Sehemu ya II
Mkandara;10185722 Na wala isifahamike kwa watu kwamba hizo 8 zilitakiwa kuwa za Tangayika (bara) kama wanavyofikiria kina
Nguruvi3 kwa sababu tu ya mchango mdogo wa Zanzibar ktk mfuko wa taifa wakati wanashindwa kuelewa kwamba Wazanzibar mil 1.3 waishio zanzibar ni asilimia 2.9 ya watu mil.45 wa bara, hivyo Zanzibar ikichangia asilimia 3 tu ya mfuko wa Taifa wametuzidi bara (mathlan JMT imekusanya bil.10 - bil.7.7 ni a bara na Zanzibar .3) hapa huwezi kusema ati Zanzibar wananufaika.
Hawa wanaosema haya nao ni wapotoshaji wengine ambao somo la uchumi limewapiga magoli kama Brazil na Ujarumani.
Ndipo usipotuelewa, tunasema hivi hata kama ni 0.00001 lazima wachangie. Kwa sasa ni sifuri.
Pili, lazima uelewe nani ameanza kufungua Pandora box.
Hawa wazanzibar unaosema mchango wao wa 03% mkubwa, wanapata wapi uhalali wa kudai mambo kwa usawa?
Fikiria kuwa tume ya Warioba wazanzibar waligoma hadi wapewe 50%.
Matumizi ya tume ni takribani bilioni 60. Kama wznz wangelipa 3% unayosema kutokana na population yao, wangechangia 3% ya bilioni 60, hiyo ni sawa na 1.8 Bilioni.
Walichokisema ni kuwa pesa zinatoka JMT. Well,kama zinatoka JMT ambako kuna znz na Tanganyika, wale wajumbe 15 sawa wanalipiwaje na JMT huku Tanganyika ikiwa haina wajumbe?
Usichanganyikiwe hapa. Tunaposema Tanganyika haina wajumbe, ni kwasababu wabunge wa JMT wakiwemo wznz ndio waliokwenda BML kwa kofia ya JMT na si Tanganyika.
Hivyo SMZ ililazimika kulipia 50% ya wajumbe wake waliokwenda kwa masilahi ya Zanzibar na si JMT.
Je, hili nalo lilihitaji account? Kwamba bill ya bilioni 60 haijulikani hadi account. Ni afadhali sikusoma uchumi.
Madai ya znz kuhusu usawa ndiyo yanachagiza Watanganyika wajiulize, inakuwaje Wazanzibar ni wazuri sana wa kudai vyeo, fursa kwa usawa, tunapofikia kuwajibika wao hukimbilia udogo na uchache?
Arguably kuna suala la siasa na uchumi. Kwamba, nafasi kama za utawala ni za kisiasa.
Ni wapi tunaweza kutenga siasa na uchumi kama separate entity tukabaki kuwa salama?
Unatakiwa ujiulize, kwanini kumekuwa na kelele za wazanzibar kutochangia. Nini mkimebadilika siku hizi.
Ni lazima kuwe na balance, huwezi kulalamika eti upewe nafasi za utawala ikiwa huna wajibu wala wa kile unachoenda kusimamia.
Hebu niambie , kwa mwendo huu ambao znz wamegoma kuchangia muungano hata kwa 0.001, unawezaje kuwa na rais wa JMT kutoka znz akaheshimika
Pili, kama znz kwa 3% ina mchango mkubwa, je kwa fursa kama ajira nini mchango wao?
Na kama ni 3% yenye maana, ni hesabu gani zinawapa 21% ya ajira?
Mkandara;10185722 Kuhusu Gharama.
Watu wengi wanachukulia swala hili juu juu tu kwa kwa sababu imependekezwa serikali ya JMT kuwa na mambo ya muungano 7 tu. Hii haiwezekani mkuu wangu wa sababu serikali ya JMT hutegemea fungu kutoka serikali zake kwa ajili ya matumizi ya nchi husika. Sasa ikiwa wizara zote zilizowekwa ktk mambo 7 ya Muungano hazizalishi ila ni matumizi matupu unafikiri hiyo serikali kuu itapata wapi fedha za kujiendesha?
Na hapa ndipo hueleweki. Kwani sasa hivi inapata wapi?
Mkandara;10185722 Na kama serikali ya shirikisho haina mamlaka kabisa ktk mambo mengine hiyo serikali itaweza vipi kuweka dhamana juu ya maswala la maendeleo ya nchi hizo ikiwa nchi hizo hazitambuliwi kimataifa?
