TUJITEGEMEE, hivi huamini kabisa
blue wave ilivyoufunika huu uchaguzi uliopita?
Kama si hujuma ya
gerrymandering iliyofanywa na
Republicans hali ingekuwa mbaya sana kwao safari hii.
Democrats walitabiriwa kushinda majimbo
23 ya
House wamevuka hadi
35!
Nafasi zilizokuwa zikigombewa kwenye
Senate ni
35 tu kati ya
100 huku
65 wakiendelea na nafasi zao kusubiri uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2020 watetee nafasi zao.
Hali hiyo ndiyo imewanusuru Republicans kutokupoteza
Senate! Kwa
House ndiko nafasi zote zilikuwa zinagombewa na Republicans wamepoteza uongozi katika baraza hilo..
Mkuu
Mag3 unakumbuka asubuhi ya matokeo ndiyo siku Sessions alitumuliwa.
Haikuwa bahati mbaya, ilipangwa ili kufunika mijadala ya GOP na Trump walivyopoteza midterm
Haya mambo yanahitaji kufuatilia kwa analysis. Kusikia tu au kuambiwa inakuwa 'mtihani'
Hoja ya kwanza ilikuwa, Obama ameshindwa maeneo aliyo kampeni kutoka kwa Trump.
Alijua wapo wanaozoa tu bila tafakuri.
Well, Obama alishiriki ku set agenda ya House na Senate akiwaambia wajikite katika ACA au Obamacare. Alitembelea maeneo akifanya mikutano ya House na Senate
Republicans wakadakia hoja ya kuhifadhi '' pre-existing conditions' .
Wapiga kura waliwahoji, walipotaka kubomoa Obamacare walilenga nini?
Trump akaiingiza ajenda ya 'caravans'. Hoja hiyo ikabaki yake na si Republicans
Kukawa na disarray ya nini hasa ni agenda ya Republicans katika midterm
Rais Trump akatumia gerrymandering ku-target maseneta wa Dems ndani ya GOP States
Imemchukua zaidi ya wiki tatu akizunguka Virginia kwa Joe Munchin(D), Nevada kwa Dean Heller(D) , North Dakota kwa Heidi Heitkamp(D), Montana kwa John Tester (D), Arizona kwa Martha McSally (R), Florida kwa Bill Nelson (D) na Missisipi kwa Roger(R)
Katika wiki tatu hiki ndicho kilichotokea . Missisipi watarudia uchaguzi kwa sheria za state
Florida kura zinahesabiwa na ni likely Republicans watashinda
Katika ''vulnerable Dems'' tuliorodhesha, Dems wametetea Nevada, Virginia na Montana
Wameshinda Arizona ambako ni red state. Hadi leo hii tarehe 13 November ni kuwa Senate itakuwa na 51 kwa 47 kukiwa na baki ya Florida na Missisipi
Jitihada za wiki tatu za ku-flip Dems senate seat zimezaa matunda ya maseneta 2 au 3
Ni jitihada nzuri, Republicans wamebaki na uongozi wa Senate! Lakini zina tija?
Hilo limefanyika kwa ghara kubwa sana ya kupoteza House
Dems wanaelekea kuwa na majority ya 230+ ndani ya House.
Hili limekuja baada ya ku-flip Republicans districts zaidi ya 20.
GOP wamepoteza maeneo mengi yakiwemo ya Ugavana wa states na mabunge ya States
Katika ugavana, Dems wamepata mgavana 7 zaidi na sasa kuwa na 23 dhidi ya 25 ya GOP huku majimbo mawili yakiwa yanahesabu kura , Florida na Georgia.
Katika hilo la ugavana, Democrats wamekomboa viti zaidi ya 300 walivyopoteza (takribani 1000)
Hivyo mabunge ya state yaliyotawaliwa na GOP yana Dems wengi kwasasa
Magavana na wabunge wa state wana maana kubwa kwa ''gerrymandering ''kama ilivyojadiliwa
Ni vema kukumbuka, Wisconsin, Kansas, Michigan, New Mexico na Maine zimekwenda Dems
Tukirudi kwa wapiga kura,Republicans wamepoteza 'independents' kwa point 10+.
Wamepoteza kwa wanawake na wasomi wakibaki na wanaume na maeneo ya vijijini
Midterm imeonyesha jambo jingine, kwamba, maeneo kama Texas, Arizona ambayo ni red state yanaingiliwa na Dems. Swing states alizoshinda Rais Trump zinapoteza rangi yake
Ted Cruz aliomba msaada kwa state ya Texas ambayo ni Red state
Kwa mtazamo huo mfupi , kuangalia impact ya kitu kimoja kisicho na maana kama Kavanaugh,ni kujidanganya,kusoma tweets bila tafakuri na kutoelewa siasa za viwango vya viunga vya DC
Tusemezane