Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)


Nimekusoma kiongozi. Lakini Sijakuelewa bado:

1. Kwanini unakataa kwamba Zitto kapotosha Wasukuma na kuonea wachaga?

2. Ujamaa wa Zitto na ACT upo wapi? Anaishi maisha gani kama mfano wa ujamaa? Fedha za kuendesha ACT Zitto anatoa Wapi? Gharama zinaendana na what he declared as his wealth pale diamond?
 
Mkuu Mkandara , the more supreme's zelotes open up, they expose him in precarious situation.

Hayo maneno si ya supreme leader. Tangu mjadala uanze jukwaa la siasa ulikoshiriki vema hadi wakati huu, hujawahi kutumia maneno ‘stahiki'

Unachokifanya ni spinning inayoonyesha ulivyotekwa na fikra za ulaghai kama supreme, wanasema ‘disingenuous''

Umetaja K'njaro na Shinyanga ili kupunguza wigo wa eneo supreme aliloshambulia .

Tuweke rekodi sawa, supreme alishambulia K'njaro na Arusha kutokea
Shinyanga na Mwanza. No more no less


Tutayatumia maneno yako kukuonyesha twisting haimsaidii supreme

1 ''Shinyanga wanachangia sana hawapewi stahiki,Kilimanjarowanachangia kidogo wanapewa stahiki''
Tunarudia kusisitiza haya si maneno yake,lakin tuyajadili kama ulivyoyaumba

Historia : Tume ya Kamala ikikusanya maoni (EAC)kushirikisha Burundi na Rwanda, Zitto alisema bungeni ‘Msiogope EAC,MbonaKilimanjaro wameendelea kuliko Kigoma?

Ukisoma kauli yake(kwa mujibu wako) Supreme leader anasema K'njaro inapata stahiki, Shinyanga haipati stahiki(ukiondoa Arusha) ili kupunguza wigo wa ''shambulio'' la kisiasa alilofanya

Tunakuuliza, kwanini alisema K'njaro inapata stahiki yake?

Je,alikuwa na takwimu za kuthibitisha hilo? Kwanini alitumia K'njaro na si mikoa 6 iliyoko mbele ya K'njaro?

Ni stahiki gani inayopata ambayo Shinyangahaipati?

Je, hii si historia ya chuki dhidi ya K'njaro kama alivyoanza wakatiwa EAC?


Tungependa wewe na Zitto mtuonyeshe stahiki zipi na kiwango gani ambazo Shinyanga inanyimwa na Arusha/K'njaro zinapata.

Ndio maana tunasema, kadri mnavyoleta utetezi usio na mashiko, mnamweka mahali pabaya kisiasa.

Leo tunajua kumbe Zitto ana data zinazoonyesha K'njaro inapata stahiki dhidi ya Shinyanga, na wala si Sumbawanga, Tabora au Lindi


Mnajribu kutuonyesha ‘attack' ya Zitto-ACT dhidi ya mikoa ya kaskazini ni ya kukusudia kabisa.
 
Mkandara Supreme ana historia ya kushambulia mikoa yakaskazini.

Nimekuonyesha nia yake ya awali aliposema ‘K'njaro ina maendeleokuliko Kigoma''


Supreme leader hakutaja Arusha na K'njaro kwa bahati mbaya.Alitaja ili kuwagawa wananchi kwa misingi ya ukanda.

Alichokusudia kusema ni watu wa Mwanza na Shinyanga ni kuwa ‘wakataeni hao, sisi tunaelewa matatizo yenu''

Si kuelewa kwa sera, bali kwa kuzusha uongo wa kulimega taifa

Sasa hivi unachokifanya katika mjadala ni kutaka kubadili mwelekeo ili tujadili mambo mengine badala ya ACT na jitihada zake za kuvunjaupinzani na kuligawa taifa

Supreme leader, anawajibika kwa kauli zake zisizo na ushahidi.

