Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Inawezekana wewe pia unachanganya vitu pia hapa.
Jumla ya Pato la Taifa-(GNP) ni sawa na jumla ya pato la taifa lakini unaongezea biashara ya ndani na biashara ya nje.Ukuaji Halisi-(Real Growth): Kwa vipengele vyote viwili jumla ya pato la utajiri (GDP) na ukuaji wa pato la utajiri (GNP), kama ukuaji ni asilimia 7% kwa mwaka, lakini mfumuko wa bei umekuwa asilimia 5% basi Ukuaji Halisi ungekuwa asilimia 2% tu kwa mwaka.

Majibu yako ni mfumo ndiyo unaotakiwa kuwajibika kama alivyosema Zitto.
Haswaa!
 
Na serikali kutokana na kodi zenu itawajibika kutoa huduma zake na ndipo maana sisi wananchi huishinikiza serikali juu kodi zetu tulolipa imezifanyia nini.

Asante. Kwanini sasa kiongozi wenu Zitto anadanganya umma kwamba wananchi wanatakiwa wapate gawio la GDP na nyie mkaunga mkono upotoshaji huu?

Kitaifa mchango wa sekta zote za uzalishaji na ujumla wake ndio Pato la Taifa sio kodi tunazolipa.
Ndio. Lakini naomba nikuulize:
Equation ya GDP ipo kama ifuatavyo:

GDP = C+I +G (X-M)

C = Consumption.
I = Investment.
G = Government Expenditure.
X = Exports
M = Import

Swali kwako:
Kwanini katika mlinganyo huo kuna "G" implying government expenditure?

Kwa maana nyingine Thamani ya bidhaa za uzalishaji kwa mkoa ndimo inatoka mshahara wako, kodi yako na kadhalika..
Ni kipi kinarudi kwenye jamii in terms of public finance kwa ajili ya kugharamia huduma za kijamii na kiuchumi? is it GDP?
 
Mchambuzi,
Wewe unazungumzia mapato ya Serikali au mapato ya Taifa? Tuelewane hapo kwanza..
Hoja ya msingi ni kwamba what makes a difference kwa wananchi in terms of maendeleo directly ni MAPATO YA SERIKALI (KODI) na sio PATO LA TAIFA (GDP). Zitto anapotosha na nyinyi mnadandia upotoshaji.
 
Inawezekana wewe pia unachanganya vitu pia hapa.
Jumla ya Pato la Taifa-(GNP) ni sawa na jumla ya pato la taifa lakini unaongezea biashara ya ndani na biashara ya nje.Ukuaji Halisi-(Real Growth): Kwa vipengele vyote viwili jumla ya pato la utajiri (GDP) na ukuaji wa pato la utajiri (GNP), kama ukuaji ni asilimia 7% kwa mwaka, lakini mfumuko wa bei umekuwa asilimia 5% basi Ukuaji Halisi ungekuwa asilimia 2% tu kwa mwaka.

Majibu yako ni mfumo ndiyo unaotakiwa kuwajibika kama alivyosema Zitto.

Naona kwenye tafsiri halisi ya GDP hatuelewani labda nikuambie hivi.

Ni ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za ndani ya nchi/ Gross Domestic Product (GDP) au ongezeko la bidhaa na huduma kutoka mwaka mmoja kwenda mwaka mwengine zinazotolewa na sekta mbalimbali ndani ya nchi.

Usikimbie maswali yangu. Based on your post 1613, nimekuuliza hivi:

  • Maswali kwako:

    1. Role ya serikali katika muktadha uliowasilisha hapo juu ni nini?
    2. Nani ni wa kuwajibika iwapo GDP ya mkoa mmoja ni ndogo kuliko GDP ya mkoa mwingine?
    3. Nani ni wa kuwajibika iwapo takwimu za GDP ya mkoa husika haziwi na mashiko kwa maisha ya wananchi walio wengi katika mkoa husika?
    4. Njia ipi ni sahihi kwa wananchi wa mkoa husika kufaidika na GDP katika muktadha wao wa uzalishaji?
    5. Mapato ya moja kwa moja kutoka katika uzalishaji wa bidhaa na huduma yanakwenda wapi? Unaweza kutufanyia mchanganuo?

    Umejibu kidogo kuhusu mfumo ndio wa kuwajibika. Kwanini Zitto anasema ni wananchi wa Arusha na Kilimanjaro?

Ritz,
Ni dhahiri kwamba hauwezi kupambana na hoja za kiuchumi. Utatafuta pa kupenya na ukikosa, utarudi kwenye matusi na harakati za kuhamisha goli. Ngoja nikupe shule kidogo. Serikali ina mapato kwa njia kuu mbili (mapato ya ndani ya taifa):

1. Mapato yatokanayo na kodi.
2. Mapato yasiyotokana na kodi.

*Tukianza na Mapato ya Kodi:
Haya ni pampoja na Corporate Income Tax, Personal Income Tax, Custom Duty, Excise Duty, Property Taxes, VAT na kodi nyinginezo za serikali kuu na serikali za mitaa.

*Tukija kwenye Mapato yasiyotokana na Kodi:
-Wizara ya mambo ya ndani kupitia uhamiaji na polisi (faini, ada za pasi za kusafiria etc).
-Wizara ya katiba (tozo na faini za mahakamani...).
-Wizara ya sayansi na tekinolojia (TCRA, Posta...).
-Wizara ya Viwanda na Biashara (Brela etc).
-Wizara ya uchukuzi (TCAA, TMA, TPA, ATC, TRL etc).
-Wizara ya Nishati (TPDC, EWURA etc).
-Ofisi ya Waziri Mkuu (Msajili wa vyama vya siasa etc).

Kote huku hakuna kodi inayokusanywa bali ada na tozo mbalimbali.

Mapato mengine huwa ni yale ya nje (Misaada + Mikopo) ambayo mjadala wake ni tofauti kabisa.

Nasubiri maswali yangu mengine niliyokuuliza awali.

Mchambuzi.

Mimi siyo mchumi nipo hapa kujifunza wala si kupambana na wewe ndiyo maana nakuiliza maswali sasa mwalimu wangu unaponipa majibu kiduchu nakuwa nashindwa kudadavua.
 
Last edited by a moderator:
Asante. Kwanini sasa kiongozi wenu Zitto anadanganya umma kwamba wananchi wanatakiwa wapate gawio la GDP na nyie mkaunga mkono upotoshaji huu?
Hakudanganya kitu pale, kwa kila GDP inavyopanda ndivyo inategemewa Kiuchumi maisha ya wananchi kupanda. Jinsi GDP inavyopanda ina maana kuna ongezeko la thamani ya pato na mara nyingi hutokana na kuwepo ongezeko la shughuli za uzalishaji. Mfano mdogo kama una shamba la hekari 10 la kahawa likazalisha Tsh Mil. 10 mwaka jana kisha mwaka huu tunategemea kuvuna Mil. 20 ina maana kuna ongezeko la shughuli za uzalishaji iwe shamba kubwa zaidi, wafanyakazi zaidi, mbegu nambolea zaidi, zana na kadhalika..

lakini ikitokea kuwepo ongezeko hilo pasipo kuzaa ajira, ununuzi wa bidhaa za uzalishaji, kuwepo na mzunguko unaotokana na ongezeko hilo lazima kuna tatizo la kiuchumi. Na hili ndilo aloangalia Zitto maana pengine wewe umetumia mashine na robot kuhudumia shamba ukakata nafasi za wafanyakazi kisha kahawa yako ukaiuza nje na kuweka fedha zako Uswiss! Mzunguko unakosekana na hivyo shambalako linakuwa halina faida kwa wananchi.

