"Mwalimu, post: 19590575, member: 11689"]Trump ana followers zaidi ya 23M kwa hiyo suala la post kupata likes 140k sio shida. Pia kutofautiana kimtazamo na majaji nayo sio shida na inaweza kutokea mara kwa mara.
Mkuu, umesema vema, Likes kama zinatumika ku ''qualify or quantify'' kauli katika mitandao kwakweli ni hatua mpya.
Nakumbuka walioamini Obama hakuzaliwa Marekani kutokana na kauli za Trump.
Namba inayoamini hivyo ikiwekwa mtandaoni ni zaidi ya milioni.
Kama ingekuwa na nafasi ya 'like' zingefika milioni.
Hilo lingefanya Obama asiwe rais wa Marekani! Sasa likes 140! kwakweli inatisha, tuachie hapo
Shida ya Trump ni anavyokabiliana na wote ambao wanatofautiana na yeye kimtazamo.
Kama hajakubaliana na uamuzi wa jaji haina shida lakini kufikia hatua ya kumdhihaki kwa kumwita "so called judge" ameonyesha kiwango kikubwa cha utoto kitu ambacho hakipaswi kuonyeshwa na mtu mzima yeyote sembuse rais wa taifa kubwa kama marekani. Na hii sio mara ya kwanza kufanya hivi, juzi hapa alimkatia simu waziri mkuu wa Australia baada ya kutokubaliana juu ya hoja za uhamiaji. Hakuna namna nyingine ya kuita tabia hii isipokuwa "utoto"!
Huyu ni Jaji wa pili kumdharau baada ya yule wa kesi ya chuo
Wiki iliyokwisha ali tweet Sally Yates ni Obama's AG.
Trump haelewi Jaji akishakuwa appointment anakuwa mtumishi wa umma si wa mtu.
Ni makosa kumwita Tillerson kama ''Trump's sec of state''
Republican kama akina Mitchell wanakuwa embarrassed na kauli zisizo na vipimo za Trump
Kauli hizo kwa upande mwingine zinamjengea sana heshima Obama
Juzi wakati wa black month history, Trump alikuwa busy akieleza mzozo wake na vyombo vya habari
Ni kama hakujua kwanini alikuwa pale na umuhimu wa siku hiyo
Kuna wanaosema ana uhuru wa kusema mawazo yake.
Ni kweli, lakini si Trump wa Tower au transition ni president kila analofanya liwe katika muktadha huo
Uhuru wa kusema unamweka mahali pagumu.
Aliulizwa kuhusu ushahidi wa wapiga kura haram milioni 3.5-5.
Utetezi wake ni sawa na mtu wa mtaani kwakweli. Hana back up ya suala analozungumzia
Akatoa kauli za exec order kuchunguza wapiga kura haramu.
Wenzake wakamwambia hata kama wapo hawafiki hata 5,000 kwa kuangalia kesi za nyuma
Kauli inapingwa na Republican ambao magavana wao ni wengi katika state ukilinganisha na Dem
Trump anajua hawezi kutetea hoja zake za nyuma. Anachokifanya ni kusingizia vyombo vya habari
Tatizo analoona ni vyombo hivyo kuweka kumbu kumbu naye hataki watu wakumbuke kasema nini
Kwa mfano, sasa hivi anatekeleza sera za Obama kwa Iran kikamilifu.
Huko nyuma alisema deal ni disaster akiaminisha umma ana mbadala mzuri ambao hadi sasa haupo
Ndivyo ilivyo kwa Obamacare ambayo hana karatasi hata moja aliyoandika ikaonekana hadi sasa
Usisahau suala la ukuta ambalo nalo limeshindikana na Mexico hawatalipa gharama ila wananchi wake
Katika mkutano wa mwisho na waandishi wakati wa Obama, wengi walisema watamkosa kwa utulivu, umakini na muhimu sana anavyoweza ku articulate policy na kuzi connect na public
Kinachoshangaza ni kuwa katika tweets, Trump anamsema Jaji kama kichekesho asiyejali usalama wa Taifa. Trump bado anadhani ukuu wake hauna ukomo.
Katika nchi inayoongozwa na constitution sheria ndizo zinatangulia na Jaji alisimamia hilo
Pamoja na kumkashfu bado Trump ametii amri ya Jaji kwa maana amri ya Mahakama bila shurti
Sasa anafuata mkondo wa sheria na pengine anaanza kuelewa maana ya mihimili miatatu huko US