Mkuu,
Swali lako ni fupi lakkni limebeba mjadala mpana sana.
"Mtaalam" wetu wa masuala ya kisiasa
Nguruvi3 nadhani anaogopa urefu wa kina cha swali lako!Tuendelee kusubiri labda anakusanya vielelezo!Wahenga walisema "ukimya una mshindo"
Naam una mshindo! Nilichokisema nasimama nacho kwa ushahidi bila shaka.
Nilikuwa nasubiri kama kuna hoja nyingine nizipitie zote kwa ujumla
Kuanzishwa kwa ACT ilikuwa ni matokeo ya mtafaruku ndani ya Chadema.
Mtafaruku ulioanza kidogo kidogo kabla ya siri kufichuliwa na Mghamba baada ya kubainika anakiuza chama
Mtafaruku ulipelekea kufukuzwa kwa Zitto, Mghamba na Mkumbo Kitila na kuanzisha ACT-Wazalendo
Kabla ya hapo, tukiwa jamvini na siasa za nchi zikiwa huru tulimshauri Zitto kuwa na subira kwani muda ungetoa matokeo makubwa kuliko haraka alizokuwa nazo.
Watu walidhani ni 'ujana' wa Zitto bila kujua nini nyuma yake
Kile kilichoitwa 'waraka' kilifunua waliokuwa nyuma ya mpango huo akiwemo Mghamba na Prof Kitila
Walipounda ACT-Wazalendo, Mghamba, Kitila na Mwenyekiti Anna Mghwirwa walikuwa viongozi
Leo Kitila ni mwanachama mtiifu wa CCM. Mghamba ni mwanachama mtifu wa CCM
Anna Mghwirwa ni mwanachama na kada mtiifu wa CCM. Albert Msando ni kada kindaki ndaki wa Lumumba
Wote hao walikuwa ni nguzo ya ACT Wazalendo ambao leo tunajua haikuwa ACT ilikuwa ni 'mpini' wa kumaliza upinzani ulioanzia ndani ya Chadema, ukahamia ACT.
Baada ya kushindikana, wakarudi ''nyumbani'' kuendelea na majukumu ya kawaida wakimwacha Zitto
Ukimtazama Zitto na historia yake utabaini alikuwa anatumiwa bila kujijua na makada wa Lumumba kama 'mpini' wa kumaliza upinzani.
Kumbuka shoka lenyewe ni Lumumba walipo akina Mghamba, Msando, Kitila na Mghwirwa
Mara baada ya kuondoka ACT-Wazalendo picha halisi ya Zitto imeonekana.
Akiwa katika chama kidogo, bado amekubali kushirikiana na wenzake aliokorofishana nao siku za nyuma, akiendeleza harakati za upinzani. Hii ni maturity ya hali ya juu sana na nampa big up
Kuna mahali hapa JF niliandika ' ACT inafanya kazi ya upinzani' kuliko chama kikuu cha upinzani Chadema
Hoja yangu ilijikita namna ACT inavyo react katika masuala ya kitaifa na kimataifa
Baada ya makada kurudi nyumbani na kupewa nafasi zao, nampa Zitto ''benefit of doubt'' , kwamba, kuna mahali alipotezwa hasa baada ya kubaini nyuma yake alizingirwa na team Lumumba iliyokuwa kazini kikamilifu
Kwangu mimi simuangalii Zitto kama ACT, namuangalia kwa hoja zake na mantiki.
Nakubaliana naye 100% akiwa sahihi na natofautiana naye 100% inapobidi kwa mantiki na hoja
Nikiangalia nyuma, ushauri wangu kwa Zitto ulikuwa sahihi kabisa, nilichoshindwa kuelewa ni nguvu kubwa iliyokuwa nyuma yake ikiwa imebeba agenda za mtaa mkubwa wa Lumumba.
Kuna wakati namuona kama 'victim of circumstances'
Sasa nasimama wapi na ACT? ACT hii ya 'one man show' Zitto ni bora sana kuliko ile ya 'Mpini' wa Lumumba
Imeonyesha kukua na kuimarika licha ya udogo wake. Imejidhihiri katika kauli na matendo
Naiangalia kama future opposition party endapo hakutakuwa na 'remnant' kutoka mtaa wa Lumumba