Utumiaji wako wa mashine na robot unaweza gharimu zaidi thamani ya uzalishaji wa mazao hayo na ukabadilisha bei ilokuwepo mwaka jana japo inategemea pia demand ya kahawa yako ndani na nje. Kwa maana nyingine Zitto analaani kitendo cha wewe kutumia mashine na robot ukawanyima wananchi ajira, ukaenda uza kahawa nje na kuweka fedha zako Uswiss...Hii ndio picha pana zaidi niloielewa mimi..

Ndio. Lakini naomba nikuulize:
Equation ya GDP ipo kama ifuatavyo:

Zk4vSxU0scvooQc2JBKJRCKRSCQSiUQikUgkEolEIpFIJBKJRCKRSCQSiUQikUgkEolEIpFIJBKJRCL5Uf4DTrymVhkh3t8AAAAASUVORK5CYII=

Swali kwako:
Kwanini katika mlinganyo huo kuna "G" implying government expenditure?
Kipande hiki hakikufunguka kwangu..

Ni kipi kinarudi kwenye jamii in terms of public finance kwa ajili ya kugharamia huduma za kijamii na kiuchumi? is it GDP?
hakuna kipi, huduma zinaweza tolewa na vyombo binafsi pia ni mchango wa pato la taifa. Hospital ya mtu binafsi ina mchango ktk GDP kama Hospital ya serikali, services hazina serikali pekee ni mjumuiko wa service zote isipokuwa tunalipa kodi ili yale mambo muhimu ya kiuchumi yashughulikiwe na serikali na ndio maana utakuta kodi zinatumiwa tofauti kwa kila nchi. Kwa mfano mfumo wa kodi na utoaji huduma wa serikali ya Tanzania, Canada na Marekani kote tunatofautiana, Sisi sehemu kubwa ya kodi yetu ipo katika matumizi ya serikali kubwa yenye mishahara mikubwa, posho na misafara badala ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi. Tunapishana vipaumbele vyetu kutokana na siasa zetu ama mazingira. Sisi hata pato la nje kama mikopo na misaada watu wanapiga kisu wakati wenzetu wako radhi wadhulumu nje, wazushe hata vita ili wauze mali zao na kupeleka mafao kwao..
 
  • GDP = C+I +G (X-M)

    C = Consumption.
    I = Investment.
    G = Government Expenditure.
    X = Exports
    M = Import

Kwa sababu Kodi ni sehemu ya pato la Taifa.. Ni kama kusema thamani ya gari lako ni gharama za ununuzi, Uagizaji, maintanance, kodi na ushuru wake. Hii ndio thamani ya Range ulopack hapo nje..Lol...
 
Hakudanganya kitu pale, kwa kila GDP inavyopanda ndiyo inategemewa Kiuchumi maisha ya wananchi hayo kupanda. Jinsi GDP inavyopanda ina maana kuna ongezeko la mapato na hivyo hivyo kuna onmgezeko la shughuli za uzalishaji. Mfano mdogo kama una shamba la hekari 10 la kahawa likazalisha Tsh Mil. 10 mwaka jana kisha mwaka huu tunategemea kuvuna Mil. 20 ina maana kuna ongezeko la shughuli za uzalishaji iwe shamba wafanyakazi zana na kadhalika..Ikitokea kuwepo ongezeko hilo pasipo kuzaa ajira zaidi lazima kuna tatizo, na hili ndilo aloangalia Zitto pengine wewe umetumia mashine na robot kuhudumia shamba ukakata nafasi za wafanyakazi. Pia utumiaji wako wa mashine na robot unaweza gharimu zaidi thamani ya uzalishaji wa mazao hayo na ukabadilisha bei ilokuwepo mwaka jana japo inategemea pia demand ya kahawa yako nje. Kwa maana nyingine Zitto analaani kitendo cha wewe kutumia mashine na robot ukawanyima wananchi ajira.