Si kweli, sasa hivi Tanzania inadhamini asilimia 88 ya madeni ya Zanzibar ambayo haitambuliki kimataifa.
Iweje kuwe na tatizo kukiwa na Tanganyika? Nadhani uanze kwanza kupinga udhamini wa Zanzibar kutoka JMT.
Kinyume chake, ni kiwewe tu cha uwepo wa Tanzania ndicho kinakusukuma kuandika majibu na si maswali
Mkandara;10185722 Nani atakaye ikopesha Tanganyika ama Zanzibar pasipo mhuri wa TAIFA maana msidhani kujiunga na UN ni kutambuliwa Uhuru wa nchi na mtawala bali hupata ridhaa ya mataifa hivyo unaweza kukopeshwa ktk miradi ya maendeleo na ukafuata masharti ya kimataifa. Tangayika na zanzbar ni sawa na mtoto wa chini ya Miaka 18 na mzazi ni JMT nani atakaye kubali kumkoposha mtoto ilihali mzazi hayupo labda awe molester!
Si kweli, na wewe kupitia uzi wako umethibitisha kuwa inawezekana.Katika uzi huo umesema ili kuondoa matatizo ya muungano, Zanzibar iruhusiwe kukopa nje(Ushahidi upo wa maneno yako)
Leo uwepo wa Tanganyika tayari unafuta hoja yako uliyosema ya Zanzibar ipewe fursa za kukopa.
Hapa kuna tatizo gani mkuu?
Kwanini uwepo wa Tanganyika uwe kikwazo lakini status quo unaipa upper hand tena ukisema Zanzibar iruhusiwe kukopa.
Kinachofanyika hapa ni Tanganyika ijivue koti(umesema sana) ili nayo iende kukopa kama Zanzibar ilivyopewa fursa hizo sasa hivi ikidhaminiwa na JMT bila kuwepo kikwazo cha UN.
Hakuna suala la UN wala nini, kama ulikubali kuwa znz ikope na ipewe fursa za kujiunga na mashirika, leo tunaposema Tanganyika ipewe fursa hiyo ili ijivue koti, tayari unageukia UN n.k. Mkuu double standards haifai.
Stick to the point, siyo kuyumba yumba . Nina evidence za maneno yako, kinachonishangaza ni kuabadilika kila siku.
Mkandara;10185722 Nani atakaye ipeleka Zanzibar au Tanganyika mahakama ya Dunia ikiwa nchi hizo zitagoma kulipa mikopo yake ambayo JMT imewawekea dhamana. Je, rais wa JMT akikataa kudhaminia kitu ambacho anakiona hakina umuhimu kwa taifa itakuwaje?
Na hata nchi husika wakiamua kuzitumia vibaya fedha hizo huyo rais atakuwa na mamlaka gani ya kusimamisha matumizi hayo maana hayamhusu!. haya ndio maswali tunayotakiwa kujiuliza kwanza kabla ya kuvamia kupendekeza mambo 7 ya Muungano.
Mkuu rudi kasome rasimu uielewe kwanza.
Pili, wewe umesema mara nyingi kwamba znz ipewe fursa zake pekee za kukopa. Fursa hizo imepewa.
Je, ikikataa kulipa nani atapelekwa mahakama ya Dunia? Kama itakayopelekwa mahakamani ni JMT iliyodhamini 88% ya madeni ya znz, kwanini uwepo wa Tanganyika ubadilishe equation nzima.
Ndicho kilichopo sasa hivi, tunachotaka kufanya ni kuongeza Tanganyika katika utaratibu unaotumika sasa hivi.
Rais wa JMT kwa mujibu wa rasimu hana kazi ya kuomba misaada na mikopo.
Rasimu imesema ‘endapo' kutakuwa na ulazima, JMT itawajibika kuwadhamini washirika.
Siyo suala la Rais kukubali tu, ni suala la vyombo vya rais kutathmini kuwa znz au Tanganyika zitakuwa na uwezo wa kulipa.
Ndiyo maana kuna bunge la JMT na vyombo vingine muhimu.
Kama nchi washirika zitatumia vibaya hiyo ni shauri yao. Hata sasa hivi zinatumia vibaya kama radar n.k.
Mbona huoni tatizo, bali S3 ndilo tatizo kubwa kwako? Kwa mfano, JMT imedhamini asilimia 88 ya deni la znz.
Nani anajua zinalipia nini.
