Naona wanajamvi unachezeshwa mduara.. Alicholete
Adharusi ndicho Zitto aliandika katika wall yake ya Facebook tarehe 5.4. Baada ya kuandika hivyo kulizuka mjadala mkali si Facebook tu bali hata hapa JF.
Baada ya mjadala mkali tena bila Zitto yeye mwenye kujitokeza kutetea alichoandika, halifanya marekebisho ya kile alichokuwa ameandika awali na kuja na alichoandika Ritz, au kile kinachooneka katika fb yake kwa sasa. Na ndo chanzo cha hotuba tarehe 19.4
Hivyo basi kilichokuwa kinajadiliwa
SI HOTUBA YA ZITTO YA TAREHE 19 MWANZA bali ni maandishi yake ya tarehe 5.4 katika Facebook yake ambao ndio yalileta mjadala humu tarehe 5.4. katika jukwaa la siasa. (Maana kwa akili za kawaida haiwezekani kitu kisemwe tarehe 19.4 na mjadala uanze tarehe 5.4)Ila kwa bahati mbaya au kwa makusudi ya moderator maandishi hayo yamebadilishwa na kusomeka kivingine si kama pale hawali. Adharusi kaleta kitu sahihi na kama kilivyoandikwa na Zitto tarehe 5.4 na Ritz kaleta hotuba ya tarehe 19.4 baada ya kuwa ameishabadilika maudhui.
Sasa je hii inatwambia nini?
Hii inatwambia kuwa haikuwa bahati mbaya Zitto kuja na uchonganishi wake kama alivyosema hapo awali
nguvuri3 maana kama angekuwa ameandika kwa bahati mbaya au kwa kutokuwa na uelewa basi tungemuona Facebook akitetea kwa hoja ni kwanini alinganishe Shinyanga na KIL/Arusha au kwanini atumie kigezo cha uchangiaji wa pato la taifa na maendeleo ya mkoa husika.
Lakini kiyume chake hakujadili chochote, hakutetea msimamo wa yeye kunyofoa hiyo mikoa, kibaya zaidi hakuomba hata SAMAHANI KWA WATU ALIOWAKWAZA KWA ANDISHI LAKE. bali alichokifanya ni kufanya marekebisho ya andishi lake kimya kimya na kuwaacha wafuasi wake solemba. Na kudhihirisha ili ukienda katika fb yake watu wametoa michango ambayo haina husiano na "andishi lilopo"
Ninampa onyo: Baba yetu wa taifa na viongozi wengine walifanya kazi kubwa sana ya kuunganisha ili taifa, lenye zaidi ya makabila 120 lakni bado sisi ni wamoja, tuna upendo, kila mtanzania ana thamani sawa na wingine. Leo hii yeye anaweza kutamba mbele ya wezanke kwa utanzania wake, tunaishi kwa amani, hatuna wasi wasi wa kuibuka kwa vita vya ukabila, tunapanga mipango yetu ya baadaye bila kuwaze kesho tutakimbilia wapi na nk. hii yote msingi wake mkuu ni umoja tulio nao. Hivyo basi hatutaraji mwanasiasa yeyote, kwa sababu yeyote kuleta siasa zake za ubaguzi. Kama anataka kujaribu siasa za ubaguzi avuke mpaka aende Burundi/Rwanda akafanye hizo siasa zake ya ubanguzi huko lakini kamwe Tanzania hazina nafasi.
Leo unamsimanga mchaga wakati kunakula, unavaa, unatibiwa tena India, unaendesha ya kifahari, unalipia mtoto wako shule, unatunza famili yako,kwa kodi za huyu huyu unayemsimanga.Swali kwako
Zitto ni faida gani upatayo?
Hizi siasa zako za kitoto tafadhali ziache hazitakusaidia wewe, hazitamsaidia mwanao, na hata hazitawasaidia wajukuu zako. Sisi watanzania tumelelewa kwa kuheshimiana, kusaidiana,hatubaguani kwa makabila yetu au kwa dini zetu, wala rangi yake, leo hii watu wenye asili ya mataifa mbali mbali wanaishi Tanzania kwa amani bila kubaguliwa au kutengwe, (tena wewe ni shaidi mzuri kwa hili).
Ni nini kosa la wana Kilimanjaro na Arusha hadi upande hizi fitina zisiso na maana yeyote? Je ni ungomvi wako na Lema? je ni ugomvi wako na Mbowe? je ni ugomvi wako na mchaga yeyote?
Kumbuka kukosana na binadamu mwenzako si jabu la ajabu lakini husitumie chuki zako katika kuleta mtikisiko katika taifa hili.Tuache tufe wa magonjwa, tufe wa uzee, tufe kwa ajali lakini tusife kwa kuuana sisi wenyewe kwa wenyewe.