Wananchi wa Shinyanga wana mchango gani katika pato la mkoa? Unaweza kutuwekea takwimu hapa kwa mfano kwenye sekta ya kilimo, madini, uvuvi n.k? Based on those figures, what and how much are thry supposed to receive in return? Receive from who?

Kipande hiki hakikufunguka kwangu..[/quote
Nilimaanisha hivi:

  • Equation ya GDP ipo kama ifuatavyo:

    GDP = C+I +G (X-M)

    C = Consumption.
    I = Investment.
    G = Government Expenditure.
    X = Exports
    M = Import

    Swali kwako:
    Kwanini katika mlinganyo huo kuna "G" implying government expenditure?​

huduma zinaweza tolewa na vyombo binafsi pia ni mchango wa pato la taifa. Hospital ya mtu binafsi ina mchango ktk GDP kama Hospital ya serikali, services hazina serikali pekee ni mjumuiko wa service zote isipokuwa tunalipa kodi ili yale mambo muhimu kwetu yashughulikiwe na serikali na ndio maana utakuta kodi zinatumiwa tofauti kwa kila nchi. Kwa mfano mfumo wa kodi na utoaji huduma wa serikali ya Tanzania, Canada na Marekani kote ni tofauti, Sisi sehemu kubwa ya kodi io kaitka matumizi ya serikali kubwa badala ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi. Tunapishana vipaumbele vyetu kutokana na siasa zetu ama mazingira..

Hoja yako ya msingi hapa ni kwamba adui wa maendeleo kwa wananchi walio wengi ni KODI na sio GDP. Aidha kodi haikusanywi ipasavyo au inakusanywa lakini haitumiwi ipasavyo. Au nimekusoma vibaya?
 
Kwa sababu Kodi ni sehemu ya pato la Taifa.. Ni kama kusema thamani ya gari lako ni gharama za ununuzi, Uagizaji, maintanance, kodi na ushuru wake. Hii ndio thamani ya Range ulopack hapo nje..Lol...
Sio kweli. Kodi sio sehemu ya pato la taifa. Uhusiano wa Kodi na Pato la taifa sio wa moja kwa moja. Kilichokuwa sehemu ya pato la taifa ni matumizi ya serikali ambayo yametokana na mapato ya kodi na mapato yasiyotokana na kodi. Kwa maana nyingine rahisi, katika equation ya GDP huko juu, hakuna sehemu tunaona "TAX". Bali tunaona expenditure ya serikali (I) ambayo hutokana na mapato ya ndani kama vile mapato kodi na mapato yasiyokuwa ya kodi, na pia mapato ya nje kama vile mikopo na misaada).

njia nyingine rahisi ya kubaini kwamba kodi sio sehemu ya pato la taifa (GDP) ni kwa kuangalia logic ya kuwa na Tax to GDP ratio ambayo niliijadili jana kwa kina.

Maswali:
1. Je, wananchi wote wa mkoa kama Shinyanga wanachangia katika pato la taifa la mkoa (GDP)?
2. Je, wachangiaji wa pato la taifa huko mikoani kama Shinyanga, wote wanalipa kodi?
3. Wananchi wanaostahili kupata returns from contribution of GDP ni wananchi gani?
 
Hoja ya msingi ni kwamba what makes a difference kwa wananchi in terms of maendeleo directly ni MAPATO YA SERIKALI (KODI) na sio PATO LA TAIFA (GDP). Zitto anapotosha na nyinyi mnadandia upotoshaji.
No sio kweli, Kodi ni sehemu tu, kwa sababu kodi yetu inaelekezwa kwenye huduma (services) za serikali lakini kodi haikupi sehemu ya malazi ama kuweka chakula mezani. Mapato za uzalishaji kwa ujumla wake ndio kodi hupatikana humo. Hapa kwetu kama GDP ilivyo usanii ndivyo kodi ni usanii mwingine, hivi vinaweza kutosaidia wananchi ikiwa serikali ina sera mbovu kama nchi yetu.

