Katika misingi ya haki, tunasema mtu hana hatia hadi ithibitishwe vinginevyo (presumption of innocence). Katika misingi hiyo muendesha mashtaka hawezi kumtuhumu (indict) mtu hadi awe na ushahidi wa kutosha. Akiwa nayo, mashtaka (prosecution) yanafuata mahakamani, halafu hatia (conviction) au hamna hatia (innocence).
Mueller hakumu-indict Trump katika ripoti yake. Kwa maana kwamba hakuhitimisha kuwa ushahidi aliokusanya unamtosha kumtuhumu kwa kosa la "obstruction." Badala yake hakutoa hitimisho kuhusiana na kesi hiyo.
"..we did not draw ultimate conclusions about the President's conduct."
Ukisoma vizuri conclusion nzima ya Mueller, hakutoa hitimisho la kusema kosa limetendwa kutokana na masuala magumu (difficult issues) ya matendo na dhamira ya Rais aliyokutana nayo, ambayo amesema yanahitaji kuwa resolved kwanza.
"The evidence we obtained about the President's actions and intent presents difficult issues that would need to be resolved if we were making a traditional prosecutorial judgement"
Hakuwa na haja ya kusema hili kwenye hitimisho lake kama lengo lake toka mwanzo lilikuwa ni kutaka utaratibu mwingine utumike kufanya maamuzi. Conclusion ndipo mahali ujumbe husika unapopatikana. Hakuna neno lolote kwenye conclusion ya Mueller lenye muelekeo wa kuitaka Congress ikaamue kuhusu obstruction.
Ukisoma Code of Federal Regulations ya mwaka 1999 na sababu za kushindwa ku-renew Ethics in Government Act ya mwaka 1977, utagundua kuwa AG amepewa mamlaka makubwa katika uteuzi na kumsimamia Special Counsel. Kwa kifupi AG ndiye Bosi wa Special Counsel.
Special Counsel aliandika ripoti akampa bosi wake, akisema amekutana na masuala magumu yanayohitaji kutatuliwa ili kutoa uamuzi fulani. AG kama Chief Prosecutor kwa kushirikiana na Deputy wake na OLC wakatatua masuala hayo na kuhitimisha kuwa ushahidi uliokusanywa hautoshelezi kumtuhumu Trump kwa obstruction.
Hakuna sehemu AG Barr amesema Trump hana hatia, hiyo ni tafsiri yako kama ilivyo kwa watu wengine. Bali Barr alichosema ni kwamba ushahidi uliokusanywa kwenye uchunguzi wa Special Counsel hautoshelezi kudai kuwa Rais amefanya kosa la obstruction.
"After reviewing the Special Counsel's final report on these issues.....Deputy Attorney General Rod Rosenstein and I have concluded that the evidence developed during the Special Counsel's investigation is not sufficient to establish that the President committed an obstruction-of-justice offense."
Mueller ndiye hakuwa na mamlaka ya kusema Trump hana hatia maana hiyo sio kazi yake.
"while this report does not conclude that the president committed a crime,
it also does not exonerate him.”
Prosecutor anafanya kazi zaidi ya indictment (kutuhumu mtu kuwa ana hatia), kwa maana kwamba anamshtaki (prosecution) mtuhumiwa kwa kosa fulani ili mahakama iamue kama kuna hatia au lah!
Basis ya hoja yako na kuweka screenshot ni kwamba hukubali kwamba prosector anam-prove mtu "guilty" na sio "innocent"!
Kama unaamini kwamba kwenye mfumo wa haki tuna-assume mtu hana hatia hadi ithibitishwe vinginevyo, prosecutor anawezaje kufanya kazi ya kuthibisha kuwa mtu hana hatia (kwa maana ya "exoneration")? Ina maana ali-assume ana hatia kabla?
Maelezo mazuri, wala hamna aliyesema Mueller anaweza kumshtaki Rais aliye madarakani, wala aliyepinga fairness principle kwa jinsi alivyoitumia Mueller.
Amesema hivyo kwenye ripoti yake? Amezungumzia hilo kwenye hitimisho lake? Alishindwaje hata kuandika hilo pendekezo?
Jambo la muhimu ni kwamba Mueller hajahitimisha kuhusu obatruction, sio kwa sababu ya utaratibu wa kikatiba unaohusu indictment na prosecution ya Rais aliye madarakani, hapana! Conclusion ya ripoti yake ipo wazi na inaelezea sababu wazi.
Mueller sio Special Counsel wa kwanza kumchunguza Rais aliye madarakani, Ken Starr alihitimisha uchunguzi wake kwa kupata ushahidi wa kutosha dhidi ya Bill Clinton.
Unadhani, Mueller angepata ushahidi wa kutosha (sufficient evidence) kwenye "conspiracy", conclusion yake ya Volume I angeiandikaje?
Endelea tu kuheshimu hizo 'rights' mkuu!
Pepripheral third parties sio watu ambao hawakupewa nafasi ya kujitetea, bali ni watu ambao hawakuwa charged na hivyo hawawezi kupata nafasi ya kujitetea.
Mkuu
Nguruvi3 mbona hujaonyesha sehemu niliposema underlying evidence zimepigwa mstari?