Mkandara, umesema
Zitto alichukua takwimu na kwenda kuzisoma tu, hivyo asilaumiwe


Tunasema hivi, kusoma ni jambo moja, kuelewa jambo jingine,na kutumia takwimu ili kuleta vurugu, uchochezi na sintofahamu ni jambo lingine

Zitto asimame na kuthibitisha kuwa mgawanyo anaotaka kuueleta katika taifa hili una uhalali wa takwimu

Hatutakaa kimya ukitushawishi,alikwenda kusoma takwimu zenye hisia kama kasuku.

Supreme ana hiari ya kuandika na kusoma mashairi kadri anavyoweza, ili mradi tu, mashairi hayalengi kutuletea vurugu


Supreme leader anatoka Kigoma na anafahamu matatizo ya kumega mataifa.

Hatutakaa kimya akiendeleza siasa za kuwagawa wananchi kwa mtindo wa kushambulia mikoa isiyo na hatia
 
.............?
 
Mkuu mbona unapenda kutumia haya maneno kuwa usitafute pa kupenyea, hapa sisi wengine tupo kwa ajili ya kusoma na kujifunza na kuna watu wengi tu wanafuatilia huu mnakasha.

Wewe ni mchumi mzuri lakini mbona unafanya makusudi kupotosha mkuu bahati mbaya au nzuri kuna raia umewanasa umekuja na zile takwimu za TRA na kutuaminisha ndiyo pato la taifa daaa!!!.

Hivi mkuu sisi ambao siyo wachumi na wavivu wa kusoma sindiyo basi tena huku mitaani kwetu tunatumia data za Tax revenue ndiyo pato la taifa na tunaona Kilimanjaro wanalipa kingi kuliko Shinyanga.

Naona kwenye huu mtego mpaka ndugu zangu kina Nguruvi3 na JokaKuu wamenasa nao wanatumia data za TRA kama reference kwenye pato la taifa.

Bado unazidi kupotosha kwenye GNP na GDP.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Ritz mjadala huu unakupwaya sana, nakushauri uwe msomaji tu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz mjadala huu unakupwaya sana, nakushauri uwe msomaji tu
Najua wewe lazima utasema hivyo sababu nawahoji mabwana zako wewe si unameza tu.

Nakushauri acha na mimi ili tusiingie huko unapotaka jifunze kusoma vitu usivyovipenda.

Ahsante.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz mjadala huu unakupwaya sana, nakushauri uwe msomaji tu

Ni kweli uko sahihi si kila kitu mtu unakijuwa tatizo la huyu jamaa anadhani kila mjadala unabase kwenye kuunga mkono dini yetu Ile. Mkandara ana ID yake hapa JF ya kuchochea udini na ushahidi ninao na niko Tayari kuthibitisha anytime.
 
Last edited by a moderator:

Naona Mjadala umekuwa mrefu hata hatufahamu ni kitu gani tunachobishania.. Hakuna pahala popote Zitto aliposema kuwa "Shinyanga wanachangia pato kubwa lakini wanapata stahiki ndogo. Kama kuna sehemu aliposema hivyo basi basi naomba unionyesha maana inawezekana hapa mambo ya GPD yanichanganya..

Ila alichosema na kitu ambacho kimefanya huu mjadala kuwa mrefu ni kuwa "Shiyanga wanachangia zaidi kuliko Arusha na Kilimanjaro lakini Kilimanjaro na Arusha pamoja na kuchangia kidogo wameendelea zaidi ya Shinynaga.

Na ndo maana wewe mwenywe huko nyuma ulisisitiza kuangalia Tax revenues ili kujua ni mkoa hupi wananchi wake "ni nguvu kazi" kuliko mkoa mwingine.. (kama nilikuelewa vizuri) na baada ya Mchambuzi kuleta takwimu za (#427) "Tax revenues" na kuonyesha Kilimanjaro/Arusha unalipa zaidi ya mara 6 (kitu km hicho) kuliko Shinyanga, na ndo hapo wewe mwenyewe ulisema "Nakubaliana na Mchambuzi sasa itabidi Zitto aelezee ni kitu gani alimaanisha) na ndicho chanzo ya post yako #439 na nyingine.