Hivyo basi GDP yetu ni ya kisanii kama ilivyo kodi zetu maana wananchi wanalipishwa kodi hata kabla ya kuanza Uzalishaji, kodi za uagizaji magari ni kubwa kuliko thamani halisi ya gari hivyo kupandisha bei ya magari nchini, nyumba za upapngaji na kadhalika kila kitu ni usanii mtupu yaani wanakisia kama GDP kutokana na demand maana hatuna viwanda vya ndani. Hivyo inawezekana kabisa kama tuna mfumo mzuri GDP yetu ingekuwa sambamba na maisha ya wananchi na Kodi zetu zikatoa huduma bora zaidi maana wanakusanya hata kabla mfanyabiashara hujaelewa utavuna nini...
 
Hoja ya msingi ni kwamba what makes a difference kwa wananchi in terms of maendeleo directly ni MAPATO YA SERIKALI (KODI) na sio PATO LA TAIFA (GDP). Zitto anapotosha na nyinyi mnadandia upotoshaji.
Hebu soma kiduchu majibu ya Waziri Kigoda.

Mheshimiwa Spika, takwimu zinaonesha uchimbaji wa madini kwa mwaka 2005 ulichangia asilimia 16.1 ya ukuaji halisi wa Pato la Taifa (GDP), ikilinganishwa na asilimia 2.7 kufikia 2010. Hali hii inaonesha Serikali imekuwa ikipata mapato madogo kadiri miaka inavyoongezeka, tofauti na mategemeo hasa ikizingatiwa kuwa idadi ya migodi imeongezeka. Kamati inaishauri Serikali kuwa, sasa umefika wakati wa kuwabana wawekezaji kwenye Sekta ya Madini ili kuchangia Pato la Taifa.-

Huu mfano hai nimekupa sasa sijui Zitto kapotosha wapi.
 
Waziri anajichanganya pia. Sentensi ya kwanza anazungumzia pato la taifa (GDP), baadae anazungumzia pato la serikali (ambalo kimsingi ni kodi, lakini hafafanui hivyo kuacha hali ya mchanganyiko). Ni kwa sababu bunge limejaa mambumbumbu ndio maana mambo kama haya yanapigiwa makofi na kelele za "ndio".
 
No sio kweli, Kodi ni sehemu tu, kwa sababu kodi yetu inaelekezwa kwenye huduma (services) za serikali lakini kodi haikupi sehemu ya malazi ama kuweka chakula mezani. Mapato za uzalishaji kwa ujumla wake ndio kodi hupatikana humo. Hapa kwetu kama GDP ilivyo usanii ndivyo kodi ni usanii mwingine, hivi vinaweza kutosaidia wananchi ikiwa serikali ina sera mbovu kama nchi yetu.

Hivyo basi GDP yetu ni ya kisanii kama ilivyo kodi zetu maana wananchi wanalipishwa kodi hata kabla ya kuanza Uzalishaji, kodi za uagizaji magari ni kubwa kuliko thamani halisi ya gari hivyo kupandisha bei ya magari nchini, nyumba za upapngaji na kadhalika kila kitu ni usanii mtupu yaani wanakisia kama GDP kutokana na demand maana hatuna viwanda vya ndani. Hivyo inawezekana kabisa kama tuna mfumo mzuri GDP yetu ingekuwa sambamba na maisha ya wananchi na Kodi zetu zikatoa huduma bora zaidi maana wanakusanya hata kabla mfanyabiashara hujaelewa utavuna nini...

Labda nikuulize:

1. Pato la Taifa maana yake ni nini?
2. Composition ya pato la taifa ni nini?
3. Nini ni uhusiano baina ya mapato ya serikali (kodi) na pato la taifa?
4. Nini ni tofauti baina ya mapato ya serikali (kodi) na pato la taifa?