Si kazi ya rais kujua SMZ imeafanyia nini, ni wajibu wake kujua kama znz inalipa deni husika. Period.
Na ndivyo itakavyokuwa kwa Tanganyika.Kwanini Tanganyika inakupa kiwewe mkuu.
Mkandara;10185722 Halafu, kumbuka lile swala la 10-2 ikabakia 8 ya JMT hili haitakuwepo tena kwa sababu JMT haitakuwa na 10 tena bali Tanganyika na 7.7 kwa sababu Zanzibar hawatachangiza .3 zao, hivyo wao watasubiri kipenga. Na wizara za visiwani/bara hazitapungua ila kutakuwa na ongezeko la matumizi kwa mabo yote isipokuwa hayo 7 ya muungano ni sawa na kusema kati ya 22 za mambo ya muungano toa 7 kuna mambo 14 yatakuwa mzigo mpya kwa bara na visiwani ambao ni maskini.
Mkuu usizunguke mbuyu. Kuna mambo 14 ambayo kila mshirika atabeba.
Kwa upande wa Tanganyika , kwasasa inayabeba yote 14. Hivyo hatutarajii kuna tofauti yoyote zaidi ya kupungua kwa mzigo.
Kwa upande wa znz itabidi wajifunze kuishi na mambo 14 waliokuwa hawana.
Hivyo hakuna suala la kugawana umasikini hapa. Lipo suala la kugawana majukumu na wajibu.
Tueleze kwa kupunguza mambo hadi 14, Tanganyika imepoteza nini kiasi cha kudhani tunagawana umasikini.
Znz haiwezi kujificha nyuma ya Tanganyika ikisema ''sisi''. Wakati wa kuwajibika inasema wao.
Hilo sasa linafikia mwisho.Hakuna kugawana umasiki mkuu. Kila mshirika atawajibika kwa watu wake.
Tena hapo juu umesema znz kwa idadi yake inachangia zaidi asilimia 3 kuliko Tanganyika.
Sisi tunasema hilo ni jambo jema, wapewe nafasi ya kutumia asilimia zao kwa maendeleo yao.
Na sisi Tanganyika hatuna kinyongo na wao kutumia kilicho chao.
Tunachukizwa wanapotumia chetu na kutulaumu kwa kuwasaidia. Hatupendi tunataka kuvua koti.
Kama wanataka tuwe wamoja, jibu ni S1.
Vinginevyo S2 ni njia ya kutaka wazanzibar waendele kunufaika katika mgongo wetu.
Sasa hivi hakuna kurudi nyuma, kila mtu aonje machungu ya muungano.
Hapo wznz wataheshimu muungano.
Kwasasa wanachukulia muungano ni haki yao, sisi tunasema ni haki yetu sote kuvuna na kuchomwa miiba.
Wazo lako la kuwa na JMT na SMZ linakataa kabisa logic zako.
Na wala Tanganyika haiwezi kuwa na nafuu kwa kuwa na znz. Ndio maana tunasema hakuna kugawana umasikini.
Mchango wao kwetu sisi ni negligible, tunagawana umasikini upi. Sisi ni masikini tu bila znz, na uwepo wao haupunguzi umasikini wetu zaidi ya kuongeza
Mkandara;10185722 Ni rahisi sana kusema kwani asilimia .3 kitu gani, ila nakuhakikishia hiyo asilimia inaweza kuvunja muungano kwa sababu haitaonekana faida ya kuwa na mambo 7 yanayo wagharimu pande zote pasipo kuwepo vyanzo vya mapato yake yenyewe. itakuja swala la mtu una deep ndani ya mfuko wako kugharamia mambo 7 wakati kuna mambo 14 muhimu kwa wananchi wako ambayo yanahitaji fedha! huu wenzdawazimu.!.
Mkandara, wewe umesema tumechukua mambo yote na kuyafanya muungano na hilo linawanyima wazanzibar fursa( bandiko lipo ukitaka kuliona).
Ukasema mambo yalikuwa 11 sasa ni 22 ambayo znz inaumia.
Ukatoa mifano mingi tu ikiwemo OIC bandari n.k. Leo tunapunguza kutoka 22 hadi 7 ikiwa ni pungufu ya yale 11 ya awali unageuza kibao.
Wazanzibar wanasema kwa ukubwa wan chi yao na watu wake hawahitaji mambo ya Tanganyika yawe ya muungano.
Wanalalamika kwanini kuwe na ujenzi wa reli ya muungano ikiwa kwao haihitajiki.
Solution ondoa hilo.