Mimi ningekuwa ni mshauri wa Biden, ningemshauri yeye aache kuropoka na atulie tu ila awe anawapa watu matumaini mazuri dhidi ya Pandemic kuwa akiwa madarakani, ataimarisha huduma za afya ili kuhakikisha Pandemic yoyoye haitaingiliana na maisha yao ya kila siku kwa vile hilo ni jambo linaloweza kufanywa na serikali yu.
Waamerika wote leo hii wanalijua hilo
Hawa wagombe wana changamoto kadhaa.
Biden analijua la kukaa kimya na amezungukwa na timu inayomshauri afanye hivyo.
Hata hivyo, Biden ana 'political gaffe' na kutotokea katika hadhira kutokana na Covid kunamsaidia sana.
Pili, Biden ana changamoto za kumpata VP. Kampeni yake imerudishiwa uhai na watu weusi wa Carolina.
Biden aliahidi VP mwanamke tena colored. Hiki ni kitanzi kwa namna fulani.
Katika orodha yake Senta Elizabeth Warren ambaye ni Mzungu.
Chaguo hilo litamweka pagumu na watu weusi wanaotaka tu mweusi.
Yupo Seneta Kamala Harris, ambaye Baba yake ni mweusi na mama yake ni Mhindi.
Kamala ana historia ya kuwa prosecutor jambo linalozua maswali kwa watu weusi.
Yupo Suzan Rice, Balozi UN na mshauri wa usalama wa Obama. Rice anaonekana kukubalika kwa namna zote, kwamba ni mweusi lakini pia ni msomi na mzoefu wa siasa za ngazi za juu za Marekani.
Yupo Stacey Adams ambaye aligombea Ugavana wa Georgia na kushindwa. Huyu amejipambanua sana kuhusu kuwa VP lakini hana uzoefu wa siasa za DC au Federal level. Anakubalika sana miongoni mwa weusi
Orodha inaendelea akiwemo gavana wa Michigan, Mayor wa Atlanta Ms Bottoms n.k.
Kwa ufupi , kutangaza kuwa atakuwa na VP mwanamke wa rangi ni kitanzi,ni lazima hilo liwe takwa na aliteeleze.
Sikuona kwanini Biden alitumia Turufu hiyo ambayo sasa inageuka kuwa shubiri.
Ni shubiri kwasababu ombi linageuka kuwa takwa na hana jinsi lazima atekeleze au atalekezwe.
Ni turufu mbaya kama ile ya kuunga mkono Black lives Matter (BLM).
Kundi la BLM ni zuri kiuharakati lakini linapoingia katika siasa ni kundi baya.
Ni kundi lenye watu ambao maono yao ni ya muda mfupi.
Hii haina maana hawana hoja, la hasha, bali hawana ujenzi wa hoja na mwelekeo mzuri. Nitafafanua
Baada ya mauaji ya George Flyod, makundi mbali mbali yaliridhika pasi na shaka lilikuwa tukio moja kati ya mengi ya ukatili dhidi ya weusi. Makampuni na taasisi zikalazmika kuchukua hatua kadhaa katika kujinasua na kashfa au ukimya wa kufumbia macho madhila hayo.
Maandamano dunia nzima yalilenga kuunga mkono weusi dhidi ya madhila.
Hata hivyo, BLM wakaenda mbali zaidi wakidai kuondolewa kwa ''sanamu' za watu mbali mbali kwa kile walichodai ni kuwakumbusha machungu ya utumwa. Hii iliambatana na kuvunjwa kwa masanamu na uharibifu mwingine.
Hakukuwepo ulazima wa kuondoa masanamu. Tatizo lililpo ni ubaguzi wa kimfumo ''systemic racism'.
Hivyo turufu ya BLM ingalikuwa kushinikiza mabadiliko ya mfumo na si kuvunja masanamu
Pili, BLM wanataka 'defund' ya Police, kwamba, bajeti za Polisi zikatwe.
Huu nao ni ujinga, Polisi ndio wanaolinda usalama kupunguza bajeti ni kuleta matatizo zaidi.
Ipo hoja kwamba Polisi ndio vinara wa mauaji ya weusi, ni ukweli na ukweli usiopingika.
Dawa ya kukabiliana na tatizo ni kubadili mfumo wa Polisi na sheria zinazowalinda na siyo kupunguza bajeti.
Tatu, BLM wanakuwa wakali mtu mweusi akiuawa. Hilo ni la kweli kwani maisha ya mtu mmoja ni makubwa sana kiasi cha kusema ni mtu mmoja. Hata hivyo, BLM wameshindwa kwenda maeneo kama Chicago ambako kwa wiki si chini ya watu 10 weusi wanauana wenyewe kwa wenyewe.
Kwanini BLM waone tukio moja moja wasione kinachoendelea Chicago?
Je, Polisi wa Chicago walipozira maeneo ya South nani anaumia?
Ni kwa mitaarufu hiyo, Biden anajifungamanisha na BLM. Hii ni liability
Kadiri miji inavyopata vurugu ndivyo kampeni yake inavyfungamanishwa na BLM na fujo nyingine.
Tumalizie kwa kusema, ukiacha gaffe kuna matatizo mawili makubwa kwa Biden.
Moja, uchaguzi wa VP utakaokidhi haja za makundi na haja ya mteuliwa kuwa Rais wakati wowote.
Pili, kundi la BLM ambalo kama ilivyo uchaguzi wa VP nalo linahitaji kuwa na ''shea'' katika kampeni ya Biden
Ni kundi linaloweza kumtishia ikiwa hatafanya abcd.
Je, Trump anaingia uchaguzi akiwa na mzigo gani? Inaendelea