Kwa hiyo nasisitiza hoja si nani anapata zaidi ya nani hoja ni kwanini Kilimanjaro na Arusha wanamaendeleo zaidi ya Shinyanga pamoja na Shinyanga kuchangia kiasi kikubwa katika pato la taifa.

Na swali langu kwako ni kuchangia kiasi kikubwa katika pato la taifa kunachangiaje maendeleo ya sehemu husika?
au kuchangia pato kubwa katika pato la taifa kunahusiana na nini kumpeleka mtoto wako shule, au mkeo kujifungulia hospitalini ? maana hivi ni vigezo muhimu vinavyoangaliwa katika maendeleo ya eneo husika..
 
Mkuu Nguruvi3 ACT bado ni mpini wa CCM kumaliza wapinzani? Maana naona zile mbwembwe za mpini zimepungua ghafla au ndo unajipanga kuja na kasi,ari na nguvu mpya??

Ila swali letu bado liko pale pale pesa ya kuendesha mkutano mkuu wa chama, pesa za kuzunguka mikoa 11 zilitoka wapi?

Pamoja na zunguka mikoa 11 waliweza kupata wanachama 7000tu.. Kwangu mimi hii ni idadi ndogo sana ukiangalia umaarufu wa Zitto, nguvu zlizotumika kutangaza chama chake, watu walivyokuwa wanajaa katika mikoni yake nilitegemea idadi kubwa zaidi ya hii.

Hii si dalili nzuri kwa kijana mdogo kama Zitto kupata mwitikio mdogo kiasi hiki. Sijui ngoja tuone katika uchaguzi mkuu ni vipi ACT itapanda chati.
 

Kwa jinsi unavyochomekea, inawezekana longolongo nzima ya mdahalo huu katika siku za karibuni sio matamshi ya Zitto huko Shinyanga. Bali preemptive efforts by the opposition to suppress ACT and Zitto. Had Rev. Mtikila said the same words, he would have gotten away with that.

Anyway, getting 7000 new members in a very short period of time isn't a small feat. How long it took CDM or CUF to reach that number? Probably more than a year. Launching and building a new party isn't that easier.
 
Alaa kumbe...!
I call for timeout...! Baada ya hapo naomba turudi kwenye mada...

Huu mjadala umefika kurasa wa 44 na nina wasi wasi utaendelea na hata kuvuka hapa ulipo lakini naomba nitoe tahadhari moja; ukitaka kuwa muongo, ujue na kutunza kumbu kumbu. Nimeshuhudia Mkuu Mkandara, si mara moja bali kila anapobanwa, hutafuta upenyo wa kutokea na mara nyingi huo ujanja wake hujikita katika kutoa watu walipofikia na kuwarudisha nyuma, mbinu inayoitwa kuhamisha magoli.

Bahati mbaya kwake ni mwepesi kusahau juzi alitetea nini, jana katetea nini na leo anatetea nini. Sasa hapa kuna mawili, ama anafanya hivyo makusudi au kwa kutojua lakini the bottomline ni kwamba anatupotezea muda na kwa kuwa hii ni JF nimeamua kumpa kavu kavu. Anaweza akauliza swali halafu akipewa jibu ataingia tena na ajenda mpya kama vile si yule yule Mkandara wa jana aliyekakamaa akidai majibu.

Mkandara anazo kila dalili za kilaghai kama huyo Supreme Leader anayemtetea na sitashangaa kama talking points zake zina source kutoka huko huko. Huu ukinyonga ni tabia iliyokomaa hapa JF ikiendekezwa hasa na watu wanafiki na wasiojiamini, huku wakijificha nyuma ya IDs zaidi ya moja. Jina la Chama cha ACT Tanzania mara Wazalendo ni kielelezo tosha kwamba kimejengwa/kuasisiwa katika misingi ya kilaghai.

Mkandara kama alivyo Supreme Leader anayo tabia ya kuuma na kupuliza, yuko kote kote kulingana na upepo unavyovuma. Tuko sisi wengine tulimpa tahadhari Supreme Leader toka siku nyingi tu zilizopita, tukiwa bado tuko naye bega kwa bega katika kuchochea mabadiliko. Wengine tulipoona hashauriki, tulimwambia ukweli hatukumficha na tulimhakikishia kwamba akiendeleza hizo tabia, hatutaendelea kuwa naye pamoja.

Nakumbuka kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2010 alipoanza kuona kwamba ana mtaji tosha na hawahitaji tena watu wa kumkosoa wala kumpa ushauri. Kuna wakati alidai angeweza kugombea Ubunge popote pale akashinda tangu Kigoma hadi Dar es Salaam au kwa maana nyingine hakukihitaji tena chama chake kufikia malengo yake. Hata sasa kwa dalili zote ni kwamba haihitaji hata hiyo ACT na hivyo kawa tayari kuigawa vipande viwili.

Swali hapa ni kwa nini aliamua kuigawa ACT vipande viwili ACT-Tanzania na ACT Wazalendo. Yawezekana alikuwa na hofu kwamba si waasisi wote wangeafiki kuunga mkono hujuma dhidi ya Upinzani kama ilivyoelekezwa na chama tawala, CCM. ACT-Wazalendo inatakiwa iwe na watu wasioweza kuhoji mamlaka aliyo nayo Supreme Leader na hata wanaochaguliwa kama viongozi katika ngazi mbali mbali, utii wao wa kwanza ni kwake.

Supreme Leader ndiye nuru, dira na taa...bila yeye hakuna kinachoendelea kama ilivyokuja kuthibitika siku ya uzinduzi. Swali ni je kuna kitu gani nyuma ya hizi nguvu za kimungu? Tumeshuhudia jinsi uchaguzi ndani ya ACT ulivyoshindwa kufanyika bila yeye, mikutano ya kuitangaza ACT isivyoweza kufanyika bila yeye na kulingana na Katiba yao inavyosema tamko lolote analolitoa hata kama lina madhara kwa chama hakuna wa kuhoji.
 

Mchambuzi:

You don't get it. Do you? Political narrative isn't story telling, but rather the framing of the message so it could resonate with the audience. In Shinyanga Zitto did just that. He framed the message. Whether you like the message or not, that's another story.

Politicians aren't college professors like you. They don't go out to teach economics 101, GDP or tax revenues. That isn't their job description. They go out to politicking. Take for example Nyerere. In order to get our independence, he blamed colonial masters for everything. If he had told us that wakoloni came to our country kuchakarika, who would have listened to him?
 


Alinda:

Ulishasema katika posti zilizopita kuwa unachukia Mkenya akiwa na nafasi ya kazi wakati mtanzania yupo mwenye ujuzi. Huo ni ubaguzi wa kitaifa. Kama wewe unaweza kufanya hivyo kwanini mluguru naye asichukie mpare anapokuwa mkuu wa wilaya ya morogoro? Anachofanya mluguru ni sawa na unachofanya wewe. Kama mpare analeta chachu za maendeleo Morogoro, kwani Mkenya asilete chachu za maendeleo Tanzania?

Katika miaka 50 ya uhuru wa nchi za kiafrika hakuna kabila moja la kiAfrika lilolosaidia kabila jingine kupata maendeleo. Kama lipo naomba unipe mifano. Na hakuna taifa moja la kiAfrika lililosaidia taifa jingine kupata maendeleo. Hata mataifa ambayo Tanzania imesaidia kupata uhuru, hayana mpango na Tanzania.

In our societies, you only grow bigger by making others smaller.
 
Mchambuzi:

Take for example Nyerere. In order to get our independence, he blamed colonial masters for everything. If he had told us that wakoloni came to our country kuchakarika, who would have listened to him?

Zitto blames Wachaga for wasukuma's impoverishment. Anabagua na kuchonganisha makabila. Nyerere didn't do that, instead he strived to Unite all ethnic groups against one dominant force that was exploiting and dehumanizing Africans.
 
Alinda, hawa ACT na supreme wataendelea kuwa mpini wa CCM.

Unaweza ona jinsi walivyoamsha hisia za umma kwa mtazamo hasi.

Tayari wanaunda kanda ili kuwagawa wananchi. Wanajenga fikra za vyama vya siasa kikanda.
Ni kwa kilekile walichokikataa kabla hawajamtimua Limbu na kupora chama.


Ni tatizo kwasababu, mwenyekiti wao anapiga marufuku wanachama kutamka UKAWA. Kazi ambayo hata CCM hawajaifanya. Katibu mkuu anapanga kuwaondoa CUF pwani, na supreme leader kuwatimua NCCR kigoma na sumu hasi kanda ya Ziwa. Hizi ni kazi za CCM ambazo ACT imepewa kama secondment

Kuhusu pesa za kuendesha mikutano, hili nalo linazua hojanyingine.
Supreme leader alitumia PAC ili wakague CDM kwavile matumizi hayakuwa wazi.

Pamoja na kuwa kiongozi, supreme aliingiza fitna akiandaliwa waraka.

Leo yule yule aliyetaka uwazi wa fedha hawezi kusema amepata kutokawapi. Hizi ndizo fitna na uongo tunaoukemea


Kuhusu wanachama, kwa Tanzania idadi si jambo la kutilia maanani sana.
Kesho Nape akizunguka anaweza kupata idadi hiyo hiyo ya kadi zilizorudishwa.

Na ni bahati mabya supreme alikoondoka hajaacha alama, ameacha majeraha ya ubaguzi yatakayomwandama kila uchao.


Kujaa mikutano, ni hulka ya wananchi kutaka kujua amekuja nakipi kipya.

Katika mwendo wa kuligawa taifa, nadhani wengi wanajiuliza hiki ndicho kipya?
 
..Zitto alipaswa kuwaeleza wana-Shinyanga ni jinsi gani ACT itaboresha sekta ya pamba.

..alitakiwa awaeleze ni jinsi gani ACT itawawezesha wachimbaji wadogo-wadogo wa madini tofauti na CCM inavyowakandamiza.

..angewaeleza ni jinsi gani ataboresha sekta ya ufugaji, ili wafugaji waweze kufaidika zaidi na mifugo yao.

..badala ya kufanya hayo Zitto anajielekeza kwenye siasa za chuki, fitina, na uchonganishi.
 

Kwanza naomba kurekebisha hapo kwenye nyekundu hakuna sehemu yeyote ile ambapo nilishasema juu ya kuwachukia Wakenya.. Si kawaida yangu kumchukia binadamu mwenzangu. Kama hipo naomba nionyeshe nanipo tayari kuomba msamaha.

Pili nafikiri hunitendei haki pale ninapokuuliza maswali na wewe badala ya kujibu basi huja na maswali mingine zaidi. Tafadhali rejea post no.870 na nakuomba kwa unyenyekevu unijibu maswali yangu. Kwani kwa kufanya hivyo nitajifunza kitu fulani kutoka kwako na pia nitakuwa nimepanua uelewa wangu katika maswala mbali mbali.
 
Wanaukumbi.

Tumsome kiduchu Zitto.

Kwa sasa ACT-Wazalendo ni Zitto Kabwe, bila Zitto Kabwe hata uhai wa ACT-Wazalendo haupo!.Ziara ya Viongozi wakuu wa ACT-Wazalendo katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mara na Mwanza imeangaza picha na kutoa majibu mengi.Ni ukweli kuwa, kuingia kwa ACT-Wazalendo kwenye uwanja wa siasa nchini umewatikisa UKAWA na unaifanya CCM kujitathmini na kuwa waangalifu katika mchakato wa kuwapata wagombea wake.Kabla ya ACT-Wazalendo, nguvu ya kisiasa ilikuwa mikononi mwa CCM na UKAWA.ACT-Wazalendo unaifanya UKAWA kukosa kwa kiwango kikubwa umuhimu wa Muungano wao kama nia yao ni kutaka kuunganisha idadi ya kura ili kuishinda CCM na siyo kuunganisha philosophy, policies and manifesto.ACT-Wazalendo unaifanya CCM kuachana na politics as usual katika mchakato wa kupata wagombea kwa sababu ACT-Wazalendo ni zaidi ya Independent candidate katika nguvu za CCM. CCM wangeweza kuendelea kufanya politics as usual kama nguvu ya kisiasa ingebakia ni UKAWA pekee kwa sababu wale wangefanyiwa vitimbwi ndani ya CCM wasingepata nafasi tena ya kukimbilia UKAWA na kupata nafasi ya kuwa wagombea kwa sababu muungano wa UKAWA umeishafukia nafasi tatu kati ya nne za wagombea kutoka vyama vinavyounda muungano wa UKAWA kuanzia udiwani, Ubunge mpaka Urais.ACT-Wazalendo imeingia kwenye uwanja wa siasa na clear-cut central idea and programme soundly ikisaidiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vingi vya mawasiliano nchini kwa sababu imebeba majibu ya mapungufu ya UKAWA na CCM katika siasa za Tanzania lakini kikubwa zaidi, inafanya siasa zake nje ya confrontational environment ukilinganisha na vyama vikubwa hasa ikichukuliwa kuwa, Watanzania wengi hawapendi siasa za vurugu.Wananchi wengi watakaojiunga na ACT-Wazalendo kutoka CCM watakuwa ni wale wanaamini CCM imeacha misingi ya uanzishwaji wake na vile vile rushwa imekuwa ni kigezo cha kupata uongozi ndani ya chama na serikali yake.Wananchi wengi watakaojiunga na ACT-Wazalendo kutoka UKAWA watakuwa ni wale wanaamini Muungano wa CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD umewanyima demokrasia ya kuchaguliwa ndani ya vyama vyao baada ya kuwekesha nguvu na pesa katika vyama hivyo na pia kuna wengine watafanya hivyo kwa sababu wanaamini ni wahanga wa uongozi wenye hekima na busara za makengeza.Ninaamini huu ni ukweli unaonekana na wachache kwa kutumia naked eye na katika ukweli huu, ndiyo nguvu ya ACT-Wazalendo kupitia kwa Zitto Kabwe inakuwa ni power broker.Ni wajinga na wapumbavu watakaopuuza na kubeza uwepo wa ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Kabwe katika mstakabali wa chaguzi za Tanzania Bara katika mazingira ya siasa za ndani ya UKAWA na CCM.Kuna baadhi ya wananchi wameanza kuja na hoja nyepesi za kisiasa kuhusiana na ujio wa ACT-Wazalendo wakiamini ni hoja mbadala au ni hoja zinazotuliza ombwe lao la fikra pevu.Kuna baadhi ya wananchi wameanza kudai eti haka ni kachama kadogo. Fine!.Hoja ya msingi hapa, Ziara walizofanya katika mikoa kumi imetoa majibu ya maana ya ''haka kachama kadogo''.Kuna baadhi wanadai ACT-Wazalendo ni chama cha wasaliti. Fine!.Hoja ya msingi hapa, wasaliti wa nani katika taifa Iinalokadiriwa na National Bureau of Statistics (NBS) office kuwa ifikapo siku ya uchaguzi, Tanzania itakuwa na watu wapatao 48,522,228, ambapo watakaokuwa na umri wa kupiga kura mwaka huu watakuwa ni watu 24,253,541.Kuna wengine wanadai, ACT-Wazalendo ni tawi la CCM. Fine!.Hoja ya msingi hapa, vyama vingine ni matawi ya nani kwa faida ya nani?Kuna wengine pia wanakuja na hoja wakisema, ACT-Wazalendo imekuja kugawa kura za UKAWA. Fine!.Hoja ya msingi hapa, kura hazigawanywi kama njugu. Kinachogawa kura ni philosophy, policies and manifesto, labda kama misingi hii ya ACT-Wazalendo inafanana na UKAWA lakini kikubwa zaidi, Tanzania hivi sasa ina zaidi ya vyama 22 vyenye usajili wa kudumu chini ya Rais aliyechaguliwa na wananchi 5,276,827 kati ya wananchi 20,137,303 waliojiandikisha kupiga kura.Wahenga walisema, ‘Mchelea mwana kulia hulia yeye’ na ‘Mdharau mwiba mguu huota tende’ lakini kwa wale wanafahamu maana yake, this is an opportunity to step back, reflect and refocus.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…