ya vyama vingi 'Political parties act' ya mwaka 1992 yenye marekebisho kadri muda unavyosonga mbele

Sheria iliambatana na uanzishwaji wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.
Ofisi hii pamoja na mambo mengine inaratibu shughuli za vyama vya siasa.

Kwa maneno mengine ndiyo mlezi wa vyama vya siasa

Sheria imeeleza masharti ya vyama kufanya mikutano na haki ya kupewa ulinzi.
Sheria inatoa fursa kwa Polisi kuzuia mikutano ikitokea ulazima wa kufanya hivyo.

Ukiisoma sheria hiyo, upande mmoja inatoa uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano na kwa upande mwingine ikitoa 'nguvu' zisizo na maelezo za uzuiwaji wa mikutano hiyo

Waziri mkuu wa awamu ya tano aliwahi toa maagizo kwa Polisi kuzuia mikutano ili kutoa fursa za watu kufanya kazi. Haukupita muda mikutano ikazuiliwa

Yamejirudia tena kwa mikutano kuzuiwa bila sababu zinazoeleweka.

Inasemwa, zipo dalili za uvunjifu wa Amani, kuchochea vurugu na kuleta kashfa.

Polisi wamezuia wakiwa ndani ya sheria, Je wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria?

Sababu za mikutano inachukua nafasi za kufanya kazi hazina mashiko.
Hakuna sheria ya nchi inayolazimisha mtu kuhudhuria mikutano kama haki ya kikatiba.

Na wala hakuna muda wa shughuli za kisiasa kufanyika katika mwaka , mwezi au wiki

Hoja ya taarifa za uvunjifu wa amani nayo inakutana na nguvu nyingine ya hoja.

Kwamba kama Polisi wana uwezo wa kubaini hali hiyo, iweje hawawezi kubaini matukio ya kihalifu yanayotikisa nchi ikiwemo mauaji yasiyo na maelezo?

Zaidi ni maswali ya wananchi, nini kinafichwa/ogopwa kisisemwe hadharani?

Endapo hoja ni kuzuia kashfa au uchonganishi kati ya serikali na wananchi, kwanini vyombo husika visisubiri kutumia kauli hizo mbele ya sheria kwa watuhumiwa?

Katika mwezi mmoja yamekuwepo matukio yasiyo na majibu ya kuridhisha.

Tatizo la sukari, mkataba wa Lugumi, wanafunzi-UDOM, bunge kuvurugika/kususiwa na wapinzani, instruments kwa mawaziri, malalamiko bunge kuingiliwa ,Bunge live n.k.

Kuzuia mikutano kunawapa wananchi wasi wasi. Nini kinafichwa au kisichotaka kusikika?

Wakidhani wana suluhu ya kukwepa tatizo, serikali inawajenga wapinzani kwa gharama bila kujijua.

Mfumo wa vyama vingi unaruhusu shughuli za kisiasa bila kizuizi zikifanywa kisheria

Tusemezane
 
DINI NA SIASA, HAPANA!
SIASA NA DINI, NDIYO!

Dhana ya kuchanganya dini na siasa ni ngumu kueleweka.

Historia inaonyesha dini zilikuwa na mifumo ya kiutawala tangu dahari, na kwamba siasa imeakiasi mifumo ya dini katika taratibu zake

Kuakisi (reflect) kunaonekana wakati dini zinapotumika katika siasa, kama nyimbo za Taifa, kuombea Taifa, Bunge na shughuli nyingine.

Katika mazingira ya kawaida kutenga dini na siasa au siasa na dini ni kutenga vitu vinavyofanya kazi pamoja.

Mfano kuwaombea mwanasiasa au Viongozi wa dini kuomba misaada ya kwa wanasiasa

Jitihada za kutenga haya zinaelezwa serikali haina dini, wananchi wanazo

Kwamba kuzungumzia siasa misikitini/Makanisani ni kuchanganya na siasa

Kinachoshangaza ni wanasiasa wanapozungumzia siasa makanisani au Misikitini, hatusikii wakisema ni vibaya kuchanganya siasa na dini.

Ni busara mambo haya yakawekwa wazi. Katiba ya nchi haizuii viongozi kuwa na dini au kutokuwa. Suala la dini ni haki ya mtu bila kuingilia utumishi wa Umma

Ni vema viongozi wa siasa wakiwaasa viongozi wa dini wasichanganye dini na siasa , nao pia wawe mfano wa kutochanganya siasa na dini.

Ni muhimu wakajiepusha na kuchanganya mambo ya utumishi wa umma nakuyafungamanisha na mambo ya kiroho.

Viongozi kama wanadamu wanahitaji malezi ya kiroho na ni haki yao.
Nao pia kama viongozi wanajukumu la kulea Taifa.

Kama walezi wa Taifa, kazi yao ni kuhakikisha ni kimbilio la wafungwa, mlevi, mwizi, waumini, wanafunzi, wafanyabiashara, wachanmungu na makahaba n.k.

Tunashauri maeneo ya dini yatumike kutafuta huduma za kiroho, yasigeuzwe viwanja vya siasa au maeneo ya kutoa kauli zinazohusu utumishi wa umma

Hiii kukaribisha viongozi wa dini katika siasa, watakemewaje wakichanganya dini na siasa? Na je, inaleta picha gani kwa jamii ?

Wale wanaoabudu chini ya mibuyu nafasi yao ipo wapi?

Ni wakati sasa wa kusema 'tusichanganye dini na siasa au siasa na dini''

Mambo ya dini yafanywe na kusimamiwa na watu wa dini

Wanasiasa wafanye na wasimamie ya siasa.

Kinyume cha hapo,tunantengeneza matatizo na mwisho wake tunasingizia kuna watu wanatuone kijicho, wapo wanaotumiwa.

Tusemezane
 
Back
Top Bottom