Nadhani ufafanuzi wako katika hili litaondoa sintofahamu iliyopo.
 
Usikimbie maswali yangu. Based on your post 1613, nimekuuliza hivi:

  • Maswali kwako:

    1. Role ya serikali katika muktadha uliowasilisha hapo juu ni nini?
    2. Nani ni wa kuwajibika iwapo GDP ya mkoa mmoja ni ndogo kuliko GDP ya mkoa mwingine?
    3. Nani ni wa kuwajibika iwapo takwimu za GDP ya mkoa husika haziwi na mashiko kwa maisha ya wananchi walio wengi katika mkoa husika?
    4. Njia ipi ni sahihi kwa wananchi wa mkoa husika kufaidika na GDP katika muktadha wao wa uzalishaji?
    5. Mapato ya moja kwa moja kutoka katika uzalishaji wa bidhaa na huduma yanakwenda wapi? Unaweza kutufanyia mchanganuo?

    Umejibu kidogo kuhusu mfumo ndio wa kuwajibika. Kwanini Zitto anasema ni wananchi wa Arusha na Kilimanjaro?

Mchambuzi.

Kwa faida ya wanaukumbi tuwekee ushahidi wa hiyo kauli yako kuwa Zitto amesema wawajibikaji ni wananchi wa Arusha na Kilimanjaro.
 
Last edited by a moderator:
Kwa sababu Kodi ni sehemu ya pato la Taifa.. Ni kama kusema thamani ya gari lako ni gharama za ununuzi, Uagizaji, maintanance, kodi na ushuru wake. Hii ndio thamani ya Range ulopack hapo nje..Lol...

Sitaki kuwaharibia mjadala lakini kuna kitu sijakielewa vizuri

Mkandara kuna sehemu umeandika kuwa Kodi si pato la Taifa bali ni pato la Serikali. Na hapo umeandika kuwa kodi ni sehemu ya pato la Taifa. Swali langu ni je kuna tofauti kati ya Kodi pato la taifa na kodi pato la serikali? Maana mie kwangu mie tunapongelea kuhusu kodi sioni tofauti kati ya serikali na taifa. Ufanunuzi wako tafadhali.

Swali la pili kwako na Mchambuzi

Tusema wanakijji wamelima shamba lao la mihogo na kuvuna mihongo yenye thamani ya mil.20, hizi mil 20 zitahesabika katika pato la Taifa!? (kama nimeelewa vizuri) Lakini hawa wanakijiji hizo mil. 20 wasipozilipia kodi labda kwa sababu ya msamaha ua ukwepaji kodi.. Je likapokuja swala la "gawio" katika maendeleo ya shughuli za jamii, je mgao utalenga hizo mil 20 au utalenga mchango wao wa kodi/ushuru?

(natumaini mtalielewa ili swali maana hizi taaluma zinawenyewe sisi wengine ni kuchota elimu tu)
 
Sio kweli. Kodi sio sehemu ya pato la taifa. Uhusiano wa Kodi na Pato la taifa sio wa moja kwa moja. Kilichokuwa sehemu ya pato la taifa ni matumizi ya serikali ambayo yametokana na mapato ya kodi na mapato yasiyotokana na kodi. Kwa maana nyingine rahisi, katika equation ya GDP huko juu, hakuna sehemu tunaona "TAX". Bali tunaona expenditure ya serikali (I) ambayo hutokana na mapato ya ndani kama vile mapato kodi na mapato yasiyokuwa ya kodi, na pia mapato ya nje kama vile mikopo na misaada).

njia nyingine rahisi ya kubaini kwamba kodi sio sehemu ya pato la taifa (GDP) ni kwa kuangalia logic ya kuwa na Tax to GDP ratio ambayo niliijadili jana kwa kina.

Maswali:
1. Je, wananchi wote wa mkoa kama Shinyanga wanachangia katika pato la taifa la mkoa (GDP)?
2. Je, wachangiaji wa pato la taifa huko mikoani kama Shinyanga, wote wanalipa kodi?
3. Wananchi wanaostahili kupata returns from contribution of GDP ni wananchi gani?
Mkuu mimi naona tunapishana lugha tu hapa. wanaposema Government Expenditure ni katika lugha ile ile ya makisio na ndio maana tunapanga bajeti ya nchi hata kabla hatujawa na fedha mkononi. Kwa hiyo bajeti walokaa mwaka huu kwa ajili ya 2015 hadi 2016 ni masikio ya matumizi ya serikali kwa mwaka kama tunavyokisia mwaka huu GDP itapanda kiasi gani lakini matokeo halisi ya GDP Kiuchumi yatategemea na mambo mengine muhimu kama mfumko wa bei na kadhalika. Hii ni dhana tu inayotangulia kwa kuthamisha mchango wa serikali katika kukuza GDP.

Hivyo kifupi tunapozungumzia kodi zetu, ni sehemu tu ya mapato mapana ya serikali ili kuiwezesha kutoa huduma zake, hivyo zile specific function za serikali katika uzalishaji ndizo huhesabiwa kama sehemu ya GDP. Kumbuka hapa tunazungumzia kodi za Shinyanga hivyo ndio maana tumechukulia swala hili kwa udogo wake badala ya kuzungumzia njia zote za mapato ya serikali kama sehemu ya GDP. Kwa hiyo matumizi ya serikali iwe vifaa vya kivita, shule, hospital, barabara, social welfare ni mchango wa serikali katika kukuza GDP japo unatokana na mapato mbali mbali mingine misaada na mikopo, lakini mwisho wa siku madeni haya yatalipwa na kodi hata kwa miaka 50 ijayo..
 
Mchambuzi.

Kwa faida ya wanaukumbi tuwekee ushahidi wa hiyo kauli yako kuwa Zitto amesema wawajibikaji ni wananchi wa Arusha na Kilimanjaro.

Mbona hoja hiyo ndio msingi wa hatua tuliyofikia leo katika uzi huu? Baada ya sisi kutoa hoja zenye kuonyesha kwamba kwamba Zitto alichanganya mambo, Zitto alipotosha, Zitto alitoa kauli za uchonganishi; Baada ya nyinyi kuona ukweli huo, sasa mnaanza kutafuta jinsi gani ya kumuokoa kwa kuomba ushahidi. Mbona ushahidi umetolewa humu, kuanzia video clips kama ile ya TUJITEGEMEE na sources nyingine nyingi? Ikafikia mahali mkaanza kujadili kwamba hakusema hayo point A bali Point B n.k? Mjadala huo endeleeni na akina Nguruvi3. Ninacho shukuru ni kwamba sasa mmekubali kwamba kulikuwa na kosa.
 
Last edited by a moderator:
Sitaki kuwaharibia mjadala lakini kuna kitu sijakielewa vizuri

Mkandara kuna sehemu umeandika kuwa Kodi si pato la Taifa bali ni pato la Serikali. Na hapo umeandika kuwa kodi ni sehemu ya pato la Taifa. Swali langu ni je kuna tofauti kati ya Kodi pato la taifa na kodi pato la serikali? Maana mie kwangu mie tunapongelea kuhusu kodi sioni tofauti kati ya serikali na taifa. Ufanunuzi wako tafadhali.

Swali la pili kwako na Mchambuzi

Tusema wanakijji wamelima shamba lao la mihogo na kuvuna mihongo yenye thamani ya mil.20, hizi mil 20 zitahesabika katika pato la Taifa!? (kama nimeelewa vizuri) Lakini hawa wanakijiji hizo mil. 20 wasipozilipia kodi labda kwa sababu ya msamaha ua ukwepaji kodi.. Je likapokuja swala la "gawio" katika maendeleo ya shughuli za jamii, je mgao utalenga hizo mil 20 au utalenga mchango wao wa kodi/ushuru?

(natumaini mtalielewa ili swali maana hizi taaluma zinawenyewe sisi wengine ni kuchota elimu tu)
Kwa sababu lugha alotumia Mchambuzi ni kama kusema Macho ndio sura ya mtu, nami nikasema hapana macho ni sehemu tu ya sura ya mtu. Macho sio sura, ila sura ni mjumuiko wa viungo vingi ikiwa ni pamoja na kope.. Lol na kama ulimsoma vizuri Mchambuzi aliendelea kukazania umuhimu wa macho wakati hata kipofu ana sura ila nikaeleza umuhimu wa macho katika kuona, unabakia pale pale kuwa ni mchago kubwa katika hisia za binadamu..

Swali la pili, kama Mchambuzi alivyosema hapo juu na kuonyesha matumizi ya serikani ni sehemu ya mchango wao ktk GDP ndivyo Zitto alichokuwa akizungumzia kwa matumaini kwamba ikiwa wao wanachangia kwa sehemu kubwa ya GDP lakini imeonyesha mchango mdogo wa serikali (Expenditure) ina maana hii ndio sababu kubwa ya Shinyanga kuwa chini. makuzi makubwa ya GDP ya SHY yatokana na vitu vingine kwa sababu serikali imeendelea kuchangia kiasi kidogo katika maisha yao ndio maana ile dhahabu imethaminishwa juu mchango wake lakini wananchi hawapati kitu na hivyo kuathiri hata mchango wao katika Kodi maana wengi wao hawana ajira.. Kifupi hakuna mzunguko ama trickle down ya kimaendeleo SHY..

Alinda
, Unaweza mtu kutoka familia tajiri sana lakini ukaishi maisha ya kimaskini ukilinganisha na ndugu zako, Yupo rafiki yangu mmoja anateswa hivyo kwa sababu ati mtoto wa nje japo yeye ndiye mfanyakazi mkubwa wa mzee. Hivyo napomtetea huyu mshikaji wangu sio kwa sababu nataka wale ndugu zake wanyimwe kitu, isipokuwa huyu anastahili kulipwa vizuri, kuishi vizuri kama nduguze na haitapunguza maisha ya ndugu zake kwa sababu fedha ipo isipokuwa zinatumiwa kwa mambo yasokuwa ya maana kama vitu vya anasa na kadhalika. Vile vile Shinyanga ingeweza kabisa kupata huduma bora kama serikali hii wangeacha kujilipa mishahara mikubwa, posho na misafara, Ufisadi wa mikataba isiyokuwa na tija ili kuhakikisha mikoa kama Shinyanga inapanda kiuchumi na hivyo kuboresha maisha ya wananchi wa mkoa huo wakati ikivutia wawekezaji zaidi..
 
Mbona hoja hiyo ndio msingi wa hatua tuliyofikia leo katika uzi huu? Baada ya sisi kutoa hoja zenye kuonyesha kwamba kwamba Zitto alichanganya mambo, Zitto alipotosha, Zitto alitoa kauli za uchonganishi; Baada ya nyinyi kuona ukweli huo, sasa mnaanza kutafuta jinsi gani ya kumuokoa kwa kuomba ushahidi. Mbona ushahidi umetolewa humu, kuanzia video clips kama ile ya TUJITEGEMEE na sources nyingine nyingi? Ikafikia mahali mkaanza kujadili kwamba hakusema hayo point A bali Point B n.k? Mjadala huo endeleeni na akina Nguruvi3. Ninacho shukuru ni kwamba sasa mmekubali kwamba kulikuwa na kosa.
Hamna ushahidi wowote ambao unaonyesha Zitto kasema wananchi wa Kilimanjaro na Arusha ndiyo wawajibikaji hata hiyo video ya Tabora hizo ni hisia zenu na chuki tu kumlisha maneno Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom