Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Naona umekuja na lawama na malalamiko mengi mwisho umeweka kipande cha hotuba ya Zitto aliyoitoa Tabora kupitia YouTube Channel ten.Kwanza nawashukuru wote mpaka hapa ambao mnachangia katika uzi huu, na wale wote ambao wanaudhuria hapa kama wasomaji wakiwa na nia ya kutaka kujua ukweli juu ya "Chama cha ACT-kuwa Mpini wa CCM kuumaliza upinzani".
Lakini nina sikitika na kuwalaumu kwa baadhi ya wachangiaji wa uzi ama kwa makusudi kuja na mabandiko ya kuhamisha mawazo ya wachangiaji na wasomaji wa uzi huu juu ya hoja iliyoko mezani. Wanajijua.
Kuna suala la Supreme Leader(SL) kutoa kauli ya kuwagawa watanzania. Mkandara, Mchambuzi, Nguruvi3 na wengine wamelijadili kwa kina. Ritz na Adharusi wamejitahidi pia kumtetea SL kuwa kauli yake haina madhara kwa kutumia namna mbalimbali za kiuandishi huku wakileta rejea zinazopishana kiasi cha kutilia shaka utetezi wao kwa SL.
Pengine tungerejea kwenye orignal source ya kauli ya SL. Yaani tupate ama audio ama video ya hotuba zote za SL pamoja na za wasaidizi wake walipokuwa ziarani na chama chao cha ACT na kuziweka hapa kwa mjadala mpana na rahisi (maana referencez itakuwa karibu) wa ACT kuwa mpini wa CCM na pia mpini wa kuligawa taifa katika misingi ya kibaguzi. Aliwahi kufanya hivyo Nguruvi3 kwenye mjadala wa Wazanzibar na haki ya kuwa taifa huru ! .
Kwa kuwa tumebahatika kumpata mtafutaji wa hotuba za Zitto (Ritz) atusaidie katika hili kwa kutuwekea hotuba hizo kwa kirefu.
Katika kuchakura chakura kutafuta hotuba za SL. Nimepata kipande hiki cha hotuba ya SL
Hata wewe jukumu lako pia kuleta hotuba za Zitto hapa ukumbini au mwanaukumbi yoyote anayo nafasi ya kufanya hivyo siyo mimi tu.
Sijui kwa nini umeamua kumtaja Ritz peke yake au ndiyo wale wale wanaumia na ninachokiandika.
Unasema utetezi wangu unatia shaka halafu hapo hapo unasema nikuletee hotuba za Zitto aalaah!!
Kwa faida ya Wanaukumbi vunja hoja yangu ya utetezi wenye shaka kwa kuweka hizo hotuba ambazo hazina shaka ndani yake ili kukata mzizi wa fitna.
Last edited by a moderator: