Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Nguruvi3,

Naona umepanic ghafla nakukumbusha tu weka maneno ya akiba maandiko yako dhidi ya Zitto siyo msahafu.

Ni ushauri mzuri sana maana kama ilivyo leo kwa Lowassa yawezekana kesho na keshokutwa ikawa kwa Zitto, akiba ya maneno kwenye siasa hizi za kitanzania zisizosimama kwenye misingi ni muhimu sana.

Umegusia mambo muhimu sana, kama kuna watu wanadhani wataweza kumcontrol Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(kwa katiba iliyopo) tena Rais mwenyewe ni Edward Ngoyai Lowassa basi watakuwa wanajidanganya sana,kinyume chake wabunge wengi wa Chadema watajenga ufuasi kwa Lowassa binafsi(Lowassa ana historia nzuri sana kwenye hili, iwe kwa vyeo au kwa favour zingine) na pia ataweza kushirikiana na wabunge wa vyama vyote ikiwepo CCM(anajua vizuri kuishi nao), hatimaye mwishowe badala ya Chadema kumsimamia ni Lowassa ndiye atakayeisimamia Chadema na kuipeleka atakavyo, tuna mifano mingi Afrika juu ya siasa za chama na urais, na wakati wote Urais uwa unashinda, Bingu wa Mutharika na Joyce Banda wa Malawi ni mifano mzuri.

Otherwise nampongeza sana Dr Slaa kwa kukubalia kuachia nafasi ya urais bila shida, sio watu wengi wanaweza kufanya hili kwenye siasa za Afrika, japo legacy yake juu ya ufisadi itaathiriwa sasa kwa kuanza kumpigia kampeni aliyemuita fisadi awe Rais lakini kwenye suala la kutokuwa na "uchu wa madaraka" atajijengea heshima kubwa.Hili litakumbukwa ata miaka mingi ijayo na kwa kweli anastahili pongezi.
 

Nakubaliana na wewe mkuu.

Kuna vijana wanasema Slaa hawezi kushinda uchaguzi. Inasikitisha sana kusikia vijana wa Chadema wakitoa kauli za namna hiyo. Yaani Slaa akatwe kwa ajili ya Lowassa!

Lowassa alipokuwa anagombea ndani ya CCM, tulishuhudia vijana wa CCM wakitoa pressure kwa uongozi wa chama chao usimpitishe kutokana na historia yake ya kukosa uadilifu. Vijana wa Chadema wenye ujasiri wa kusimama na kuuambia uongozi wao ukweli wako wapi? Je, ni kweli vijana wote wanakubali kuwa Dr. Slaa hafai kuongoza nchi? Kama wanaamini anafaa, kwanini hawasimami kutoa sauti yao juu ya hilo?

Kwahiyo hapa tunaona kwamba iwapo mission ya Lowassa itafanikiwa, nchi itakuwa inamilikiwa na kikundi kidogo cha watu. Wanaopinga wote watanyamazishwa.

Kila jamii itavuna inachopanda...
 



Maajabu unapomshauri mwingine kuweka akiba ya maneno lakini haipiti hata robo dk wewe unafanya kile kile ambacho umemshauri mwingine.. Hapo ndipo uwa anashindwa kuwaelewa binadamu.
 
[/COLOR]

Maajabu unapomshauri mwingine kuweka akiba ya maneno lakini haipiti hata robo dk wewe unafanya kile kile ambacho umemshauri mwingine.. Hapo ndipo uwa anashindwa kuwaelewa binadamu.

Alinda wapi sijaweka akiba?kumpongeza Dr Slaa?


Ukiona Tindu Lissu, ambaye ndiye aliyekuwa kinara wa kupinga Lowassa kuachiwa nafasi ya kugombea urais Chadema, ukiona anasema hayo ujue hiyo ni done deal.
 

Haya mapenzi yako na Dr. Slaa yametoka wapi?

Kuhusu Dr. Slaa kukatwa ni nani atamkata? maana ninachoelewa mpaka dk hii hakuna aliyerudisha form ya kugombea urais kupitia Chadema. Sasa hili swala la Dr. Slaa kukatwa sijui umelitoa wapi?

Hivi si ni wewe uliyekuwa unamvua nguo huyu Mzee kila siku? wewe si ndo ulikuwa unasema Padre hawezi kuwa rais? au umesahau kuwa huyu Dr.Slaa unayemsema ni yule yule Slaa uliyekuwa unamvua nguo kila siku humu ndani..
 


Hapo kwenye nyekundu hizo ni hisia tu.. Wewe umekuwa mstari wa mbele kutushauri kuachana na hisia hisia lakini haipiti hata dk unakuja na hisia.. Jamani vijana ishini kutokana na yale msemayo..
 


Hapo kwenye nyekundu hizo ni hisia tu.. Wewe umekuwa mstari wa mbele kutushauri kuachana na hisia hisia lakini haipiti hata dk unakuja na hisia.. Jamani vijana ishini kutokana na yale msemayo..

Upo sahihi kabisa, lakini ukinisoma vizuri nimejadili kwa muktadha wa katiba(Rais wa Tanzania ni kila kitu) na kwa muktadha wa historia, kumbuka tuna mifano mingi ya siasa za Afrika kwenye case kama hii na ipo wazi.
Na hapa tunamuongelea Edward Lowassa ambaye sio mgeni kwenye siasa na kama akishinda basi sehemu kubwa ya wabunge wa CCM watakuwa comfortable kufanya nae kazi.
 
Tangu Lini Lissu akachagua mgombe urais kupitia Ukawa?

Mpaka hapo umeishaelewa kwanini nimekwambia kabla ya kumwambia mtu aweke akiba ya maneno inakubidi uanze wewe ili kuonyesha mfano.

Ok haidhuru, wacha tusubiri liwekwe wazi zaidi ili hizo shaka zisiwepo.
 


Uliongea yanaweza kuwa kweli au si kweli.. lengo langu nilitaka kukuonyesha huwezi kuongea siasa bila kuwa na hisia.. hisia za kitu fulani ndizo zinazokutuma kujenga hoja ya kitu chochote hivyo basi hisia ni muhimu.. Unaponiongela mimi hiyo tayari ni hisia zako juu yangu au unapojenga hoja ambayo inaweza kuwa ni kweli au si kweli tayari ni hisia. Hivyo basi natumaini utaondokana na neno "mnajadili kwa hisia hisia tu" Kwa sababu nikwambia jadili kitu chochote bila hisia si dhani kama utaweza.
 

Mkuu Mag3

Kwa kuwa mpaka sasa hakuna tangazo lolote rasmi juu ya Lowasa kujiunga rasmi na CHADEMA na kuchukua fomu ya kugombea urais sitachangia hili kwa sasa mpaka hapo itakapokuwa rasmi.

Nitarudi...
 
Last edited by a moderator:
wanaduru asalam aleykhum!!
Nimependa sana ulipotakla kujua msimamo wa wanaduru wengine juu ya EL.
LAKIN SWALI LA MSINGI JE KUNA CHUKI NDANI YETU AMA NI USHABIKI TUU??


Karibu dada yangu gfsonwin..

Kama ni chuki kwa Lowassa basi hizi chuki zimetokana na viongozi wa Chadema kutuaminisha kuwa Lowassa ni fisadi..
Kuna watu wanasema kuwa tatizo ni mfumo mimi swali langu ni je huo mfumo ndo ulikwenda kuchukua pesa benki na kulipa Richmond? au Escrow mfumo ndo ulibeba pesa kwenye mifuko ya Rambo? waliofanya hivyo ni watu ambao na Lowassa yumo (kama tulivyoaminishwa)

Na vita yetu ni Ufisadi na rushwa, Lowassa tuambiwa kuwa alikuwa anahonga wajumbe wa mkutano mkuu wazi wazi, tumeshuhudia Lowassa akichangia makanisa na misikiti pesa nyingi tu, tumeshuhudia watu wakisombwa kwenda kwenye mkutano wake Arusha na nk. Sasa huyu mtu ndo hawe mgombea urais kupitia Chadema? Kama Ukawa hawana mgombea urais kama ilivyoanda ya viongozi wa kiafrika kutoandaa viongozi mapema basi waende hata wakamwazime Makongoro walau hana harufu ya rushwa lakini si Lowassa..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mag3

Kwa kuwa mpaka sasa hakuna tangazo lolote rasmi juu ya Lowasa kujiunga rasmi na CHADEMA na kuchukua fomu ya kugombea urais sitachangia hili kwa sasa mpaka hapo itakapokuwa rasmi.

Nitarudi...

Changia ndugu yangu kwani wote tukikaa kimya hawa viongozi wa vyama watafanya wanavyotaka wao kwa manufaa ya matumbo yao. Ni lazima tuwambie ukweli mapema na tuonyeshe chuki zetu juu ya hiki kitu labda wanaweza kubadilika.

Tusikubali wanasiasa watufanye wanavyotaka wao.. wako hapo kwa ajili yetu na wako hapo kusiliza ni nini tunataka si vinginevyo..
 

Mkuu,

Unaweza kuonyesha uthibitisho kuwa mimi nimeshawahi kusema padri hawezi kuwa Rais?

Nadhani kwenye jukwaa hili kuna haja ya kuwa sober zaidi. Tuongee vitu tulivyo na uhakika navyo. Tukileta mambo ya mchafukoge kwenye jukwaa hili tutaliharibu.
 
Tunaambiwa Shetani alikuwa malaika akamuasi Mungu, kwa hiyo Shetani ni malaika muasi, tukaambiwa tumlaani nakumkemea kwa nguvu zote, kama shetani akitubu maasi yake akarudia kazi yake ya utumishi kwa Allah sisi tuliokuwa tukimlaani tutaficha wapi nyuso zetu?
 

Mpaka sasa kinachoendelea ni sarakasi za mitandaoni huyu kaposti hili na yule kapost vile... hakuna aliye wazi kusema once and for all nini kinachoendelea zaidi ya kauli za reja reja kwamba "UKAWA tunamkaribisha Lowasa etc etc........
Hata Lowasa mwenyewe alipotoka machinjioni Dodoma alisema ataitisha press conference kusema yake ya moyoni mpaka sasa kimyaa! Kila mwenye mdomo anasema lake na kila mwenye smart phone au computer anapost la kwake!

Sina uhakika lengo haswa la CHADEMA na UKAWA kwa ujumla ni nini lakini wanacheza gamble kubwa mno ambayo either inaweza kuwaingiza madarakani au kuwamaliza kabisa kisiasa endapo watashindwa!

Namna pekee ambayo ujio wa Lowasa unaweza kuwa wa maana ni pale ambapo ataamua kumwaga ugali na mboga yote kuhusu Richmond ili kukata mzizi wa fitina once and for all. Gumu zaidi ni kujikana uswahiba wake na kina Rostam, Karamagi, Prof wa milioni 10 za mboga... akifanikiwa haya basi ujio wake utakuwa ni wa impact kubwa kuweza kuiangusha CCM.
 
Siasa zetu zinachekesha sana wakati mwingine, amenifurahisha sana jana mwanasiasa msomi, Prof Lipumba

Akizungumza kuhusu harakati zilizokuwa zikiendeshwa kwamba "Lowassa ni fisadi na hasafishiki" Lipumba amesema, "…masuala ya ufisadi ni masuala ya mfumo, mpaka sasa hakuna mashtaka mahakamani dhidi ya Lowassa. Tunawakaribisha Watanzania wote kujiunga na UKAWA kupitia chama chochote," amesisitiza Lipumba.

Bila shaka sasa kwa Prof Lipumba uwepo wa kesi mahakamani ni kigezo muhimu cha kuzingatiwa kabla ya kumtuhumu mtu kwa ufisadi, lakini alipochukua fomu kugombea urais hicho kigezo cha kesi alikisahau

Profesa Ibrahim Lipumba amechukua fomu ya kugombea urais kupitia chama hicho na kuahidi kupambana na rushwa huku akishangaa kuwapo watuhumiwa wa ufisadi waliotakiwa kuwa mahabusu lakini wakichukua fomu za kuwania urais kupitia CCM, alisema watu hao wanastahili kuwa jela na mali zao zitaifishwe.




 

Mag3: Najibu kwa kifupi sana:

1 mpaka 6 mkandara yuko sahihi

7 na 8, napingana na mkandara; si kweli kuwa CCM walijiandaa, kumekuwa na several unplanned meetings within CCM to discuss this matter

9, Well sijajua maana imekaa kihisia zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…