"General Mangi, post: 29887921, member: 190025"]Mimi nina maswli kadhaa
1. Je seneti haiwezi kuzuia baadhu ya mambo yanayoendelea House kusimama?
Mkuu, US wana Bunge(congress) lenye mfumo wa Bicameral ikimaanisha kuna upper chamber(senate) na Lower Chamber(House of reps) . Kwetu tuna Unicameral ambayo ni Bunge tu
Chamber hizi zinafanya kazi kwa ushirikiano ingawa senate ina majukumu zaidi ya kuthibitisha Wateuliwa
Senate haiwezi kuzuia shughuli za House na wala House haiwezi kuzuia shughuli za senate
Kinachoweza kutokea katika miswada ni upande mmoja kukwamisha upande mwingine
Ndiyo maana mswada wenye utata kwa pande mbili lazima ufanyiwe ''reconciliation''
Ni rahisi miswada kupita ikiwa chama kimoja kitamiliki House na senate
Spika wa House na senate majority leader wataongea lugha moja
Senate ina wajumbe wachache (100) akiwemo VP.
Ni wastani wa maseneta 2 kwa state, inaweza kuwa zaidi au pungufu kutokana na sheria kama za electoral college. State moja katika electoral college inaweza kuwa na wajumbe wengi bila kujali eneo lake
Pamoja na nguvu ya seneti ukilinganisha na House, Spika wa House ni mtu wa 3 katika ngazi za utawala
Rais ''asipokuwepo'' makamu wa Rais anafuata na kisha Spika. Hapa siyo senate majority leader
Ukilingaalia suala hili, utabaini walioweka walikuwa na makusudi.
Kwanza, Spika anawawakilishi wengi ndani ya House wanaotokana na wananchi moja kwa moja
Pili, kuhakikisha senate inabaki na nguvu za ''checks and balances'' hata Rais au VP wanapokuwa hawapo.
Miswada inayoweza kupewa 'veto' na congress kwamba Rais hana mamlaka ya kuibadili.
Tuliona katika vikwazo dhidi ya Russia ambapo Bunge liliona Trump anaweza kubadili au kuondoa vipengele. Ni kama mswada wenye ''seal''
Kwa ilivyo sasa House ni ya Dems ndiyo maana jana walipitisha mswada wa kufungua serikali
Senate ni ya Republicans bado wanasita kujadili hilo kwani ni kumweka Rais katika wakati mgumu
2. Rais hana uwezo wa kuivunja house?
Walioandika katiba ya US zama hizo wanasema Rais anachaguliwa kwa electoral college.
Senator na House rep wanachaguliwa moja kwa moja na wananchi.Rais hawezi kuvunja ''Congress'
Mifumo inayoweza kuvunja bunge ni ile ya Waziri Mkuu kuwa kiongozi Bungeni kama UK , Canada, n.k.
Endapo hataungwa mkono, au atapoteza kura ya imani basi jawabu ni kuvunja Bunge na kuitisha uchaguzi
Kwetu sisi mfumo umechukua huku na kule kwamba Rais ni kiongozi wa state na Government kama ilivyo US, lakini bunge letu ni la mfumo wa commonwealth. Hili nalo lilitakiwa kuangaliwa katika katiba
3. Kama kuna baadhi ya mambo yamekwama house mfn miswada kushindwa kupita, bajeti kukwama, Seneti haiwezi kupitisha?
Jibu lake ni kama nilivyoeleza awali
Ikumbukwe pamoja na uwepo wa Congress, Rais amepewa nguvu za kutekeleza mambo kadhaa bila ruhusa ikiitwa executive Order. Mambo hayo yameaanishwa kikatiba na yakikiukwa mhimili wa mahakama unatafsiri
Kuna shauri mahakamu kuu. Obama alitumia executive order kuruhusu wakazi (DACA) kupata muda zaidi wa kuishi US. Wapo wanaosema hiyo si sehemu ya mamlaka ya executive order, wamelifikishamahakamani
Rais pia amepewa kura ya 'veto', anaweza kuukataa mswada hata kama umepitishwa na senate na House
Senate nayo ina utaratibu wa mambo yanayoweza kupitishwa kwa simple majority na yanayohitaji 60 votes
Kwa maana kuwa ili kupata 60 kwa mgawanyo uliopo ni lazima suala likubaliwe 'bipartisan'
Hii si sheria ni kanuni zinazotungwa na senate na zinaweza kubadilishwa kwa kile wanachotania 'nuke option'
Kwa kuiangalia katiba ya US mfumo wao umesukwa kwa kutambua mihimili mitatu ya nchi ikiwa huru
Ni mfumo unaozingatia mgawanyo wa madaraka na unalinda kila upande kisheria
Congress inaweza kumuondoa Rais madarakani kwa makosa.
Mchakato 'process' hiyo si rahisi kama inavyodhaniwa.
Ni lazima kuwe na 'article of impeachment' ipitishwe na House na kisha ipate 2/3 ya maseneta
Kwa ujumla wa maseneta 100, ni lazima wapatikane 67
Kwa hali ya senate ya sasa ambayo ni takribani 47 kwa 53 , maana yake ni kuwa kama Dems watataka 'impeachment' kwa Trump lazima wapate Republicans 20 kuwaunga mkono
Hili halimaanishi haiwezekani, lakini lazima kuwepo na hoja za msingi za kufanya hivyo
Hoja hizo ndizo zinamtia Kiwewe Rais Trump na ''Russia''.
Kwamba, yanaweza kufumuliwa mambo yatakayosababisha GOP wamwache kama ilivyokuwa kwa Rais Nixon
Nixon alijiuzulu kwa kuwa maseneta wa Republicans walimuacha na kujiunga na Dems kwa uzito wa kosa
Hivyo, aliona ni vema ajiuzulu kwani asingeweza kuhimili kishindo
Kwa upande wa Majaji nao ni hivyo hivyo.
Huteuliwa na Rais aliyeko madarakani, huthibitishwa na seneti. Wakishakuwa majaji hiyo ni kwa maisha.
Kwamba, kuwaondoa kirahisi ni jambo gumu sana linalohitaji mchakato wa kimahakama
Lakini pia mfumo wao umetengenezwa kuhakikisha watendaji wanawajibika kwa Rais tu bali na congress. Kwamba wanaweza kuitwa na kuhojiwa na Bunge
Unaona wakuu wa FBI, Wakuu wa CIA na Intel community, Reserve bank n.k wakiitwa kufafanua hoja
Minyukano unayoiona US ni 'health' na ndiyo maana taifa hilo linaendelea.
Kwamba, kuna mifumo iliyotengenezwa kuhakikisha nchi inakwenda si kwa matakwa bali kwa mujibu wa katiba